Zoezi la Uhawilishaji fedha za walengwa Kaya za mpango katika dirisha la Novemba/Disemba 2023 limefanyika leo tarehe 26 Machi, 2024 Wilaya ya Ngorongoro katika kijiji cha Lopolun ambapo jumla ya Kaya 140 zimenufaika.

Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe. Kanali Wilson Sakulo pamoja na mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro na Mratibu wa TASAF Wilaya Bw. Thomas Nade,  wamefika katika Ofisi ya Kijiji cha Lopolun Kata ya Olorien Magaiduru kushuhudia uendeshaji wa zoezi hilo ukifanyika, huku kiasi cha shilingi 6, 750, 000.00 kikitolewa kwa kaya 140.

Ikumbukwe Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa kiasi cha shilingi 442, 540, 000.00 za kitanzania katika Vijiji 68 wilayani Ngorongoro kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii -TASAF

Mfuko huu wa TASAF ulianzishwa na Serikali mwaka 2000, ikiwa ni moja ya mbinu za kutokomeza umasikini.





Share To:

Post A Comment: