Articles by "MIKAKATI"
Showing posts with label MIKAKATI. Show all posts


 Na Mwamvua Mwinyi, Rufiji


KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2023 ,Abdallah Shaib ametoa rai kwa Watanzania wenye uwezo wa kifedha, kutumia fursa ya kuwekeza na kujenga viwanda ili kuongeza ajira na kuinua uchumi na pato la Taifa.

Ameeleza Serikali inaendelea  kutengeneza mazingira bora na rafiki kwa Taasisi na makampuni ili wawekeze pasipo kuwa na changamoto kwenye uwekezaji.

Akiweka jiwe la msingi katika shamba la Miwa la Kampuni ya Lake Agro ambayo inafanya kilimo Cha miwa kwa ajili ya kujenga kiwanda cha uzalishaji sukari,kata ya Chemchem , Rufiji Mkoani Pwani alieleza, uwekezaji huo ni mfano wa kuigwa kwani ni uwekezaji mkubwa.

Awali Meneja Uwekezaji wa Mradi huo, Nassoro Abubakari ameeleza , endapo kiwanda kikikamilika kinatarajia kutoa ajira zisizopungua 3,400 .

Ameeleza kwamba,wanatarajia kuanza uzalishaji wa sukari ifikapo 2025 lengo likiwa kuanza kuzalisha tani 60,000 kwa mwaka na hivyo kumaliza uhaba wa sukari ya matumizi ya nyumbani huku ukitarajiwa kugharimu sh. Biln 738.3 .

Akipokea Mwenge wa Uhuru ukitokea Kisarawe,Mkuu wa wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele amesema Mwenge ukiwa Rufiji unapitia miradi Saba yenye thamani ya zaidi ya bilioni 739.7.

Kati ya miradi hiyo minne imewekwa jiwe la msingi, mmoja unazinduliwa na miwili kukaguliwa kwenye kata 11 kati 13 zilizopo wilayani hapo umbali wa km.200.

"Kati ya fedha zilizochangia miradi, Halmashauri imechangia milioni 67, Serikali Kuu Bilioni 1.230.9, wahisani milioni 120 na wananchi Bilioni 738.3.
Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma nchini ambayo kila mwaka hufanyika kuanzia tarehe 16 -23 Juni, Leo Juni 21,2022 wamejotokeza kuchangia damu na kufanya usafi katika Hospitali ya Uhuru iliyopo katika Wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
Watumishi mbalimbali wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,wakichangia damnu katika Benki ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama katika Hospitali ya Uhuru iliyopo Chamwino Mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma nchini ambayo kila mwaka hufanyika kuanzia tarehe 16 -23 Juni. 
Mbali na uchangiaji Damu katika Benki ya damu ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wameshiriki kufanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Uhuru iliyopo Chamwino Mkoani Dodoma, 
 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma nchini ambayo kila mwaka hufanyika kuanzia tarehe 16 -23 Juni. 
Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakishiriki kufanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Uhuru iliyopo Chamwino Mkoani Dodoma,  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma nchini ambayo kila mwaka hufanyika kuanzia tarehe 16 -23 Juni. 

Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakishiriki kufanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Uhuru iliyopo Chamwino Mkoani Dodoma,  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma nchini ambayo kila mwaka hufanyika kuanzia tarehe 16 -23 Juni. 

Na Mwandishi Wetu

KATIKA kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma nchini ambayo kila mwaka hufanyika kuanzia tarehe 16 -23 Juni, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imechangia damu na kufanya usafi katika Hospitali ya Uhuru iliyopo katika wilayani Chamwino mkoani Dodoma.

Watumishi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi wameshiriki utoaji wa damu ikiwa ni kuunga mkono jitihada za kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa, akina mama wajawazito na watoto.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Chamwino, Dkt. Abdul Pumzi amesema uhitaji wa damu katika hospitali zetu nchini ni mkubwa mno, hivyo amewapongeza watumishi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kujitoa kwao kwa kuchangia damu kama sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma.




MKUU wa wilaya ya Mkinga Kanali Maulid Surumbu kushoto akipokea mmoja ya miche ya michikichi 30,000 kutoka kwa Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Mazao Wakala wa Mbegu za Kilimo nchini (ASA) Makao Makuu Morogoro Dkt Justin Ringo kwa ajili ya kuwakabidhiwa DAWASA kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mazingira (Dawasa) Mhandisi Modester Mushi kwa ajili ya kuhifadhi mazingira kando kando ya Mto Ruvu na kuwaongezea wananchi kipato




MKUU wa wilaya ya Mkinga Kanali Maulid Surumbu katika akimkabidhi miche ya michikichi 30,000 Mkuu wa Kitengo cha Mazingira (Dawasa) Mhandisi Modester Mushi kwa ajili ya kuhifadhi mazingira kando kando ya Mto Ruvu na kuwaongezea wananchi kipato ambapo miche hiyo ilitolewa na Wakala wa Mbegu za Kilimo nchini (ASA)kulia ni Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Mazao Wakala wa Mbegu za Kilimo nchini (ASA) Makao Makuu Morogoro Dkt Justin Ringo
MKUU wa wilaya ya Mkinga Kanali Maulid Surumbu katika akimkabidhi miche ya michikichi 30,000 Mkuu wa Kitengo cha Mazingira (Dawasa) Mhandisi Modester Mushi kwa ajili ya kuhifadhi mazingira kando kando ya Mto Ruvu na kuwaongezea wananchi kipato ambapo miche hiyo ilitolewa na Wakala wa Mbegu za Kilimo nchini (ASA)kulia ni Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Mazao Wakala wa Mbegu za Kilimo nchini (ASA) Makao Makuu Morogoro Dkt Justin Ringo
MKUU wa wilaya ya Mkinga Kanali Maulid Surumbu akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Mazao Wakala wa Mbegu za Kilimo nchini (ASA) Makao Makuu Morogoro Dkt Justin Ringo
Mkuu wa wilaya ya Mkinga Kanali Maulid Surumbu akisistiza jambo wakati wa halfa hiyo kulia ni Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Mazao Wakala wa Mbegu za Kilimo nchini (ASA) Makao Makuu Morogoro Dkt Justin Ringo

Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Mazao Wakala wa Mbegu za Kilimo nchini (ASA) Makao Makuu Morogoro Dkt Justin Ringo akizungumza wakati wa halfa hiyo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Kanali Maulid Surumbu

Mkuu wa Kitengo cha Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) Mhandisi Modester Mushi akizungumza wakati wa halfa hiyo

Wakiangalia Bwawa



Sehemu ya mbegu za mchikichi zilizopo kwenye Shamba la Mbegu la Mwele






NA OSCAR ASSENGA,MKINGA.



WAKALA wa Mbegu za Kilimo Tanzania (ASA) umesema kwamba lengo lao kubwa hivi sasa ni kuhakikisha tatizo la uhaba wa mafuta linapungua nchini kwa kutumia zao la mchikichi ambalo ni zao la kimkakati kwa kuzalisha mafuta.

Hatua hiyo inatajwa kwamba itapunguza gharama kubwa ambazo Taifa linaingia kuagiza mafuta kutoka nje na hivyo kuondokana na adha ya kutumia fedha nyingi kila mwaka kwa ajili ya bidhaa hiyo.

Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Mazao Wakala wa Mbegu za Kilimo nchini (ASA) Makao Makuu Morogoro Dkt Justin Ringo wakati wa halfa ya makabidhiano ya Mbegu za Michikichi 30,000 kwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Dar es Salaam (Dawasa)kwa ajili ya kuhifadhi mazingira kando kando ya Mto Ruvu na kuwaongezea wananchi kipato

Halfa hiyo ilifanyika kwenye Shamba la Mwele lililopo kata ya Maramba wilayani Mkinga ambalo limepewa jukumu la kuzalisha mbegu za michikichi, Miche hiyo ilitolewa na Wakala wa Mbegu za Kilimo nchini (ASA)

Alisema mbali na michikichi na wameongeza maeneo ya mengine makubwa ya hekta kwa ajili ya kuzalisha zao la alizeti na mashamba mengine waliopanga kuzalisha mazao mengine kwa kuona shida iliyojitokeza wakaona wazalishe mazao ya alizeti.

“Lengo kubwa ni kwenda sambamba na msisitizo wa seriali kuhakikisha mafuta yanapatikana nchini kwa kupatikana mbegu bora za alizeti na michikichi lakini nipende kuwakaribisha wananchi wajipatie mbegu bora za mazao kuinua nchi kiuchumi wao”Alisema

Alisema michikichi hiyo inatokana na Wakala huo kukuza miche kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti Tanzania (TARI) wanapata miche kutoka kwao wanaikuza na kuitoa kwa wadau mbalimbali kama walivyofanya kwa Dawasa.

Awali akizungumza wakati akipokea mbegu hizo za Michikichi, Mkuu wa Kitengo cha Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) Mhandisi Modester Mushi alisema pamoja na wao kutoa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira wanatumia maji kutoka kwenye vyanzo vya mito na hapo lengo lao linaanzia kwenye mto Ruvu ambao unawapatia maji zaidi ya asilimia 92 huduma inayotolewa Dar Es Salaam na Pwani.

Alisema kwamba wameamua kuchukua miche hiyo ya michikichi pamoja na uelekeo wa Serikali katika kuona kwamba wanataka kuzalisha mafuta nchini wao wameona ni zao ambalo litasaidia kutunza chanzo.

Aidha alisema kingo za Mito kwa hivi sasa zinaathirika kwa shughuli za binadamu ikiwemo kilimo, ufugaji hivyo shughuli hizo wananchi wanafanya ili waweze kupata mahitaji yao mbalimbali.

“Hivyo ni tuna imani kwamba upandaji zao la michikichi mwananchi badala ya kupanda mazao ya muda mfupi kupitia michikichi ataweza kuvuna mara nne kwa mwaka na atakuwa mmojawapo anachangia hatua na jitihada za serikali katika kutengeneza mafuta na kipato chake kitabadilika na kitakuwa zaidi ya hivi sasa”Alisema

Alisema miche hiyo itakapokuwa pembezoni ya mto itasaidia kupunguza shughuli za mara kwa mara zinazohusisha kugusa ardhi kulima na itapunguza kiasi kikubwa tope au mchanga ambao unatokana na shughuli hizo unaopelekea mamlaka kuwa na gharama za juu kwenye uzalishaji wa maji.

Naye kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga Kanali Maulid Surumbu alisema mara kwa mara Waziri Mkuu Kasim Majaliwa amekuwa akielekea Kigoma kuhamasisha zao la michikichi ili liweze kuzalishwa kwa wingi ili mwisho wa siku waweze kuondokana na tatizo la mafuta nchini.

Mkuu huyo wa wilaya aliwahamasisha wananchi wa wilaya ya Mkinga zao hilo la mchikichi hata wilaya hiyo linastawi vizuri hivyo watumie fursa ya uwepo wa shamba la mwele ambalo limepewa jukumu lakuzalisha zao la michikichi kutoa mbegu kwa wananchi.

Hata hivyo alisema wilaya hiyo wana mashamba mengi yanayomilikiwa na Taasisi, Halmashauri na watu binafsi ambapo mashamba hayo yakitumika vizuri kuzalisha zao la mchikichi nao watakuwa miongoni mwa dau watakaochangia kupunguza gharama zinazoingiwa na serikali kuagiza mafuta nje ya nchi.
Mwish



NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

Shirika la Omuka Hub iliyoanzishwa na Mhe Neema Lugangira kwa lengo la kuimarisha ushiriki wa sekta ya kidijitali kwa vijana, wanawake, wanahabri, shule na usalama wa intaneti kwa mikoa iliyo pembezoni mwa Tanzania.


Moja ya Vipaumbele vya Omuka Hub ni kuhakikisha kunawepo mazingira wezeshi ya kuwafanya Wanawake Wanasiasa kuwa salama wanapokuwa Mitandaoni hivyo kuanzisha Programu ya Kupinga Ukatilii wa Kijinsia Mitandaoni kwa Wanawake Wanasiasa. 


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Omuka Hub, Lovelet Lwakatare, wakati wa Maonyesho ya Teknologia ya Kupambana na Ukatili wa Kijinsia  yaliyoandaliwa na Shirika la Tangible Tanzania ambalo Mkurugenzi wake ni Madam Geline Fuko.

“Kwa upande wa Ukatili wa Kijinsia, sisi Omuka Hub tumejikita zaidi katika kupambana na ukatili wa kijinsia mitandaoni wanaofanyiwa wanawake wanasiasa na kupitia programu yetu hii tumeanzisha Kikundi cha Wabunge Vinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwa Wanawake Wanasiasa. 


Kikundi hiki kina Wabunge 21 Vinara kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua kushirikiana kupaza sauti kupinga ukatili wa aina hii na kupitia Programu yetu tutahakikisha tunaweza mazingira wezeshi ya usalama mitandaoni kupitia maboresho wa Sera, Sheria na Kanuni.” Alisema Lovelet.


Aidha aliongeza kuwa uzoefu mitandaoni unatuonyesha kwamba wanawake wanasiasa wanavyokuwa katika mitandao ya kijamii na wakiweka kazi zao, kuna idadi kubwa ya watu ambao hawajikiti katika hoja kwa kuchangia au kuuliza maswali bali wanahamishia hoja upande wa uanamke wao kama muonekano wao, jambo ambalo halifanyiki kwa wanaume wanasiasa.


"Shirika la Omuka Hub linapinga ukatili huo na tunataka tuchangie kuweka usawa wa kijinsia mitandaoni ili mwanamke mwanasiasa aweze kutumia Mitandao kwa uhuru sawa na makundi mengine. 


Hii itasaidia  wanawake waweze kujiamini wanapokuwa katika mitandao ya kijamii kuzungumza na wananchi wao bila kuulizwa kwa nini nywele amekata, kwanini amevaa vile ambavyo amevaa, anafaa kwa hili, kwa lile na hivyo ndivyo ambavyo tutawawezesha wanawake wengi zaidi kushiriki kwenye siasa na kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa.


Katika maadhimisho hayo ya siku 16 kupinga ukatili wa kijinsia duniani kote ambayo dunia inajitambulisha kama The ‘Orange World’  “Sisi Omuka Hub tunapinga, tunakemea tunatoa rai kwa watu wote kuacha ukatili wa kijinsia wanaofanya mitandaoni kwa wanawake wanasiasa na tunahamasisha watu wanapokuwa katika mijadala waweze kuchangia kwa hoja na isiwe muonekano wao, mavazi yao, familia zao au masuala yao binafsi." Alisema Lovelet.


"Kwa niaba ya Omuka Hub  tunamshukuru sana Madam Geline Fuko, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tangible Tanzania kwa kutupa fursa ya kuwa kati ya Mashirika yaliyochaguliwa kushiriki katika maonyesho ya teknologia ya kupambana na ukatili wa kijinsia katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwl Nyerere Dar es Salaam, tarehe 26 Novemba 2021 na tulifurahia sana mrejesho mazuri ya kazi zetu tuliopata kutoka kwa Mgeni Rasmi, Mhe Madam Kate Somvongsiri, Mwakilishi Mkazi wa Shirika  la Kimataifa la Misaada la Serikali ya Marekani (USAID Mission Director, Tanzania). " alimalizia Lovelet.

Wabunge  21 ambao ni Wabunge Vinara wa Kupinga Ukatilii wa Kijinsia Mitandaoni kwa Wanawake Wanasiasa (MP Champions Addressing Online Gender Based Violence on Women in Politics) ni Neema Lugangira, Salome Makamba, Nusrat Hanje, Judith Kapinga, Felista Njau,  Condester Sichalwe, Ng'wasi Kamani,  Jesca Kishoa, Keysha Khadija Taya, Tauhida Garlos, Mariam Ditopile, Catherine Magige, Lathifa Juakali, Rashid Shangazi, Elly Kingu, Abubakari Assenga, Festo Sanga, Rama S. Rama, Zaytuni Swai, Kassim Hassan Haji na Jac

 

 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb), akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Ngw’ilabuzu Ludigija (mwenye kaunda suti) juu ya maboresho ya miundombinu inayofanywa katika mnada wa kimataifa wa Pugu uliopo jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Miundombinu na Uendelezaji Masoko ya Mifugo Bw. Humphrey Killo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb), akikagua ubora wa matofali yanayotumika katika ujenzi wa uzio katika mnada wa kimataifa wa Pugu uliopo jijini Dar es Salaam, mara baada ya kufanya ziara ya kikazi ya siku moja katika mnada huo ili kusikiliza kero zinzowakabili wafanyabiashara na kukagua maboresho ya miundombinu.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb), akisikiliza maelezo mbalimbali kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Ngw’ilabuzu Ludigija (mwenye kaunda suti) na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Miundombinu na Uendelezaji Masoko ya Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Humphrey Killo, Mhe. Ulega amefanya ziara ya kikazi ya siku moja katika mnada wa kimataifa wa Pugu uliopo jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb), akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Ilala, mnada wa kimataifa wa Pugu na maafisa kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, baada ya kukagua eneo la kuhifadhia mbuzi katika mnada huo alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja.

 

Na. Edward Kondela

 

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) amesikiliza kero za wafanyabiashara wa mnada wa kimataifa wa Pugu uliopo jijini Dar es Salaam ukiwemo utaratibu wa utoaji wa huduma katika mnada huo, uhaba wa maji, uchakavu wa miundombinu ya kuhifadhia mifugo na ubovu wa eneo la kushusha na kupakia mifugo.

 

Akiwa jijini Dar es Salaam katika ziara ya kikazi ya siku moja katika mnada huo (26.08.2021), Naibu Waziri Ulega amearifiwa pia changamoto ya ukosefu wa taa ndani ya mnada huo, jambo ambalo Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam, Bi. Tabu Shaibu ameahidi kulishughulikia ndani ya wiki moja.

 

Wakifafanua juu ya changamoto hizo baadhi ya wafanyabiashara hao wamemueleza Naibu Waziri Ulega kuwa biashara katika mnada huo inaanza saa moja asubuhi, lakini changamoto wanayoipata ni suala la ukatishaji wa ushuru ambapo watumishi wanafungua ofisi saa tatu asubuhi kwa mujibu wa mwongozo wa minida.

 

Aidha wameeleza kuwa bado wanakabiliana na kero mbalimbali ikiwemo ya uchakavu wa paa la eneo la kuhifadhia mifugo yao, wakisema wakati wa mvua wanapata shida ya kujikinga wao pamoja na mifugo wanayoihifadhi.

 

Akifafanua juu ya utatuzi wa kero hizo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) amewaelekeza watendaji wa mifugo wa wizara hiyo, kurekebisha mwongozo wa mnada ili kuruhusu shughuli za huduma kuanza saa moja asubuhi badala ya saa tatu asubuhi.

 

“Lengo la ziara hii ni kuangalia utekelezaji wa shughuli mbalimbali ikiwemo kukagua ujenzi wa uzio unaozunguka mnada huu pamoja na kupokea na kushughulikia kero zinazowakabili wafanyabiashara.” Amesema Mhe. Ulega

 

Ameongeza kuwa mwongozo huo uliwekwa wa saa tatu asubuhi kutokana na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu ambao wanaweza kufanya ujanja wa kwenda na mifugo katika minada kisha kuondoka nayo kwa kisingizio cha kukosa wateja na kuikosesha serikali mapato.

 

Amebainisha sababu nyingine kuwa ni upatikanaji wa huduma za kifedha kwa muda wa kuanzia saa moja asubuhi, hata hivyo amesema kitendo cha huduma hizo kuanza saa tatu badala ya saa moja asubuhi kinasababisha watanzania kukosa biashara kwa wale wanaotegemea mazao ya mifugo.

 

“Shusheni muda hadi saa moja asubuhi, ongeeni na watu wa mabenki waanze kutoa huduma kuanzia muda huo. Polisi wapo wana uwezo na uweledi wataimarisha ulinzi. Rais Samia Suluhu Hassan anapenda watu wafanye kazi na kulipa ushuru naagiza shusheni muda.” Amesema Mhe. Ulega.

 

Kuhusu changamoto la paa, Mhe. Ulega amesema mkandarasi ameshapatikana na kazi ya kupaua na kurekebisha eneo itaanza mara moja  na itafanyika usiku na mchana na kwamba Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), imeshafikisha maji katika mnada huo.

 

Ameongeza kuwa kilichobaki ni miundombinu ya mabomba na mchakato utakamilika ndani ya wiki moja na kuhusu uzio kazi imeshaanza na amemuelekeza mkandarasi akamilishe kazi hiyo hadi Septemba 5 mwaka huu.

 

Pia Naibu Waziri Ulega amewaarifu wafanyabiashara hao kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameupa mnada wa Pugu Shilingi Milioni 600, kwa ajili kutengeneza eneo la kunyweshea mifugo maji na mkandarasi ameshapatikana kwa ajili ya kazi hiyo itakayoanza wiki ijayo.

 

 

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), Prof. Peter Msoffe akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuingia kwenye ofisi za NARCO jijini Dodoma kwa ajili ya kukabidhiwa ofisi leo July 1,2021.

Aliyekuwa Meneje Mkuu wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), Bw. Masele Shilagi (kulia) akimkabidhi gari Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Prof. Peter Msoffe (katikati) wakati wa makabidhiano ya ofisi yaliyofanyika jijini Dodoma. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji na Masoko (WMUV), Bw. Stephen Michael.

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), Prof. Peter Msoffe (kulia) akipokea taarifa ya makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo, Bw. Masele Shilagi (kushoto). Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji na Masoko (WMUV), Bw. Stephen Michael akishuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika kwenye Ofisi za NARCO jijini Dodoma.

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), Prof. Peter Msoffe (kulia) akipeana mkono na aliyekuwa Kaimu Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Bw. Masele Shilagi baada ya kukabidhiana ofisi jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji na Masoko (WMUV), Bw. Stephen Michael akizungumza na viongozi na watumishi wa Kampuni ya Ranchi za Taifa mara baada ya kumalizika kwa makabidhiano ya ofisi jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji na Masoko (WMUV), Bw. Stephen Michael (wa tatu kutoka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi na watumishi wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) mara baada ya kukamilika kwa makabidhiano ya ofisi yaliyofanyika jijini Dodoma.


Meneja Mkuu wa Kampuni za Ranchi za Taifa (NARCO), Prof. Peter Msoffe ametaja mikakati itakayosaidia kampuni hiyo kuweza kujiendesha kibiashara Zaidi.

Prof. Msoffe ameibainisha mikakati hiyo baada ya kumalizika kwa kikao cha makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Kaimu Meneja Mkuu wa NARCO, Masele Shilagi kilichofanyika leo July 1,2021 jijini Dodoma.

Akizungumzia mikakati hiyo, Prof. Msoffe amesema kuwa serikali inataka kampuni hiyo iwe kitovu cha umahiri wa masuala yote yanayohusu ranchi. Katika kuhakikisha hilo linafanikiwa ni lazima kampuni ijipange katika uzalishaji wa nyama ya kutosha iliyo bora, uzalishaji wa mifugo iliyo bora, kutoa mafunzo kwa wataalam na wafugaji, kujiendesha kibiashara na kuweza kupeleka gawio serikalini.

Aidha, amesema ana matarajio makubwa kuwa hayo yataweza kutekelezeka kwa kuwa yeye ameikuta kampuni ikiwa inaendelea kuimarika hivyo kwa kushirikiana na viongozi na watendaji wa kampuni wataweza kutekeleza mikakati hiyo ambayo itawasaidia kuweza kutimiza azma ya serikali kwa kampuni hiyo.

Naye Masele Shilagi ambaye alikuwa ni Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ranchi za Taifa amesema kuwa kampuni imekuwa ikiendelea kuimarika kimapato ambapo iliweza kujiendesha bila kutumia ruzuku kutoka serikalini. Pia wameweza kusimamia mapato na matumizi ambapo kampuni imekuwa ikipata hati safi.

Lakini pia amesema kampuni imeweza kupima baadhi ya ranchi zake na kushughulikia migogoro iliyokuwepo ikiwemo ya uvamizi wa wananchi kwenye maeneo ya ranchi. Aidha, Masele amewashukuru viongozi na watumishi wa NARCO kwa ushirikiano waliompatia kipindi cha uongozi wake na kuwaomba waendelee kutoa ushirikiano kwa Meneja Mkuu mpya.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Uzalishaji na Masoko, Stephen Michael amesema kuwa viongozi na watendaji wanao wajibu wa kujipanga vizuri ili kuhakikisha malengo na matarajio ya serikali yanatimizwa. NARCO inazo fursa nyingi kwenye uzalishaji wa nyama bora, mifugo bora, malisho na utoaji wa elimu kwa wafugaji.

Michael amesema katika kuhakikisha fursa zinatumika na mapato yanaongezeka kama serikali ilivyopanga, ni lazima uongozi uone namna bora ya kushirikiana na sekta binafsi lengo likiwa ni kuongeza uzalishaji na kuongeza mapato.

 

 Timu ya wataalamu wa Tanesco kitengo cha masoko makao makuu ikishirikiana na ofisa huduma kwa wateja mkoa wa Tabora umeendelea na zoezi la uhamasishaji wa wananchi kwenye miradi inayotekelezwa na wakala wa umeme vijijini REA kupitia mkandarasi wa umeme kampuni ya Sengerema Electrica group (SEGL) ili kuandaa wananchi kuanza maandalizi ya wiring kwenye nyumba zao mkoani Tabora.

Pamoja na kuanza maaandalizi ya utandazaji wa miundombinu ya umeme kwenye nyumba pia wananchi hao wamepata fursa ya kujifunza maswala mbali mbali yanayohusu taratibu za kufuata ili kujiunganishia huduma ya umeme, Gharama ya kuunganisha umeme, wigo wa mradi kwenye maeneo yao, matumizi ya UMETA na umuhimu wa kutunza miundombinu ya shirika ikiwemo tahadhari ya kuchoma moto hovyo hasa wakati wa kiangazi.

Wanchi pia wamepata fursa ya kuuliza na kupata elimu mbalimbali zinazohusiana na huduma za ki-Tanesco kama vile makundi ya matumizi ya wateja, adha iliyojitkeza ya manunuzi ya LUKU kwa siku za karibuni, na hali ya kukatika kwa umeme kwenye maeneo yao.

Wananchi wa maeneo mengi bado wameendelea kulalamikia wigo mdogo wa mtandao wa miundombinu ya umeme kwenye maeneo huku wakisisitiza kuwa hata miradi ya upanuzi bado haiwezi kutatua mahitaji yao kwani maeneo mengi bado yameachwa. Zoezi la uhamasishji unaendelea kwenye wilaya zote za mkoa wa Tabora(Sikonge, Urambo, Kaliua, Uyui, Nzega na Igung) isipokuwa Tabora manispaa ambayo haijanufaika na mradi wa upanuzi IIA(Densification IIA).

 

Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora (TBS) Bw.Mosses Mbambe (katikati) akifuatiliakikao kazi na Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFFA) kilichofanyika leo katika ofisi za Makao makuu TBS leo Jijini Dar es Salaam.

Mawakala wa wa Forodha (TAFFA) wakifuatilia kikao kazi ambacho kiliwakutanisha na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kujadili ni namna gani wanaweza kutatua changamoto zao katika utendaji kazi wao.


NA EMMANUEL MBATILO

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wamekutana na wanachama wa chama cha Mawakala wa Forodha (TAFFA) kwaajili ya kujadili ni namna gani wanaweza kuboresha utendaji kazi wao katika kuhakikisha wanakuza biashara na kumlinda mtumiaji.

lengo ni kuwapitisha katika taratibu za ukaguzi na upimaji wa bidhaa ambao unafanya na shirika hilo na vilevile wamewapitisha katika mfumo wa electronic window system ili waufahamu namna ya kuutumia na kurahisisha utoaji wa mizigo katika vituo vya forodha.

Akizungumza mara baada ya mkutano huo Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora (TBS) Bw.Mosses Mbambe amesema kuwa changamoto iliyopo kwasasa ni utumiaji wa mfumo wa electronic window system inaonekana kwamba baadhi ya mawakala hawaufahamu mfumo huo na kuweza kupelekea ucheleweshaji wa utoaji wa mizigo kutoka katika vituo vya forodha.

"Kama hauwezi kutumia huu mfumo kuna athari zinaweza kujitokeza hasa kuchelewesha mzigo kutoka katika kituo cha forodha na mzigo ukichelewa kutoka ina maana mteja hataweza kupata mzigo wake kwa wakati vilevile inaweza kupelekea mlundikano wa mizigo katika vituo vya forodha". Amesema Bw.Mbambe.

Kwa upande wake Meneja wa masuala ya ukaguzi wa bidhaa zinazotoka nje (TBS) Mhandisi Saidi Mkwawa amesema kuwa kuna baadhi ya mawakala wamekuwa wakilalamika kuna tatizo kwenye mfumo wa kuweza kufanya usajili na kuweza kutoa nyaraka zao kwaajili ya kufanyiwa ukaguzi ambapo kumekuwa na changamoto mbalimbali.

"Dhamira ya Serikali ni kumuepushia usumbufu yule wakala ambaye anafanya biashara kwasababu mfumo huu zamani kila unaemuona wakala wa forodha alikuwa lazima aweze kufanya maombi ya mifumo mbalimbali, aende Shirika la wakala wa meli TASAC, afike TBS kwenye mfumo tofauti ama aende kwenye mifumo mingine ya serikali. Lakini serikali ikaona yakwamba kuwe na mfumo mmoja ambao utarahisisha na kutoa ufanisi lakini kila jambo jipya linalokuja lazima liwe na changamoto zake". Amesema Mhandisi Mkwawa.

Nae Katibu Mtendaji (TAFFA) Bw.Elitunu Mallamia amesema kuwa kupitia mkutano huo unazidi kukuza mahusiano yao na TBS ambao wanashirikiana nao kwenye kusaidia nchi iweze kuingiza bidhaa bora na bidhaa ambazo zitawalinda watumiaji.

Sambamba na hayo Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Masoko (TBS), Bi.Gladness Kaseka amewakaribisha wadau mbalimbali wanaoona kuna changamoto wanazipitia katika utendaji ili waweze kufanya nao kikao na kujadili ni namna gani wanaweza kumaliza ama kupungua changamoto hizo.

 

Rais Samia Suluhu Hassan akimwapisha Pauline Gekul kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma jana.

Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Lugha Bashungwa (asiye na Miwani) akizungumza na Viongozi Wakuu wa Wizara; kushoto ni Naibu wake Mhe. Pauline Gekul, kulia ni Katibu Mkuu na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas na wa kwanza ni Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Ally Possi, mara baada ya hafla ya uapisho iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma jana.Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul na Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Ally Possi (katikati) na Mkurugezi wa Utawala wa Wizara hiyo Bernard Marcelline mara baada ya hafla ya uapisho iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma jana.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul akizungumza na Katibu Mkuu na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas(mwenye suti ya bluu) na Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Ally Possi, mara baada ya hafla ya uapisho iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma jana.




·       Bashungwa amshukuru Mhe.Rais

 

Na John Mapepele, Dodoma

 

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Pauline Gekul ameahidi kuimarisha ushirikiano  kwa wadau wa  tasnia za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kutimiza  ahadi za Ilani ya Chama cha Mapinduzi  na  ahadi alizozitoa Mheshimiwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan wakati wa Kampeni za Uchaguzi   Mkuu mwaka 2020. 

Mhe. Gekul ameyasema haya muda mfupi baada ya kuapishwa  kuwa Naibu Waziri kwenye tasnia hizo na Mhe. Rais kwenye Ikulu ya  Jijini Dodoma jana ambapo amewahakikishia wadau wote nchini kuendeleza ushirikiano  ili kuleta mapinduzi makubwa katika Wizara hiyo kwa kushirikiana na Waziri mwenye dhamana hiyo Mhe. Innocent Bachungwa.

“ Nitatoa ushirikiano kwa Waziri wangu lakini pia kwa wadau wote wa tasnia hii ya Wizara yetu ili kuhakikisha michezo, utamaduni, habari, Sanaa kila jambo liende  kulingana na ahadi alizotoa  mama yetu mpendwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ” amesisitiza Gekul

Amesema katika kutenda kazi hii mpya pia atazingatia miongozo aliyoitoa Mhe. Rais kwenye hotuba yake awali ambapo alielekeza mambo mahususi ya kuyafanyia kazi.

Akizungumzia uteuzi wa Naibu Waziri Gekul mara baada ya kukamilisha zoezi la kuwaapisha Katibu Mkuu Kiongozi, Mawaziri na Manaibu Mawaziri, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan amesema. “Nimemtoa Wizara ya Mifugo, pengine anajua mambo ya mifugo mifugo, lakini nikaona aende kwenye michezo awasaidie wanawake”

Amesema wanawake wamefanikiwa kuleta vikombe vitatu hapa nchini na hawatajwi kama ilivyo kwa upande wa wanaume ambapo ameeleza kuwa awali yeye ndiye alipewa kazi hiyo kwenye kipindi cha kwanza cha Awamu ya Tano na Hayati, Rais Magufuli hivyo amempa  Mhe. Gekul kwa matarajio makubwa.

 

 Amefafanua kuwa wanawake wamekuwa akifanya vizuri kwenye michezo mbalimbali hivyo aende akasimamie hilo kikamilifu

“Wanawake kwenye michezo wanafanya vizuri, hawasifiwi lakini wanaume wakishinda tu, katia goli huku viwanja vinagawiwa” ameongeza Mhe. Rais Samia.

Naye Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa amemshukuru Mhe. Rais kwa kuwa  na Imani nao na kuendelea kuwateua kusimamia tasnia hizo na kumuahidi kufanya kazi kwa ushirikiano, uadilifu na ubunifu mkubwa  ili kutimiza ahadi za Serikali kwa wananchi wake.

“Kipekee ninamshukuru  sana Rais wangu, Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea  kutuamini naomba kumhakikishia kuwa tutafanya kazi  bila kuchoka  na kwa ushirikiano  mkubwa  baina yetu sote, sisi  na wadau wetu wote ili kukamilisha ahadi katika kipindi kifupi” ameongeza Mhe. Bashungwa

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora; Mhe Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo bungeni

 

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) kupitia NGOs Mh .Neema Lugangira akiuliza swali bungeni

MWANDISHI WETU, DODOMA.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora; Mhe Deogratius Ndejembi amesema Serikali tayari imeanzisha kanzidata kwa walengwa wote wanaopokea fedha za TASAF ambao ulianza kwa Halmashauri 19 nchini lakini kwa sasa umekwisha kuzifikia Halmashauri 39.

Aliyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu maswali mawili ya ya nyongeza ya Mbunge wa Viti Maalum (CCM) kupitia NGOs Mh Neema Lugangira ambaye alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuanzisha kanzidata kwa kutumia Tehama ili kuhakikisha wanufaika wa mpango wa TASAF ni wale waliokidhi vigezo ambavyo vimewekwa.

Sambamba na kuondoa mianya ya watu wanaonufaika na mpango huo kusajiliwa mara mbili kwenye maeneo tofauti tofauti jambo ambalo linapelekea wengine kukosa fursa hiyo muhimu.

Naibu Waziri huyo alisema pia wataanza kuweka mfumo wa kuunganisha kanzidata na NIDA na mitandao ya simu ili walengwa badala ya kupokea fedha dirishani kwa wale wanaoenda kugawa fedha hizo ziende moja kwa moja kwenye simu zao ili kuhakikisha hakuna malipo mara mbili.

Alisema kwa sababu kumekuwa na malalamiko kwamba watu wanapokea mara mbili fedha na hata mtu akiwa hayupo zinachukuliwa na watu wengine hivyo ili kudhibiti hilo lisiendelee kutokea ndio maana watakwenda kuweka mfumo huo kwenye Halmashauri zote 185 za Tanzania Bara na maeneo ya Uguja na Pemba.

Katika swali lake la pili Mbunge Neema aliuliza Je serikali ina mpango gani kuhakikisha kaya ambazo hazikunufaika awali sasa zinanufaika kwenye awamu ya tatu ya TASAF hususani wazee sio tu kwa Manispaa ya Bukoba bali pia mkoa wa Kagera na Taifa kwa Ujumla.

Akijibu swali la pili la Mbunge huyo, Naibu Waziri huyo alisema Serikali itatanua mpango huu kwa wazee ambao hawakuingia na kaya ambazo hazikuingia wataingia hivyo aliwatoa mashaka wabunge wa majimbo na viti maalum nchini kuwa mpango huo unakwenda kwenye kaya milioni 1.4 ambazo ni sawasawa watu milioni 7 ambao watakwenda kunufaika na mpango huu wa TASAF.

 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali, akizungumza kuhusu matengenezo ya Mitambo na Magari yanayotumika katika Kilimo cha umwagiliaji na ujenzi wa miundombinu yake.
Moja ya mtambo katika ofisi za Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Dodoma ukiwa Tayari kukodishwa kwa ajili ya Shuguguli za kilimo cha Umwagiliaji na Ujenzi wa Miundombinu yake.
moja ya gari lililopaki zaidi ya mwaka mmoja aina ya Nissan Diesel lenye namba za Usajili STJ 328, likifanyiwa matengenezo tayari kwa shughuli za umwagiliaji.
 baadhi ya Mitambo ambayo ipo katika hatua ya kufanyiwa matengenezo.

Baadhi ya Magari yaliyopo tayari kukodishwa kwa ajili ya shughuli za kilimo cha Umwagiliaji na ujenzi.

 NA MWANDISHI WETU,DODOMA
IMEELEZWA kuwa katika robo ya pili ya mwaka wa Serikali,Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inategemea na inaendelea kutekeleza majukumu ambayo imepangiwa ikiwa ni pamoja na kutengeneza na kukarabati magari na mitambo iliyokuwa imeharibika na kuacha kufanyakazi kwa muda mrefu, vitendea kazi ambavyo vinatumika katika kuendeleza sekta ya umwagiliaji.

Hayo yamesemwa, na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaale, alipokuwa akizungumza Mjini Dodoma, kuhusu ufufuaji na ukarabati wa mitambo inayotumika katika ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya Umwagiliaji.

“tunapojenga Miundombinu ya umwagiliaji tunahitaji mitambo na magari makubwa, Kwa hivyo inafanyika kazi kubwa kwasasa yakufufua vitendea kazi hivyo ili kuweza kujenga uwezo wa Tume na kuendeleza miundombinu ya umwagiliaji.” Alisema Bw. Kaali

Aliendelea kusema kuwa vitendea kazi hivyo ni muhimu sana hasa kwa sasa wakati ambao Tume inakaribia kuanza kutekeleza miradi ya umwagiliaji kwa kupitia force account.

“Miradi hii ambayo inategemea kuanza kutekelezwa kupitia force account inategemea kuanza kutekelezwa mwezi huu hivyo tunahitaji kuwa na vitendea kazi vyakutosha, na mpaka sasa tumeweza kufufua mitambo iliyopo mikoa ya Mbeya ambapo kulikuwa na mitamboa mbayo ilikuwa imeharibika tumeweza kuifufua lakini pia hata hapa makao makuu Dodoma kumekuwa ma mitambomingi, ambayo nayo pia ilikuwa imeharibika ilikuwa haifanyikazi tumeweza kuifufua tumefufua mitambo kama miwili kwa hapa Dodoma katika robo hii ya mwaka, lakini pia tuna maroli matatu,na kule Mbeya tunategemea kufufua eskaveta ambayo ilikuwa imeharibika tunategemea nayo itaanza kufanya kazi.”Alisisitiza

AidhaBw. Kaali aliongeza kwa kusema kuwa,kwa upande wa mitambo ambayo ufanisi wake umeanza kupungua, nayo itafanyiwa matengenezo yaani,mitambo ambayo imekaa kwa muda mrefu bila kupata matunzo na matengenezo kwa wakati.

“tunatengemea kumaliza matengenezo hayo ili tuweze kuanza utekelezaji wa miradi ya force account, ambayo tunategemea kuanza mwezihuu.”

Awali, Akizungumza kuhusu swala la kukodisha mitambo kwa taasisi ambazo zinauhitaji, Bw. Kaali ametoa wito kuwa,Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inakodisha mitambo ya umwagiliaji na mitambo mizito ya ujenzi kama vile Buldoza na Maroli, kwa wadau mbalimbali kama vile mashirika ya umma.

Alieleza pia kwa watu Binafsi na taasisi mbalimbali ilikuweza kuchangia katika maendeleo ya nchi huku akieleza vipaumbele vya ukodishawaji wa mitambo hiyo,vinatolewakwa wale wanaofanya shughuli za umwagiliaji wanaotaka kuendeleza skimu zao za umwagiliaji.