KAHAMA
Wanafunzi wa shule ya sekondari Rwepas iliyopo manispaa ya kahama wamefanya ziara ya kimasomo na utalii katika hifadhi ya wanyama Jambo na kiwanda cha Jambo mkoani Shinyqnga pamoja na kisiwa cha saa nane kilichopo jijini Mwanza.
Wakiwa katika kiwanda cha Jambo waanfunzi hao wamepata fursa ya kutembea kiwanda cha Jambo katika sekta ya uzlishaji Maji,Mikate,Juisi ,Maji na Iscreem.
Wakiwa katika eneo la kiwanda wamefundishwa namna ya shughuli za Uzalishaji wa bidhaa zote za kiwanda cha Jambo.
Katika hatua nyingine wanafunzi walipata nafasi ya kutembelea hifadhi ya Jambo na kuona wanyama na ndege mbali.bali waliofugwa katika eneo hilo pamoja na kijifunza tabia zao.
Baada ya hapo wanafunzi hao walisafiri hadi jijini Mwanza na kutembelea hifadhi ya taifa ya kisiwa cha saa nane kilichopo katikati ya ziwa victoria.
Wakiwa eneo hilo wamejifunza historia ya kisiwa hicho pamoja na kutembea vivutio tofauti vilivyopo katika kisiwa hicho.
Baada ya ziara hiyo wanafunzi hao wameushukuru uongozi wa Shule ya Rwepas kwa kuwapa muda wa kusafiri na kujifunza mambo mbalimbali nje ya shule.
"Tunashukuru sana uongozi wa Shule yetu ya Rwepas kwa kutupa fursa ya kujifunza mambo mbalimbali kwa vitendo,tumeona simba na wanyama wengine pamoja na kujifunza mambo kadha wa kadha" Wamesema wanafunzi hao.











Post A Comment: