Articles by "MAGENDO"
Showing posts with label MAGENDO. Show all posts

 

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha  ACP-Justine Masejo akizungumza na waandishi wa habari

Na Woinde Shizza, -ARUSHA
JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha kwa kipindi cha mwezi januari hadi Machi 2021, lilifanya operesheni maalum ya kupambana na madawa ya kulevya katika mkoa wa Arusha ambapo limefanikiwa kukamata watuhumiwa 157waliokutwa na madawa ya kulevya aina ya Heroine, Bhangi na Mirungi.

Akionge na waandishi wa habari Kamanda w polisi mkoa wa Arusha ACP-Justine Masejo alisema kuwa kufuatia Operesheni hiyo walifanikiwa kukamata watuhumiwa 12 wote wa Kiume wakiwa na madawa ya kulevya aina ya Heroine kiasi cha gramu 536 na jumla ya kesi 11 zimefunguliwa na zipo katika hatua mbalimbali.

Alisema kwa upande wa madawa ya kulevya aina ya bhangi, kesi 81 zilifunguliwa ambapo jumla ya kilogramu 114 na gramu 624 zilipatikana pamoja na watuhumiwa 87 kukamatwa kati yao wanaume 76 na wanawake 11 huku akibainisha kuwa kesi hizo zipo katika hatua mbalimbali za kiupelelezi.

"Aidha katika operesheni hiyo tulifanikiwa kupata kilogramu 271 za Mirungi
ambapo jumla ya kesi 49 na watuhumiwa 58 walikamatwa kati yao wa
kiume 53 na wa kike ni 05 kesi hizo pia zipo katika hatua mbalimbali za
upelelezi."Alisema

Alibainisha kuwa jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linaendelea na operesheni kali dhidi ya wananchi wanaojihusisha na madawa ya kulevya pamoja na matumizi na biashara ya madawa ya kulevya na kusema kuwa hawata sita kuwachukulia hatua kali za kisheria pindi tutakapo wakamata ambapo pia aliwaomba wananchi kushirikiana na nao ilikutokomeza kabisa matumizi na Biashara ya madawa ya kulevya

Alitoa onyo kwa baadhi ya watu wachache wanaojihusisha na matumizi na biashara ya madawa ya kulevya kuacha mara moja biashara hiyo ya madawa ya kulevya ambapo aliwaomba wananchi wa mkoa wa Arusha kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa zinazohusiana na uhalifu na wahalifu ili mkoa uendele kuwa shwari asanteni.

 Na Mwandishi wetu Mihambwe

Zoezi la uandikishwaji na uboreshwaji wa Wapiga kura kwenye daftari la kudumu la Wapiga kura limeenda vyema kwa amani na utulivu.

Hayo yamejidhihirisha kwenye ziara aliyoifanya Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu alipotembelea na kukagua vituo mbalimbali vya uandikishaji ambapo alijionea amani na utulivu ikitawala huku Watu wengi wenye sifa wakijitokeza kuandikisha na wengine kufanya maboresho ya taarifa zao.

"Huu ni mzunguko wa awamu ya pili ya uandikishaji ambapo amani imetawala, Wananchi wakijitokeza kwa wingi kujiandikisha na wengine kuboresha taarifa zao kwenye daftari la kudumu ili wapate sifa ya kuwachagua viongozi wanaowataka kwenye uchaguzi mkuu. Makundi rika ya jinsia zote wamejitokeza." Alisema Gavana Shilatu.

Katika ziara hiyo Gavana Shilatu aliambatana na baadhi ya Wajumbe kamati ya ulinzi na usalama ya Tarafa ambapo Wananchi wengi wamepongeza zoezi lilivyoendeshwa na kusimamiwa vyema ndani ya Tarafa ya Mihambwe.

 Watoto waishio katika mazingira hatarishi kutoka Kituo cha Safina mkoani Singida wakifurahia jambo pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya SPRF muda mfupi baada ya kupata chakula kwenye maadhimisho ya miaka 5 ya Taasisi hiyo.
 Mmoja wa wafanyakazi wa Taasisi ya SPRF,  Issa Hassan (kulia) akiteta jambo na Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa Mandewa kwenye maadhimisho ya miaka mitano ya taasisi hiyo jana.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya SPRF, Dkt. Suleiman Muttani, akizungumza jambo na Katibu wa Taasisi hiyo Dkt. Mwajuma Ulaya na Mwenyekiti wa Sauti ya Mwanamke Kijiji cha Kipumbwiko Mwajuma Suleiman kwenye moja ya shughuli za maadhimisho hayo.
 Afisa Takwimu wa SPRF, Boniventure Kagenzi akiteta jambo na muuguzi wa hospitali ya Rufaa Mandewa kwenye maadhimisho ya miaka mitano ya taasisi hiyo jana.
 Afisa Ufuatiliaji wa SPRF, Mwedinuhu Beleko, akiteta jambo na muuguzi wa hospitali ya Rufaa Mandewa kwenye maadhimisho ya miaka mitano ya taasisi hiyo.
 Katibu wa Taasisi ya SPRF, Dkt Mwajuma Ulaya akizungumza na watoto wa kituo cha watoto yatima na waishio kwenye mazingira magumu cha Safina (hawapo pichani). Kushoto ni Mwanasheria wa taasisi hiyo,  Paul Kigeje.

Mkurugenzi wa SPRF, Dkt Suleiman Muttani akikabidhi zawadi ya taulo za kijani ambazo zinaaminika kuwa salama zaidi kwa matumizi ya watoto wachanga badala kutumia nguo za mama. Zoezi hilo lilifanyika ndani ya Hospitali ya Rufaa ya Mandewa mkoani hapa kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 5 ya SPRF.
Na Mwandishi Wetu, Singida

TAASISI isiyo ya kiserikali ya Stars of Poverty Rescue Foundation (SPRF)  hatimaye imeadhimisha miaka mitano tangu kuanzishwa kwake huku ikitekeleza kwa vitendo malengo endelevu ya maendeleo kitaifa na kidunia sambamba na kujenga dhamira yenye taswira chanya kwa jamii, hususan uhamasishaji wa kina dhidi ukatili wa kijinsia kwa mwanamke na mtoto wa kike

Akizungumza muda mfupi baada ya kukabidhi zawadi ya taulo za kijani kwa ajili ya kuwafunika watoto waliozaliwa kabla ya umri‘ njiti,’ ndani ya Hospitali ya Rufaa ya Mandewa mkoani hapa jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo DkSuleimani Muttani alisema azma iliyopo ni kuendelea kusaidiana na serikali kutekeleza Mkukuta kama suluhisho la gharama za umaskini


SPRF ilipata pia nafasi ya kujumuika na kupata chakula cha mchana na watoto yatima na waishio kwenye mazingira hatarishi wa kituo cha Safina mkoani hapa kabla ya kuanza hafla ya maadhimisho hayo yaliyokutanisha viongozi mbalimbali wa dini, jamii na serikali, wakiwemo watu mashuhuri


“Tunawashukuru SPRF kwa kutukumbuka na kutenga muda wao kuja kula chakula cha mchana pamoja nasi, Mwenyezi Mungu awabariki sana…mana wengine ni matajiri na wana uwezo lakini huwa hawatukumbuki,” alisema Ndahani Julius, mmoja wa watoto wanaotoka kituo cha watoto yatima cha Safina mkoani hapa


Muttani alisema Malengo mengine ya taasisi hiyo, ambayo miradi yake ipo chini ya ufadhili wa Foundation for Civil Society (FCS), ni kukuza ushirikiano miongoni mwa wadau na jamii, taasisi za kitaifa na kimataifa katika kutokomeza umaskini wa kipato nchini na kwingineko, sambamba na kuimarisha uwezo wa kitaasisi katika kukua na kutekeleza program endelevu

Shirika hilo tangu kuanzishwa kwake Desemba mwaka 2014, likihamisha makao yake kutoka Dar es Salaam hadi Singida, kwa nyakati tofauti mpaka sasa limefanikiwa kuanzisha Kliniki ya akinamama inayojulikana kama Pride, mradi wa kufuga kuku Kindai sambamba na kutekeleza mradi wa Aware unaoendelea kufanya vizuri mpaka sasa kwenye kata 5 ndani ya wilaya yaIkungi

“ESPRF na jamii ndio moto wetu, mradi huu wa aware umesaidia sana kumfanya mwanamke kutambua haki zake, lakini madhara ya mila zilizopitwa na wakati, masuala ya ukeketaji na mimba na ndoa utotoni ndani ya jamii,” alisema

Muttani alisema pia shirika hilo limefanikiwa kuanzisha Kamati kwenye vijiji 8 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto huku wakihamasisha uanzishwaji wa vikundi mathalani Sauti ya Mwanamke na Sauti ya Mwanafunzi kulingana na makundi rika, vikundi ambavyo vimekuwa chachu ya mageuzi ya kifikra dhidi ya mila potofu na masuala ya ukatili ndani ya jamii

Alisema ili kuyapa nguvu mashirika yasiyo ya kiserikali kutimiza majukumu yake ipasavyo, anatamani kuona serikali kupitia bajeti yake inatenga walau asilimia moja au mbili ya bajeti ili kusadia mashirika hayo

Mkurugenzi huyo aliitaka jamii ya watanzania kuwa na tabia ya kuzichangia asasi hizo ili kuzipa nguvu na hamasa kuweza kufanya kazi zake ipasavyo


Kwaupande wake, Afisa Ufatiliaji wa SPRF, Mwedinuhu Beleko alisema tatizo la ukatili wa kijinsia hasa ukeketaji ni changamoto kubwa ndani ya mkoa wa Singida, baadhi ya watu bado wanafanya kwa siri na hasa nyakati za usiku wa manane.


“Nichukue nafasi hii kuwasihi sana viongozi wa kimila, wazazi, viongozi wa dini, Jeshi la Polisi na jamii kwa ujumla tushikamane ili kwa pamoja tuweze kutokomeza vitendo vya ukeketaji,” alisema Beleko


Beleko alisema pamoja na mambo mengine, maadhimisho hayo yanatoa fursa ya wao kujitathmini kujua walipotoka, walipo na wanapoelekea katika mtazamo wa kuona jamii inakuwa na uelewa mpana hasa kwenye masuala ya ukatili wa kijinsia na namna bora ya kukabiliana na umaskini wa kipato

Aidha, Muttani akizungumzia miaka minne ya RaisMagufuli, pamoja na kumpongeza lakini amemsihi azitazame taasisi za kiraia kama vyombo vyenye jukumu muhimu kwa taifa na kwamba zinafika mbali zaidi ambapo wakati mwingine serikali haiwezi kufika

Tunafanya kazi ya aina moja hakuna uadui, na ni dhahiri asasi hizi zinalipa kodi kwa taifa hivyo zinapaswa kutazamwa kwa jicho la kipekee kama chachu ya mabadiliko na chanzo cha maendeleo ndani ya jamii. 

Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Maadhimisho ya Miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Hifadhi za taifa Tanzania (TANAPA) na Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro yanatarajia kupamba moto katika viwanja vya Fort Coma nje ya Hifadhi ya Serengeti ambapo Wageni wa kitaifa na kimataifa watashiriki kwa lengo la kuhamasisha uhifadhi enelevu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.


Kamishna Mkuu wa Uhifadhi wa Shirika Hifadhi za taifa (TANAPA) ,Dr.Allan Kijazi amesema kuwa hifadhi  ya Serengeti na Mamlaka ya Hifadhi za Ngorongoro zilianzishwa kwa pamoja mwaka 1959 hivyo kwa pamoja zinasheherekea miaka 60 tangu kuanzishwa kwake licha ya mafanikio na changamoto mbalimbali ambazo zimepitia bado zimeweza kuingiza watalii wengi na kuliingizua taifa mapato makubwa.

Kijazi anasema kuwa maadhimishohayo yatapamwa na wageni kutoka nchi mbalimbali duniani,pamoja na watafiti wakubwa waliowahi kutafiti juu ya Hifadhi ya Serengeti na Ngorongoro ,wadau wa uhifadhi ambao wamekua wakiunga mkono juhudi za uhifadhi watafika katika maadhimisho hao yatakayofanyika Disemba 23 mwaka huu .

Aidha amesema kuwa Mgeni Rasmi katika Maadhimisho hayo anatarajia kuwa Makamu wa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ,Mh.Samia Suluhu  huku akiongozana na Viongozi wengine wa kitaifa ambao watashiriki katika maadhimisho hayo muhimu .

“Kabla ya Maadhimisho hayo kutakua na kongamano la uhifadhi litakalofanyika Disemba 21 mwaka huu katika eneo la  Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ambapo litajumuisha wadau wa uhifadhi pamoja na Wataalamu wa masuala ya uhifadhi huku tukiangazia utalii endelevu kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla” Anaeleza Kijazi

Kwa upande wake Kaimu Kamishana  wa Uhifadhi Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCCA),Asangye Bangu amesema kuwa Kongamano kubwa la uhifadhi litafanyika katika Mamlaka hiyo hivyo amewataka wadau kufika kwa wingi na kuhudhuria katika kongamano hilo muhimu kwa maendeleo ya uhifadhi.

Assangye amesema kuwa tayari Mamlaka hiyo imepata utambulisho wa utalii wa miamba na tayari wameanza kuingiza mapato kwa wingi suala ambalo litajadiliwa katika kongamano na namna ya kuongeza utalii.

Anasema kuwa pia kongamano hilo litaangalia namna ya kuboresha utalii wa mali kale ambao pia umekua ukiliingizia taifa fedha za kigeni.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inatarajia kufungua kitengo cha tiba za mifupa na misuli katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara Kwangwa mara hospitali hiyo itakapokamilika kujengwa.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa hospitali hiyo iliyopo Manispaa ya Musoma mkoani Mara, leo mchana (Jumamosi, Desemba 7, 2019), Waziri Mkuu amesema kitengo hicho kitakuwa cha pili kwa ukubwa kikifuatia cha MOI Muhimbili.

“Lengo la kufungua kitengo hiki kwenye hospitali hii ni kusogeza huduma karibu na wananchi hususan wa Kanda ya Ziwa ambao kwa sasa wanategemea huduma hizo kutoka hospitali ya Bugando, jijini Mwanza ambayo pia imezidiwa kutokana na udogo wa kitengo hicho kwenye hospitali hiyo,” amesema.

Amesema kuwa ujenzi wa hospitali ya Kwangwa ni miongoni mwa miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano ambapo mbali na kutoa huduma za afya lakini pia hospitali hiyo itafungua fursa zaidi za kiuchumi kwa mkoa wa Mara.

Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliagiza kutolewa kwa shilingi bilioni 15 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo uliokwama kwa zaidi ya miaka 40 na ameridhishwa na ujenzi wake unaotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Bw. Adam Malima alisema hospitali hiyo inatarajiwa kuanza kutoa huduma ya mama na mtoto ifikapo Februari, mwakani baada ya kukamilika kwa jengo A (wing A) mapema mwakani.

Bw. Malima alisema kuwa huduma za rufaa za hospitali ya mkoa wa Mara zinatarajiwa kuanza kutolewa Mei, mwakani huku huduma za kibingwa zikitarajiwa kuanza kutolewa kabla ya mwisho wa mwaka 2020.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa baada ya Rais Magufuli kupokea ombi kutoka mkoa wa Mara kuhusu kusaidia mkwamo wa ujenzi huo, Serikali ilitoa fedha zote (sh. bilioni 15) kwa mara moja ili kukamilisha ujenzi huo.

Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu akiwa ameambatana na mkewe Mama Mary Majaliwa, ameiwakilisha Serikali kwenye mazishi ya kaka wa mke wa aliyekuwa Rais wa kwanza wa Tanzania, Mama Maria Nyerere katika kijiji cha Kinesi kilichopo wilayani Rorya, mkoani Mara.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, DESEMBA 7, 2019

Mkuu wa wilaya Tabora mjini Ndg. Komanya Eric Kitwala tarehe 3 Disemba 2019 ameitisha kikao cha kazi kwa viongozi wa serikali ya Mtaa kutoka Mitaa 134, Vijiji 41 pamoja na Vitongoji  156 waliochaguliwa katika uchaguzi wa serikali za Mtaa mwaka 2019 ikiwa ni pamoja na kuwapongeza.

Akiongea katika hadhara hiyo Ndg. Kitwala amewapongeza kwa kuchaguliwa kuongoza serikali ya Mtaa na kuwaasa kutumia dhamana hiyo kwa uadirifu na kuzingatia msingi wa utawala Bora, kanuni na miongozo ya matumizi ya fedha kwa weledi.

Mumebeba matarajio ya watanzania wengi ambao wana imani kubwa na uongozi wa awamu ya tano chini ya Jemedari  Dkt. John Pombe Magufuli, hivyo zingatieni utumishi ulio karibu na wananchi kwa kutatua kero zao hususani upande wa ardhi  Ndg. Kitwala amesema.

Kwa nyakati tofauti Wenyeviti hao wamempongeza Mkuu wa Wilaya kuitisha kikao hicho chenye dhima ya kuwapongeza sanjari na maelekezo ya miongozo ya kazi. Hivyo wameahidi kuzingatia weledi wakati wa kutimiza majukumu yao.

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari Mihayo kimehudhuliwa na Mwenyekiti wa Ccm Wilaya ya Tabora Mjini Mhe. Mohammed Katete, Katibu Tawala Wilaya wa Wilaya pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora

Imetolewa na
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya
Tabora Mjini 🇹🇿


NA SALVATORY NTANDU
Wachimbaji na wamiliki wa maeneo yenye  madini ya ujenzi wilayani kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuwa leseni za uchimbaji ambazo zitawasaidia kuepukana na kutaifishwa kwa madini hayo pindi yanapokamatwa  na kubainika kutolipiwa kodi ya serikali.

Kauli hiyo imetolewa jana na Kamishina wa madini wa mkoa wa Shinyanga Mhandisi Joseph Kumburu kwenye mkutano maalumu na wamiliki wa maeneo ya uchimbaji, wachimbaji, wasafirishaji mjini kahama kuhusiana na kuwa na leseni za uchimbaji wa madini ya Ujenzi.

Amesema kwa mujibu wa sheria ya Madini ya mwaka 2010 kifungu cha sita na marekebisho ya kifungu cha 30 ni kosa la kufanya shughuli za madini bila kibali hivyo wanapaswa kuwa na leseni na hawatakubali kuendelea na  uchimbaji holela wa madini ya ujenzi katika mji wa kahama.

“Tumekuja kutoa elimu kwa kundi hilo linalojihusisha na shughuli za madini ili waitambue sheria hii na namna inavyofanya kazi endapo tukiacha uchimbaji huu holela ukaendelea katika wilaya ya kahama maeneo mengi yatabaki kuwa na mashimo”alisema Kumburu.

Naye mwenyekiti wa Wachimbaji wa madini ya Ujenzi katika wilaya ya kahama Martine Clemency amesema bado wanakabiliwa na changamoto nyingi katika uchimbaji wa madini hayo kutokana na mrundikano wa tozo pindi wanaposafirisha madini ya ujenzi.

“Msafirishaji wa madini haya anatozwa kodi shilingi 2500 kwa kila gari na wakati mwingine hutozwa zaidi ya mara mbili kutokana na kuwepo kwa mageti mengi kabla ya kufikisha mzigo kwa mteja wake jambo ambalo limekuwa likisababisha usumbufu kwa madereva wangu”alisema Martine.

Kwa upande wake ofisa Mazingira wa halamshauri ya mji wa Kahama Johanes Mwebesa amesema halamshauri ya mji imetenga maeneo ya uchimbaji wa madini katika kata ya Ngogwa  na wachimbaji wote wa madini ya Ujenzi waliopo mjini watalazimika kwenda huko ili kuzuia uharibifu wa mazingira.

“Tumefanya tahimini na kujiridhisha kuwa maeneo ambayo tumeyatenga yanafaa kwaajili ya shughuli hizo na muda si mrefu mtalazimika kwenda huko na kuondoka hapa mjini kwaajili ya shughuli hizo za uchimbaji madini Ujenzi”alisema Mwebesa.

Mkutano huo umejumusha wachimbaji,wamiliki wa magari na madereva wapatao 100 na madini ujenzi ambayo yanapaswa kulipiwa ushuru ni pamoja na kokoto,mchanga na moramu.
Na Eleuteri Mangi, Kongwa
Serikali inaendelea kubainisha maeneo yaliyotumiwa na wapingania uhuru wa nchi za Kusini mwa Afrika ambayo yanasimamiwa kupitia Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Afrika iliyopo chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
 
Akiwa katika ziara ya kikazi wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma wakati akitembelea maeneo ya historia ya Ukombozi wa Afrika, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema kuwa Serikali kupitia wizara hiyo inaandaa sheria ya kulinda na kuhifadhi urithi wa ukombozi wa Afrika unaopatikana nchini.
 
“Lengo kubwa ni kuhakikisha maeneo haya yanalindwa kisheria ili yaweze kutumika kama vivutio vya utalii wa kiutamaduni pamoja na utalii wa kihistoria kwa sababu huu ni urithi muhimu wa historia nzuri ya nchi yetu, haya ni maeneo yaliyotumika kusaidia ukombozi wa Nchi za Kusini mwa Afrika” alisema Naibu Waziri Shonza.
  
Katika kutekeleza Programu ya Uhifadhi na Uendelezaji wa historia ya Ukombozi wa Afrika, Wizara inaendelea kutekeleza majukumu mbalimbali ikiwemo, ukarabati wa jengo lililokuwa la Kamati ya Ukombozi ya iliyokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) ambayo kwa sasa ni Umoja wa Afrika (AU).
 
Kazi nyingine ambazo Serikali imekamilisha ni uandaaji wa tovuti ya Programu, ubainishaji wa maeneo yaliyotumika wakati wa harakati za ukombozi, utambuzi wa nyaraka na vitu mbalimbali vinavyohusiana na harakati hizo pamoja na kufanya mahojiano na watu walioshiriki au kushuhudia harakati za ukombozi wa Afrika ambayo yamehifadhiwa kwa njia ya kidigitali.
 
Mji wa Kongwa kihistoria ni kitovu cha harakati za Ukombozi wa Afrika kwani harakati zote za mapambano ya kutafuta uhuru zilianzia Kongwa na baadaye zikaendelea katika maeneo mengine nchini kama sehemu ya kupanua wigo wa harakati hizo na huduma kwa Wapigania Uhuru.
 
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo Deogratius Ndejembi amesema kuwa Kongwa ni eneo kongwe lililotumiwa na Wapigania uhuru kutoka vyama mbalimbali vya Ukombozi kutoka nchi za Kusini mwa Afrika. 
 
Aidha, Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa eneo hilo lilitumika kwa ajili ya mafunzo kwa wapigania uhuru ambapo kwa sasa lina vielelezo muhimu vya kihistoria vilivyopo katika eneo hilo yakiwemo maeneo ya Handaki alilokuwa akilitumia Samora Mashel, nyumba za Makazi kwa wapigania uhuru, majengo ya shule ya sekondari Kongwa, eneo la Mafunzo ya kijeshi, kiwanja cha ndege na makaburi ya wapigania uhuru. 
 
Maeneo mengine ya kihistoria ni makaburi ya mashujaa wa harakati za ukombozi ambayo jumla yake ni 11; makaburi matano ya wapigania uhuru kutoka Msumbiji, makaburi matatu ya wapigania uhuru kutoka Afrika Kusini na makaburi matatu ya wapigania uhuru kutoka Namibia.
 
Naibu Waziri Shonza yupo katika ziara ya kikazi kutembelea maeneo ya ya historia ya ukombozi wa Afrika katika mikoa ya Dodoma wilaya ya Kongwa, Morogoro wilaya Kilosa, Manispaa ya Morogoro pamoja na Mkoa wa Pwani wilaya za Chalinze na Bagamoyo.  
 MKUU wa wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga Yonna Mark akifungumza wakati akifungua mkutano wafanyabiashara eneo la Horohoro wilayani Mkinga ulioandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Tanga ikiwa ni kutoa elimu juu ya umuhimu wa wao kulipa kodi kwa hiari kulia ni Afisa Mfawidhi wa Forodha wa TRA Horohoro Bakari Athmani na Afisa Habari wa Jumuiya ya wafanyabiashara Mkoani Tanga (JWT) Selestine Kiria kushoto ni Meneja wa TRA wilaya za Muheza na MkingaDaudi Njohole



 Meneja wa TRA wilaya za Muheza na MkingaDaudi Njohole akizungumza wakati wa mkutano huo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Mark akifuatiliwa na Afisa Mfawidhi  Forodha wa TRA Horohoro Bakari Athmani na Afisa Habari wa Jumuiya ya wafanyabiashara Mkoani Tanga (JWT) Selestine Kiria 
 Afisa Mfawidhi wa Forodha wa TRA Horohoro Bakari Athmani akizungumza kulia ni Afisa Habari wa Jumuiya ya wafanyabiashara Mkoani Tanga (JWT) Selestine Kiria kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Mark
 Afisa Elimu Mlipa Kodi wa TRA mkoani Tanga Salim Bakar akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo 
 Afisa Elimu Mlipa Kodi wa TRA mkoani Tanga Salim Bakar akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo 

 Afisa Habari wa Jumuiya ya wafanyabiashara Mkoani Tanga (JWT) Selestine Kiria akieleza jambo katika mkutano huo
 Sehemu ya wafanyabiashara wakiwa kwenye mkutano huo

MKUU wa wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga Yona Mark amewaonya wenyeviti wapya wa vijiji na vitongoji wilayani humo kuacha kujshughulisha na biashara za magendo badala yake wawe ndio walinzi wa kuwafichua wahusika ili kukomesha vitendo hivyo.

Mark aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wafanyabiashara eneo la Horohoro wilayani Mkinga ulioandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Tanga ikiwa ni kutoa elimu juu ya umuhimu wa wao kulipa kodi kwa hiari.

Alisema kutokana na wilaya hiyo kuwa mpakani mwa nchi ya Kenya hivyo ikiwemo ukanda wa bahari na nchi kavu hivyo upo uwezekano wa vitendo vya namna hivyo kufanya huku akiwataka viongozi hao kuvikemea na kutokuviruhusu kwenye maeneo yao.

“Ndugu zangu wevyeviti wa vijiji na vitongoji acheni kushirikia kwenye vitendo vya biashara za magendo kwani kufanya hivyo tunaikosesha serikali mapato yake ambayo yangesaidia kuchochea shughuli za kimaendeleo lakini pia niwaambie kwamba tutakaobaini tutashughulikiwa kwa mujibu wa sheria”Alisema Mkuu huyo wa wilaya

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba wataendelea kushirikiana na TRA kufanya operesheni za kupambana na vitendo vya biashara haramu za magendo ili kuvikomesha kabisa kwani kutoka Tanga mpaka mpakani eneo la Horohoro wana kilomita 70 za maji hivyo kupambana na hilo wataanzisha bandari ndogo eneo la moa wilayani Mkinga.

Alisema kwamba wanaanzisha ili kuiwezesha serikali kupata kodi huku akieleza wanatarajia kulifanya hilo miezi michache ijayo watakuwa wamekwisha kufungua huku akiwataka wafanyabiashara hao kutumia njia halali za kupisha bidhaa zao badala ya zile za panya.

,dc akizungumzia mashine za EFD alisema zinawasaidia wafanyabiashara kutokana na kwamba zinaweka mahesabu yao vizuri kutokana na kwamba kila kinachouxwa kinaonekana.hata hivyo aliwataka wafanyabiashara kutangaza biashara zao ili ziweze kutambulika na hatimaye kuweza kupata wateja na hatimaye kuwza kuingiza kipato.ulipaji wa kodi

Awali akizungumza Afisa Elimu Mlipa Kodi wa TRA mkoani Tanga Salim Bakar alisema kwamba hivi sasa walipa kodi wanatambua umuhimu wa kulipa kodi kutokana na Serikali ya awamu ya tano kutekeleza mambo kwa vitendo na kuonekana maendeleo mbalimbali ikiwemo madawa, elimu bure na miradi mbalimbali inatekelezwa kupitia kodi hizo.

Naye kwa upande wake ,Diwani wa Kata ya Duga (CCM) Ally Ally amesema umuhimu wa kulipa kodi kwa wananchi ni mkubwa kutokana na kwamba maendeleo yanayopatikana yanatokana na uwepo wa ulipaji wa kodi hizo.

“Mimi kama diwani wa Kata ya Duga nitaendelea kuhakikisha ninahamasisha wananchi kuendelea kulipa kodi kwa lengo la kusaidia kuchochea kasi ya ukuaji wa maendeleo “Alisema

Hata hivyo pia Afisa Habari wa Jumuiya ya wafanyabiashara Mkoani Tanga (JWT) Selestine Kiria aliwataka wafanyabiashara kuhakikisha wanalipa kodi kwa hiari ili kuwasaidia ukuaji wa maendeleo.

“Kwani wafanyabiashara kulipa kodi ndio Taifa linaendelea lakini pia kuchochea ukuaji wa maendeleo lakini pia hakikisheni mnatoa risiti wakati mnapouza bidhaa zenu “Alisema

Mwisho.