Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru, Dkt. Bakari George, amewapongeza watumishi wa chuo hicho kwa jinsi wanavyotekeleza vizuri majukumu yao.

Dkt. Bakari ametoa pongezi hizo leo Aprili 30, 2025 ikiwa ni ujumbe maalum wa Mkuu wa Chuo kwa Watumishi wa TICD kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani itakayoadhimishwa Mei 1, 2025.

Katika hotuba yake kwa watumishi, Dkt. Bakari amesisitiza mambo anuai kwa ajili ya kuimarisha utendaji na kuleta matokeo chanya. 

"Nawapongeza [kila mmoja] kwa kufanya kazi kwa bidii kwa kipindi cha 2024/2025. Natoa rai tuendelee kutekeleza majukumu yetu kwa bidii na uadilifu", amesisitiza Dkt. Bakari.

" Lakini naomba kuwasisitiza kuwa mwaka huu [2025] ni mwaka wa uchaguzi mkuu hapa nchini kwetu. Hivyo twende tukajiandishe na tukapige kura kama ilivyo kauli mbiu ya maadhimisho ya Mei Mosi, 2025", ameeleza Dkt. Bakari.

Nao viongozi wengine waliopata fursa ya kutoa salamu katika kikao hicho akiwemo Bi. Janeth Zemba, Kaimu Mkuu wa Chuo - Mipango, Fedha na Utawala na Dkt. Rose Kiwia - Kaimu Mkurugenzi wa Taaluma na Bw. Dickson Lukumay - Mwenyekiti wa THTU - TICD na Bw. Clement Berege - Meneja Rasilimali Watu, wameungana na Mkuu wa Chuo kuwapongeza watumishi wa TICD kwa jinsi ambavyo wanajituma katika kutekeleza majukumu yao.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Chuo amewapatia zawadi ya vyeti na fedha watumishi hodari wa chuo kwa mwaka 2024/2025.

















Share To:

Post A Comment: