Na Mwamvua Mwinyi, Rufiji


KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2023 ,Abdallah Shaib ametoa rai kwa Watanzania wenye uwezo wa kifedha, kutumia fursa ya kuwekeza na kujenga viwanda ili kuongeza ajira na kuinua uchumi na pato la Taifa.

Ameeleza Serikali inaendelea  kutengeneza mazingira bora na rafiki kwa Taasisi na makampuni ili wawekeze pasipo kuwa na changamoto kwenye uwekezaji.

Akiweka jiwe la msingi katika shamba la Miwa la Kampuni ya Lake Agro ambayo inafanya kilimo Cha miwa kwa ajili ya kujenga kiwanda cha uzalishaji sukari,kata ya Chemchem , Rufiji Mkoani Pwani alieleza, uwekezaji huo ni mfano wa kuigwa kwani ni uwekezaji mkubwa.

Awali Meneja Uwekezaji wa Mradi huo, Nassoro Abubakari ameeleza , endapo kiwanda kikikamilika kinatarajia kutoa ajira zisizopungua 3,400 .

Ameeleza kwamba,wanatarajia kuanza uzalishaji wa sukari ifikapo 2025 lengo likiwa kuanza kuzalisha tani 60,000 kwa mwaka na hivyo kumaliza uhaba wa sukari ya matumizi ya nyumbani huku ukitarajiwa kugharimu sh. Biln 738.3 .

Akipokea Mwenge wa Uhuru ukitokea Kisarawe,Mkuu wa wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele amesema Mwenge ukiwa Rufiji unapitia miradi Saba yenye thamani ya zaidi ya bilioni 739.7.

Kati ya miradi hiyo minne imewekwa jiwe la msingi, mmoja unazinduliwa na miwili kukaguliwa kwenye kata 11 kati 13 zilizopo wilayani hapo umbali wa km.200.

"Kati ya fedha zilizochangia miradi, Halmashauri imechangia milioni 67, Serikali Kuu Bilioni 1.230.9, wahisani milioni 120 na wananchi Bilioni 738.3.
Share To:

Post A Comment: