.
NA DENIS CHAMBI TANGA.
MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt.Batilda Burian amewasisitiza watumishi wa umma, watendaji wa taasisi pamoja na wakurugenzi wa halmashauri zote mkoani humo kutambua thamani ya fedha zinazoteolewa na serikali kwaajili utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kuhakikisha kuwa wanazuia ubadhilifu fedha na mianya yote ya rushwa ambayo inaweza kuwa kikwazo katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Akitoa rai hiyo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Tanga, mkuu wa wilaya ya Handeni Salum Nyamwese katika warsha ya wadau wa usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoa wa Tanga iliyoandaliwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU amewataka kuonyesha uzalendo uwajibikaji pamoja na kutokuwa sababu ya kuzuia maendeleo kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa mkoani humo.

"Rushwa ni adui mkubwa wa maendeleo ya Taifa lolote, kuhujumu matumizi sahihi ya rasilimali za umma, kudhoofisha ubora wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kupunguza ufanisi wa utoaji wa huduma kwa wananchi na kuondoa imani kwa wananchi , taasisi za serikali serikali kwa ujumla"
"Hatuwezi kufikia malengo ya maendeleo ambayo tumejiwekea kufikia kwenye dira ya maendeleo ya mwaka 2050 ikiwa tutaruhusu rushwa, ubadhilifu , ufisadi na ukiukwaji wa taratibu kuendelea" amesema Nyamwese

"Mapambano dhidi ya rushwa sio jukumu la TAKUKURU pekee mapambano haya ni ya kwetu sisi sote ambao tuna wajibu Kila kiongozi na Kila mtishi kwenye eneo lake kushiriki katika mapambano dhidi ya rushwa na hii inaakisi kaulimbiu ya kuzuia rushwa ni jukumu lako na langu tutimize wajibu wetu" amesisitiza.
Amesema serikali inautazama mkoa wa Tanga kama kitomvu cha biashara na utakaowavutia wawekezaji mbalimbali kutoka nje ya nchi kupitia miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo bomba la mafuta , ujenzi wa barabara inayotoka Tanga Hadi Dar es salaam pamoja na uboreshaji wa bandari ambapo kupitia fedha zilizoletwa ndani ya miaka mitano takribani Trillion 3.17 hazitokuwa na maana kama watendaji wa wasimamizi wa miradi hiyo hawatawajibika kikamilifu kwenye nafasi zao.

"Rais ametuamini na kutukabidhi dhamana ya kusimamia rasilimali za umma kwa niaba ya wananchi, hizo fedha zinazokuja na kupelekwa kwenye miradi hatuna budi kuonyesha kwamba imani hiyo hajaiweka mahali pasipo sahihi Kila moja wetu awajinike kikamilifu katika kufanya kazi kwa weledi ubadhilifu na uzalendo wa hali ya juu sisi kama watendaji kazi kubwa tuliyonayo ni kidaiwa matokeo" ameongeza Nyamwese.
Awali akizungumza mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Tanga 'TAKUKURU' Ramadhani Ndwatah amesema kuwa wamefanikiwa kufanya tahmini na kupitia miradi yote inayotekelezwa ndani ya mkoa ambapo wamebaini baadhi ya changamoto zilizochangiwa na usimamizi mbovu, ucheleweshwaji wa miradi na matumizi yasiyosahihi ya fedha zilizotolewa kwenye miradi husika ambapo iliweza kuchukua hatua kisheria .
" Licha ya mafanikio yaliyopatikana kwenye miradi ya maendeleo lakini bado kuna changamoto ya udhaifu katika utekelezaji wa miradi ucheleweshwaji wa miradi kwa baadhi ya wadau wenye dhamana, kuongeza gharama zisizo za lazima na kupunguza manufaa yanahotarajiwa kwa wananchi"
"Kutokana na changamoto hizo zilizojitoleza tumeona ni vyema kukaa na wadau wa usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili tuweze kukumbuahana kuhusu wajibu wao katika usimamizi na utekelezaji wa programu na miradi inayotekelezwa katika maeneo yetu" amesema Ndwatah.

Amewataka wadau wote wenye dhamana ya usimamizi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa kushirikiana kikamilifu na TAKUKURU ili kuweza kutimiza adhima ya serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo kupitia miradi inayotekelezwa kwenye maendeleo mbalimbali.
Akizungumza katika warsha hiyo mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Tanga mhandishi Juma Hamsini ameiomba serikali kupitia mamlaka za serikali tawala za mikoa na serikali za mitaa 'TAMUSEMI' mara wanapopeleka BOQ za ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo madarasa kuzingatia thamani halisi ya vifaa vinavyotumika kwenye miradi husika.

Post A Comment: