Na.Ashura Mohamed - Arusha.

Maonesho ya Karibu- KiliFair yamefunguliwa rasmi Jijini Arusha ambapo pamoja na kuchangia ukuaji wa pato la taifa Jukwaa hilo linatahwa kama kitovu cha kukutanisha wauzaji na waonenyeshaji kutoka mataifa mbali mbali barani Afrika

Maonesho hayo ambayo ambayo yanazidi kukua mwaka hadi mwaka yanawakutanisha wadau wa sekta ya utalii barani Afrika na Dunia kwa Ujumla kwa lengo la kutangeneza mnyororo wa Uchumi ndani ya sekta hiyo ili kuendelea kufanya vizuri zaidi,ambapo jukwaa hilo  huwakutanisha wadau wa ndani na nje ya nchi  ambao wameendelea kuwekeza na kuchagiza ongezeko la watalii katika Hifadhi za Taifa nchini.

Akifungua Maonesho hayo  Juni 05, 2026 katika Viwanja vya Magereza jijini Arusha, Mkurugenzi wa Utalii Dkt. Thereza Mugobi kwa niaba ya Waziri waMaliasili na Utalii alisema kuwa Karibu-KiliFair ni zaidi ya maonesho,ambao ni  uwekezaji wa kimkakati katika mustakabali wa utalii wa Tanzania. 

Dkt.Mugobi amesema kuwa Uhusiano huo wa kibiashara ulioanzishwa katika jukwaa hilo la Karibu KiliFair umezalisha ushirikiano mpya, kuongeza idadi ya watalii wanaowasili nchini, kuvutia uwekezaji, kutengeneza ajira, na kuimarisha maisha ya jamii zinazotegemea utalii. 

"Serikali itaendelea kuwekeza katika miundombinu ya utalii ikiwemo malazi, viwanja vya ndege, barabara ili kuboresha uzoefu wa watalii na kuwafikisha katika maeneo mbalimbali yenye vivutio kwa urahisi,pia Wizara itaendelea kutangaza vivutio vyake kupitia njia za kidijitali ili kuyafikia masoko mbalimbali duniani." Amesema Dkt. Mugobi.

Naye  mwakilishi kutoka “TATO” Wilbard Chambulo, amesema kuwa maonesho haya ni daraja linalounganisha wadau wa ndani ambao ni mawakala wa utalii na waongoza watalii pamoja na mawakala wa kimataifa kutoka katika mabara yote duniani.

Mkurugenzi Mwenza wa Karibu-KiliFair, Dominic Shoo, amesema ongezeko la washiriki kutoka mataifa mbalimbali ni ishara kuwa Tanzania imeendelea kujijengea heshima kama kitovu muhimu cha biashara ya utalii katika ukanda wa Afrika Mashariki

Shoo ameongeza kuwa ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi utaendelea kuwa nguzo muhimu katika juhudi za kuitangaza Tanzania na kuongeza mchango wa utalii katika uchumi wa taifa

Karibu-KiliFair imeendelea kuwa moja ya maonesho makubwa zaidi ya utalii katika Afrika Mashariki, yakitoa nafasi kwa wadau kutangaza vivutio vya utalii, kujenga mitandao ya biashara na kuibua fursa mpya za uwekezaji ndani ya sekta hiyo.

Maonesho haya yatamalizika kesho Jumapili June 07 ambapo mwaka huu yamekutanisha zaidi ya watu 1000 kutoka mataifa mbali mbali.







Share To:

Post A Comment: