Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Waumini wa kanisa katoliki parokia ya Lubaga Mjini Shinyanga wamekumbushwa wajibu wa kuuishi upendo wa Mungu kwa matendo ya kweli,ikiwa ni pamoja na kusaidia wenye uhitaji.

Mafundiyo hayo yametolewa na shemasi James Mrema wa parokia ya Lubaga wakati akihubiri katika adhimisho la misa takatifu ya jumapili iliyokwenda sanjari  na kuombea marehemu waliofariki Dunia kwenye ajali ya Meli ya MV Bukoba mnamo  Mei 21, 1996 Mkoani Mwanza

Amesema ni wajibu wa kila Mkristu kuuishi upendo wa Mungu kwa kuwasaidia kwa namna mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwaombea watu wengine wakimemo wagonjwa,na wale waliotangulia mbele za Mungu ambao wanahitaji huruma ya Mungu

Shemasi James amesisitiza kuhusu wajibu wa kumtumikia Mungu katika Imani ya kweli,kushiriki ibada, na matendo ya huruma.

Waumini wa kanisa katoliki parokia ya Lubaga Mjini Shinyanga wameungana na watanzania wengine Nchini kuwakumbuka ndugu,jamaa na marafiki walipoteza maisha kutokana na ajali ya Meli ya Mv Bukoba mnamo Mei 21, Mwaka 1996

Katika serikali iliwakilishwa na Neema Mkandala kwa niamba ya mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, ambaye katika salamu zake amewakumbusha ndugu na jamaa waliopoteza maisha katika ajali ya MV Bukoba  pamoja na mambo mengine amesema watanzania wanapaswa kuishi maisha yanayompendeza Mungu, ikiwa ni pamoja na kupinga ukatili unaoendelea.

“Katika kuendelea kuwaenzi wapendwa wetu tukumbuke kufanya matendo mema yakumpendeza Mungu serikali ya awamu ya sita ikiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kukemea vitendo viovu vya mmomonyoko wa maadili katika jamii zetu na kukemea ukatili wa kijinsia, katika kuwaenzi ndugu zetu niwaombe waumini wote tuwe msitari wa mbele katika kutoa taarifa kuhusiana na ukatili unaofanyika katika jamii zetu kwenye vyombo husika na tufanye matendo mema kwa kuwa na maadili yakumpendeza mwenyezi Mungu”. Amesema Neema Mkandala

Share To:

Misalaba

Post A Comment: