Articles by "Matuki BREAKING NEWS"
Showing posts with label Matuki BREAKING NEWS. Show all posts

 Moja ya jukumu la Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) ni kukagua mbolea zinazozalishwa nchini au kuingizwa nchini kutoka nje ya nchi kabla ya kumfikia mkulima.


Jukumu hilo ni takwa la kisheria na linatekelezwa kikamilifu ambapo kila muingizaji wa mbolea huhakikisha mbolea yake inakaguliwa na kupewa kibali cha kuingia sokoni.

Leo tarehe 14 Novemba, 2023 Maafisa Udhibiti Ubora kutoka TFRA, John W. Sostheness na Levin A. Magera wamefanya ukaguzi katika bandari kavu ya kampuni la Afri- ICD iliyopo eneo la Tazara, Jijini Dar Es Salaam baada ya shehena ya tani 966.28 za Mbolea ya Ammonium Sulphate (SA)21%N kuingizwa nchini na kampuni ya mbolea ya Staco Agrochem.

Katika ukaguzi huo wataalam walijiridhisha kwa kukagua nyaraka mbalimbali ikiwa ni pamoja na kibali cha kuingiza mzigo kutoka TFRA (fertilizer import permit) , Bill permit , Assesment form ya TRA na Taarifa za maabara za Mbolea kabla ya kuja nchini ili kupata taarifa za Mbolea hiyo, kabla ya kuipeleka maabara kwa uchunguzi zaidi wa kikemikali ( Chemical analysis).

Aidha, wataalam hao wamechukua sampuli kwa mjibu wa Sheria ili kupeleka maabara kujua Ubora wa Mbolea kabla haijapelekwa kwa wafanyabiashara hadi kwa mkulima.

Utekelezaji wa jukumu hili unasaidia katika kuhakikisha wakulima wanapata mbolea bora ili waweze kuzalisha Kwa tija.


 

Afisa Udhibiti Ubora kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), John W. Sosthenes akijaza fomu maalum  ya kuchukulia sampuli   ya mbolea kwa ajili ya uchunguzi wa Ubora wake   maabara.
 

Afisa Udhibiti ubora wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Levin A. Magera akifunga mfuko uliotumika kuhifadhia sampuli ya mbolea tayari kwa ajili ya kuipeleka maabara ili kudhibitisha ubora wake kabla hazijaingizwa kwa sokoni.
 

Maafisa Udhibiti Ubora kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), John W. Sosthenes (katikati walikosimama) na Levin A. Magera (kushoto waliosimama) wakishuhudia ufunguaji wa kontena lililokuwa bandari kavu Afri- ICD eneo la Tazara Jijini Dar es Salaam tayari kwa  kuchukua sampuli ya mbolea kuipeleka maabara, wa pili kulia ni Afisa Mgomboaji (Clearing and Forwarding Officer) wa Pamyco  Lucas Yonas.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ametoa siku tatu (3) kwa wakazi wa Kata ya Haubi iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kuhakikisha wanarudisha anuani za Makazi zilizo wekwa na serikali kwa ajili ya utambulisho ajili kwa Wananchi wote waliotoa huku akiwaeleza hatua za kisheria zitachukuliwa kwa watakaoenda kinyume na maelekezo hayo.

Kauli hiyo imetolewa Septemba 15,2023 wakati wa ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa ya kukagua miradi ya maendeleo na miundombinu mbalimbali katika shule mpya ya Sekondari katika Kata ya Bolisa, Shule mpya ya Sekondari Ntomoko iliyopo katika Kata ya Haubi sambamba na kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Kata ya Haubi, Ujenzi huo unatekelezwa kupitia Fedha za SEQUIP.

"Kawatangazieni na wengine tunatoa siku tatu kwa yeyote aliyetoa anuani za Makazi ahakikishe anarudisha sehemu husika alipotoa kwa asiyerudisha tutamfungulia mashitaka "amesisitiza Senyamule 

Aidha, Kiasi cha zaidi  ya shilingi  Millioni 544 zimewekwa kwenye account ya  Shule ya Sekondari Hubali kwa ajili ya Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Bolisa unaohusisha Jengo moja la Utawala, Vyumba nane vya madarasa, matundu nane ya vyoo vya wanafunzi, Jengo moja la Maktaba, Jengo moja la Tehama pamoja na  majengo matatu ya maabara .

Pia, Katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ilipokea kiasi cha zaidi ya shilingi Millioni 544 kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Ntomoko iliyopo katika Kata ya Haubi, mradi ambao unahusisha ujenzi wa Jengo moja la Utawala, Jengo moja la Tehema, Vyumba viwili vya madarasa na Ofisi moja, katika (BLOCK A na B ), Vyumba viwili vya madarasa (BLOCK C na D), Ujenzi wa madarasa matatu ,Jengo la Maktaba, matundu nane ya vyoo, kichomea taka ,chumba cha mahitaji maalum pamoja na tenki la maji ya ardhini.

Mhe.Senyamule amehimiza suala la Usalama wakati akijibu changamoto mbalimbali za wananchi wa Kata ya Haubi amewataka wazazi na walezi kusimamia malezi ya watoto wao ili kulinda mila na tamaduni pamoja na maadili ya  taifa.

"Suala la Usalama linaanza na sisi, tuanze wote kwa pamoja kwa kuchukua hatua za kusimamia malezi mazuri ili nchi yetu  isiwe na watoto wabakaji, walawiti, wavuta bangi na mmomonyoko wa maadili." Amesisitiza Senyamule 

Mkuu wa Mkoa huyo amewaasa vijana na watu wote wanaojishughulisha na kilimo na biashara ya bangi  kuacha mara moja kwani ni kinyume na taratibu za nchini ya Tanzania na kuwaagiza kuhakikisha kila mmoja anakuwa mlinzi wa mwenzake kwa kukemea na kutoa taarifa kwenye vyombo vya sheria. 

"Natoa shime mnajua bangi ni kinyume cha sheria na taratibu wengine tayari wapo ndani, kama kuna watu bado  wanaweka bangi ndani watumieni salamu, hatutaki vijana wetu waharibikiwe kama kuna wanaolima tuwakemee kwahiyo lazima kila mtu awe mlinzi wa mwenzake." Amesisitiza Mhe.Senyamule


Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith  Mahenge  (katikati) akizungumza na baadhi ya wajumbe wa kamati ya mbio za Mwenge wa Uhuru wakati wa akikagua Miradi ya Mwenge wa Uhuru itakayozinduliwa, kufunguliwa ,kuwekewe mawe ya msingi na kutembelewa.

Mratibu  Mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani  ambaye ni Afisa, akielezea kukamilika kwa maandalizi ya mbio za Mwenge wa Uhuru mkoani hapa
Ukaguzi wa miradi hiyo ukifanyika. 



Na Dotto Mwaibale, Singida


 MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith  Mahenge  amekagua Miradi ya Mwenge wa Uhuru itakayozinduliwa, kufunguliwa ,kuwekewe mawe ya msingi na kutembelewa.

Akikagua eneo la mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kati ya Mkoa wa Singida na Tabora i

Malendi Wilaya  ya Iramba Mahenge amewaomba wananchi, viongozi wa dini, Siasa, mashirika naTaasisi za Serikali na binafsi,vyama vya wafanyakazi pamoja na watumishi kushiriki kikamilifu katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru yatakayofanyika Tarehe 20/07/2021 na maeneo yote ya miradi pamoja  mikesha.

Mkuu wa Mkoa amewahakikishia Wananchi kuwa tahadhari zote za ugonjwa wa corona zitachukuliwa muda wote hadi  Mwenge wa Uhuru utakapo kabidhiwa Mkoa wa Dodoma Tarehe 25/07/2021.

Mratibu  Mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani  ambaye ni Afisa Vijana mkoa amemuhakishia mkuu wa mkoa wa Singida kuwa maandalizi yote muhimu yamekwisha fanyika katika wilaya zote za mkoa kwa ujumla.

Mwenge huo katika Mkoa wa Singida utakimbizwa katika wilaya tano za kiutawala  ambazo ni Iramba, Mkalama, Singida, Ikungi na Manyoni.

 
Muonekano wa sehemu ya uanzishwaji wa barabara mpya ya Mwandiga hadi Mwamgongo mkoani Kigoma inayokadiriwa kuwa na urefu wa kilometa 65 baada ya kukamilika kwake. PICHA NA WUU

Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Asa Makanika, akimuelezea jambo Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, wakati Naibu waziri huyo akikagua mradi wa uanzishwaji wa barabara mpya ya Mwandiga hadi Mwamgongo mkoani Kigoma inayokadiriwa kuwa na urefu wa kilometa 65 baada ya kukamilika kwake.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Kigoma, Mhandisi Narcis Choma, akitoa maelezo ya ujenzi wa daraja dogo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, katika mradi wa uanzishwaji wa barabara mpya ya Mwandiga hadi Mwamgongo mkoani Kigoma inayokadiriwa kuwa na urefu wa kilometa 65 baada ya kukamilika kwake. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Asa Makanika.


Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Kigoma, Mhandisi Narcis Choma (kushoto), wakati akikagua ujenzi wa daraja dogo katika mradi wa uanzishwaji wa barabara mpya ya Mwandiga hadi Mwamgongo mkoani Kigoma inayokadiriwa kuwa na urefu wa kilometa 65 baada ya kukamilika kwake. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Asa Makanika.

 

Imeelezwa kuwa Serikali imeanza ujenzi wa barabara ya Mwandiga- Chankere - Mwamgongo (Km 65) kwa kiwango cha changarawe ili kurahisisha huduma za usafiri na usafirishaji kwa wananchi wa jimbo la Kigoma Kaskazini na mikoa jirani kwa ujumla.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, wakati wa ziara yake mkoani Kigoma alipokuwa akikagua barabara hiyo.

Kasekenya, amesema kuwa nia ya Serikali ni kuifungua barabara hiyo na kuikamilisha kwa kiwango cha changarawe ambapo imekuwa ikitenga fedha mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo.

"Nimefika na nimejionea mwenyewe na sasa ni utekelezaji zaidi, niwahakikishie wananchi wa Kigoma Kaskazini kuwa Serikali ipo kazini na barabara hii itaendelea kutengewa fedha kila mwaka ili kuhakikisha inakamilika", amesema Kasekenya.

Amemtaka Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Kigoma, Mhandisi Narcis Choma, Kuhakikisha ujenzi wa barabara hiyo unafika hadi Kagunga na ipitike wakati wote, pamoja na kuhakikisha kuwa anaweka zege kwenye maeneo yenye miinuko mikubwa sana na kuweka makalvati mengi na imara kwenye maeneo yenye maporomoko ya maji.

Kwa upande wake, Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini, Mheshimiwa Asa Makanika, amesema kuwa Barabara hiyo ni muhimu kwani ni mkombozi kwa watu wa Kigoma Kaskazini na pia itarahisisha huduma za usafiri na usafirishaji hususan katika kata za Ziwani, Mugongo na Kagunga.

"Tunategemea barabara hii kuwa mkombozi kwa wananchi wa huku, kwani kwa sasa wananchi wengi hutumia usafiri wa majini kufuata huduma muhimu kama za kiafya na elimu na wanatumia masaa Saba kufika mjini, naamini kujengwa kwa barabara hii kutakuwa ni kicheko kwa wananchi wangu, amesema Mheshimiwa Makanika.

Naye, Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Kigoma, Mhandisi Narcis Choma, amesema kuwa mpango uliopo sasa ni kuweka uzio pembeni ili kuzuia magari kuanguka hasa kwenye miinuko mikali.

Ameongeza kuwa tangu mwaka wa fedha 2018 /2019 Serikali imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo kwa kwa kiwango cha changarawe na kufafanua kuwa mpaka sasa eneo la kilometa nane la mlima limeshakatwa na linapitika.
 

 
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka akizungumza katika mkutano wa pamoja baina ya Viongozi wa Mkoa huo na Wafanyabiashara wadogo wadogo.Mmoja wa Wafanyabiashara wadogo wa Jiji la Dodoma aliyetambulika kwa jina la Dangote akitoa maoni yake kwenye mkutano wa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka.
Wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma wakiwa wanamsikiliza Mkuu wa Mkoa, Anthony Mtaka katika mkutano wa pamoja uliolenga kutatua changamoto za wafanyabiashara hao.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka amewaruhusu wajasiriamali wa Jiji la Dodoma kufanya biashara zao hadi usiku huku akiahidi kuwaboreshea miundombinu.


RC Mtaka ameyasema hayo jijini Dodoma alipokua akizungumza na wafanyabiashara wadogo wadogo ambapo ameahidi Serikali ya Mkoa itashughulikia changamoto ya taa za Barabarani pamoja na kuhakikisha ulinzi wa uhakika unakuepo masaa yote.

Ametoa kauli hiyo alipokua akijibu swali la mmoja wa wamachinga hao aliyeomba kuongezewa kiwango cha muda wa kufanya Biashara zao, ndipo RC Mtaka aliporuhusu kufanya biashara zao hadi asubuhi.

" Hili eneo la Nyerere Square ambalo mnafanyia biashara hatuwezi kuwaongezea muda kama mnavyotaka muwe mnaanza kufanya biashara asubuhi, hatufanyi hivyo kwa kuwa hili ni eneo la Barabara ndio maana tukatoa kibali muwe mnaanza biashara zenu hapa jioni.

Lakini sasa kwa kuwa Dodoma ni Jiji tutaufanya mchana kuwa mrefu zaidi ya usiku kwa maana sasa mnaweza kufanya biashara zenu hadi asubuhi, niwaahidi tutaboresha miundombinu ya taa na patrol ya Polisi itakua inapita kuhakikisha usalama upo muda wote," Amesema RC Mtaka.

Aidha RC Mtaka pia amewataka wafanyabiashara hao wadogo wadogo kuzingatia sheria na kanuni za kufanya kwao biashara ili wasilete athari kwa wananchi wengine wakati wanatimiza majukumu yao.

RC Mtaka pia amewataka viongozi wa Serikali kuanzia mamlaka za chini kutokuwa kikwazo kwa wafanyabiashara hao na badala yake wawe sehemu ya kuwawezesha kukua kibiashara na kufikia malengo yao.

Mkutano huo uliwahusisha Wafanyabiashara wadogo kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Tawala wa Mkoa Dk Fatma Mganga, Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Dodoma,Wakuu wa Wilaya na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde.


Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi

MAONI YA WADAU JUU YA BAJETI KUU YA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA 2021/2022

11JUNE 2020.

Mkurugenzi wa Afya na Lishe ya Jamii kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Ray Masumo akisoma hotuba yake wakati wa kufunguwa semina kwa waandishi wa habari iliyokuwa na lengo la kuwajengea uwezo wanahabari kuhusiana na ulaji unaofaa na mtindo bora wa maisha ili kuepuka jamii kupata magonjwa yasiyo ya kuambukiza leo Juni 10,2021 katika ukimbi wa mikutano wa tasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo ya Lishe , Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) Dkt. Esther Nkuba akizungumza jambo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi semina kwa waandishi wa habari kuhusu ulaji unaofaa na mitindo bora ya maisha.kulia ni Mkurugenzi wa Afya na Lishe ya Jamii kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Ray Masumo.
Afisa Lishe Mtafiti Mwandamizi, Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) Bi. Julieth Shine akiwafundisha waandishi wa habari kuhusu Lishe na magonjwa sugu katika semina iliyoandaliwa na Taasisi ya hiyo jijini Dar es Salaam.
Afisa Mawasiliano Mtafiti, Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) Bw. Fredy Lwoga akieleza katika semina jijini Dar es Salaam kuhusu wajibu wa waandishi wa habari katika kuelimisha jamii kuhusu ulaji unaofaa na mitindo bora ya maisha.


Mkutano ukiendelea.

 MKURUGENZI wa Afya na Lishe ya Jamii kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Ray Masumo, amesema kwamba waandishi wa habari ni wadau muhimu katika kutoa taarifa za lishe bora pamoja na kukabiliana na magonjwa.


Dkt. Masumo amesema hayo Juni 10,2021 wakati wa kufunguwa semina kwa waandishi wa habari iliyokuwa na lengo la kuwajengea uwezo wanahabari kuhusiana na ulaji unaofaa na mtindo bora wa maisha ili kuepuka jamii kupata magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

“Magonjwa yasiyo ya kuambukizwa yanasababishwa na ulaji usiofaa na mtindo isiyo bora ya maisha, kwa kula vyakula venye chumvi nyingi na mafuta mengi au vinywaji vyenye sukari nyingi pia ni miongoni mwa viashiria hatarishi kwa magonjwa yasiyo kuambukiza” amesema Dkt. Masumo.

Amefafanua kuwa mtindo isiyo bora ya maisha ni kutofanya mazoezi, matumizi ya sigara na tumbaku pamoja na unywaji wa pombe ambavyo usababisha mtu kupata magonjwa yasiyo kuambukiza.

Ameongeza kulingana na tafiti mbalimbali za hivi karibuni zinaonesha kumekuwa na ongezeko kubwa la watu wenye uzito uliozidi pamoja na unene uliopitiliza.

Dkt. Masumo ambaye alikuwa anamwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, amesema kuwa pia kuna ongezeko la magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama kisukari, saratani pamoja na magonjwa ya moyo na shinikizo la damu.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo ya Lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Dkt. Esther Nkuba, amesema kumekuwa na taarifa mbalimbali katika mitandao ambazo sio sahihi na kujenga hofu kwa wagonjwa.
Hivyo amesema ushiriki wa wanahabari katika semina hiyo ni fursa kwa kuandika taarifa za lishe uweledi kwa ajili kuelimisha jamii kuhusu ulaji unaofaa na mtindo bora wa maisha.

 

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha  ACP-Justine Masejo akizungumza na waandishi wa habari

Na Woinde Shizza, -ARUSHA
JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha kwa kipindi cha mwezi januari hadi Machi 2021, lilifanya operesheni maalum ya kupambana na madawa ya kulevya katika mkoa wa Arusha ambapo limefanikiwa kukamata watuhumiwa 157waliokutwa na madawa ya kulevya aina ya Heroine, Bhangi na Mirungi.

Akionge na waandishi wa habari Kamanda w polisi mkoa wa Arusha ACP-Justine Masejo alisema kuwa kufuatia Operesheni hiyo walifanikiwa kukamata watuhumiwa 12 wote wa Kiume wakiwa na madawa ya kulevya aina ya Heroine kiasi cha gramu 536 na jumla ya kesi 11 zimefunguliwa na zipo katika hatua mbalimbali.

Alisema kwa upande wa madawa ya kulevya aina ya bhangi, kesi 81 zilifunguliwa ambapo jumla ya kilogramu 114 na gramu 624 zilipatikana pamoja na watuhumiwa 87 kukamatwa kati yao wanaume 76 na wanawake 11 huku akibainisha kuwa kesi hizo zipo katika hatua mbalimbali za kiupelelezi.

"Aidha katika operesheni hiyo tulifanikiwa kupata kilogramu 271 za Mirungi
ambapo jumla ya kesi 49 na watuhumiwa 58 walikamatwa kati yao wa
kiume 53 na wa kike ni 05 kesi hizo pia zipo katika hatua mbalimbali za
upelelezi."Alisema

Alibainisha kuwa jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linaendelea na operesheni kali dhidi ya wananchi wanaojihusisha na madawa ya kulevya pamoja na matumizi na biashara ya madawa ya kulevya na kusema kuwa hawata sita kuwachukulia hatua kali za kisheria pindi tutakapo wakamata ambapo pia aliwaomba wananchi kushirikiana na nao ilikutokomeza kabisa matumizi na Biashara ya madawa ya kulevya

Alitoa onyo kwa baadhi ya watu wachache wanaojihusisha na matumizi na biashara ya madawa ya kulevya kuacha mara moja biashara hiyo ya madawa ya kulevya ambapo aliwaomba wananchi wa mkoa wa Arusha kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa zinazohusiana na uhalifu na wahalifu ili mkoa uendele kuwa shwari asanteni.

Na,Jusline Marco;Arusha

Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini kupitia Idaya ya Jinsia limezindua mradi wa Afya wa mabadiliko ya mwili kwa kugawa taulo za kike na nguo za ndani kwa wanafunzi wa kike ambao ni wahitaji pamoja na vitabu 6000 vya makuzi kwa vijana wakike ambapo kila jimbo litapokea vitabu 1000 huku vitabu vya mimi mwili wangu na mungu 1500 vitatolewa kwa vijana wa kike na wakiume.

Akizindua  mradi huo Naibu Katibu Mkuu,Misioni na Uinjilisti wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati Mch.Jason Kahembe amesema kuwa mradi huo ambao utahusika na kuwasaidia watoto kike kupata vifaa vya kujikinga wakati wa hedhi umelenga kuwafikia watoto wa kike walio vijijini na wenye uhitaji mkubwa.

Aidha mch.Kahembe amewataka wazazi kuhakikisha wanatimiza mahitaji kamili ya watoto wa kike hasa mahitaji ya kibaiolojia kwani kundi hilo ndilo lenye chsngamoto kubwa katila suala zima la ukuaji wa mabadiliko ya mwili ambapo amewasihi akina mama kuwa karibu na watoto wao kwa kujenga mazingira yatakayomfanya mtoto kuwa wazi kuwaeleza mahitaji yao.

Vilevile ameongeza kuwa ukosefu wa mahitaji muhimu kwa mtoto wakike kunapelekea kuwepo kwa ushawishi mkubwa ambao unaweza kumuingiza mtoto huyo na ni chanhamoto kubwa ambayo wazazi wasipowasaidia ni rahisi kwao kujiingiza katika vitendo vya ukahaba ili waweze kutimiza mahitaji yao hivyo kupitia mradi huo ambao umefadhiliwa na wanafunzi wa kanisa la Denish Rutheran Mission lililopo nchini Denimac wataweza kuwafilia wasichana wengi zaidi.

Ameongeza kuwa ili mradi huo uweze kuwa endelevu ni jukumu la lila kanisa kutoa michango yao na kuweza kuwasaidia wasichana wenye changamoto ya vifaa vya kujihifadhi wakati wakiwa katika mzunguko wao wa hedhi.

Akitoa taarifa za utekelezaji wa mradi huo,Katibu wa Idara ya Jinsia kutoka katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati Bi.Loikelo Sanga amesema kuwa lengo la mradi huo ni kuondoa mtazamo hasi uliojengeka kwa jamii kwa kipindi cha vizazi vilivyopita kuhusiana na mabadiliko ya mwili kwa vijana wanapofikia umri wa kupevuka ambapo changamoto kubwa imeonekana kwa mtoto wa kike kwasababu hali hiyo huonekana kama ni uchafu au laana hivyo hupelekea mabinti hao kuona kama wametengwa na pengine kushindwa kabisa kuhudhuria masomo yao.

Ameongeza kuwa kama watekelezaji wa mradi huo wamekuja na mbinu ya kutoa elimu kwa jamii ili kuwasaidia watoto wa kike kujiamini,kuwa huru,kuwa na ujasiri katika vipindi vya hedhi pamoja na kumfanya kuwa chachu ya mabadiliko kwa wengine sambamba na kumuwezesha kufanya kazi zake za kawaida kwasababu wengi wao hukumbana na changamoto nyingi pindi wanapoingia katika mzunguko wao wa hedhi.

Pamoja na hayo Loikelo amesema lengo la kuwahusisha vijana wa kiume katika mradi huo ni ili kuondoa mtazamo hasi ambao jamii wanao hususani jamii ya kifugaji ili wajue kuwa ni mfumo ambao mungu aliuweka kwa wanawake wote.

Ameeleza kuwa kama idara wamajipanga kuwafikia wasichana walio katika maeneo ya vijijini kwa kuziangalia zaidi shule zilizopo katika majimbo 6 ya Dayosisi pamoja na shule za serikali kwa kulenga wasichana wenye uhitaji walio kwenye maeneo yasiyofikika ambayo yana changamoto hizo ambapo mkakati walionao ni kutoa mafunzo kwa wazazi ili kuweza kuondoa mtizamo hasi walionao kusudi kuweza kumfanya mtoto wa kike akaishi kwa amani ndani ya jamii inayomzunguka.

Awali akizungumza katika uzinduzi huo mwakilishi kutoka Denish Lutheran Mission Bi.Ruth Bach-Svenden amesema kuwa mradi huo ambao unazindiliwa katika majimbo yaliyo chini ya kanisa la KKKT unatokana na michango ya wanafunzi kutoka nchini Denimac kwa kujali na kutambua changamoto zinazowakumba watoto wa kike katika kipindi cha ukuaji.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini Kati Bi.Rose Makara amesema kuwa uzinduzi wa mradi huo katika Shule ya sekondani Ekenywa ni uwakilishi wa shule nyingine ambazo zitafikiwa na utekelezaji wa mradi huo ambapo amewataka watekelezaji wa mradi huo kuepuka laana ya Mungu kwa kuupeleka mradi huo kwa walengwa kwa uaminifu.

"Sisi Dayosisi tunajitahidi kutafuta mbinu zote njema za kuwasaidia ili katila kipindi cha ukuwaji muweze kupita salama na kuwa mfano wa mabadiliko chana katika jamii.'alisisituza katibu mkuu

Sambamba na hayo ameeleza kuwa mafanikio ya mradi huo ni kuweka mafunzo katika vitendo na kubadili mtazamo hasi uliojengwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine juu ya mabadiliko ya miili ambapo amesema kuwa ni matumaini kuwa mradi huo utakuwa na ufanisi mkubwa na kuwafikia walengwa halisi.
Na. Farida Ramadhani na Ivona Tumsime, WFM, Dodoma
Serikali imezitaka Taasisi zote za Umma kuhakikisha zinapata kibali cha Waziri wa Fedha na Mipango kabla ya kuanzisha mfumo wowote wa kielektroniki wa usimamizi wa fedha za umma kama ilivyoelekezwa katika Waraka wa Hazina.

Agizo hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James wakati wa hafla ya kupokea ripoti ya tathmini ya Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato na Usimamizi wa Fedha za Umma.

Bw. James alisema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango ndio yenye mamlaka ya kutoa muongozo wa uanzishwaji wa mifumo ya usimamizi wa fedha za umma na kutoa angalizo kuwa wote watakaokiuka agizo hilo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

“Nawasisitiza Maafisa Masuuli wote kuhakikisha mnapata ridhaa ya Wizara ya Fedha na Mipango kabla ya kufanya ununuzi, uundaji, usimikaji na utumiaji wa mfumo wowote wa kielektroniki wa usimamizi wa fedha za umma katika mafungu au Taasisi zenu kama ilivyoelekezwa katika Waraka huo”, alisisitiza Bw. James.

Alisema kuwa Serikali hufanya jitihada mbalimbali katika kuboresha na kuanzisha mifumo mbalimbali ya kielektroniki ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji mapato na kusimamia matumizi ya Fedha za Umma.

Alisema mpaka sasa Serikali imeshabuni na kutengeneza mifumo mikubwa ya kielektroniki minne ambayo ni Mfumo wa Ukusanyaji wa Mapato ya Kodi, Maduhuli, Tozo na Huduma Mbalimbali za Serikali (GePG), Mfumo wa Usimamizi na Udhibiti wa Matumizi na Malipo ya Serikali (MUSE), Mfumo wa Usimamizi wa Miradi ya Maendeleo (NPMIS) na Mfumo wa Usimamizi wa Misamaha ya Kodi.

Bw. James alibainisha kuwa Mfumo wa MUSE unawezesha Wizara, Idara zinazojitegemea, Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri zote, Wakala na Taasisi zingine za Serikali kusimamia na kudhibiti mapato, malipo ya matumizi ya kawaida na kulipa malipo kwa njia ya kiektroniki kupitia Benki Kuu na Benki za Biashara.

Akizungumzia Mfumo wa Usimamizi wa Miradi ya Maendeleo (NPMIS), Katibu Mkuu huyo alisema mfumo huo ulianzishwa ili kuiwezesha Serikali na wadau wengine kupata taarifa sahihi za miradi ya maendeleo kwa wakati.

Alisema kuwa kila Taasisi inayotaka kutekeleza mradi wowote wa maendeleo ni lazima ahakikishe kuwa inatumia mfumo katika kufanya maombi na utekelezaji wa mradi. Hakuna malipo au mgao wa pesa za maendeleo zitalipwa nje ya mfumo. Nazitaka taasisi zote zenye miradi inayotegemea pesa kutoka Serikalini kuhakikisha miradi yote iko kwenye kanzidata hii ya miradi”, alisema.

Katibu Mkuu huyo alisema Mfumo wa GePG ulianzishwa kwa lengo la kutatua changamoto mbalimbali za ukusanyaji mapato ikiwemo ugumu wa kupata taarifa ya makusanyo yanayofanyika kwa wakati huo huo, gharama kubwa za miamala inayohusu makusanyo ya Fedha za Umma, utaratibu usio rafiki kwa Mlipaji wa huduma za umma na machaguo machache ya njia za kulipia (Benki, Mitandao ya simu za mkononi au Mawakala).

Alisema pia Mfumo wa Usimamizi na Utoaji wa Misamaha ya Kodi ya Ongezeko la Thamani Serikalini umeanzishwa ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizokuwepo Serikalini katika zoezi zima la usimamizi na utoaji wa misamaha ya kodi ya ongezeko la thamani Serikalini ikiwemo Wizara/Taasisi/Halmashauri kuwasilisha Wizara ya Fedha na Mipango baadhi ya orodha za vifaa visivyokidhi vigezo vya kupata msamaha wa VAT.

Kwa upande wake Mtafiti aliyefanya tathmini ya Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanya wa Mapato na Usimamizi wa Fedha za Umma kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Joel Mtebe, alisema kuwa, alifanya utafiti katika taasisi za Serikali 271 kwenye mikoa 11 na kubaini kuwa mfumo umerahisisha ukusanyaji wa maduhuri ya Serikali kwa asilimia 87 kutokana na wananchi kutokwenda moja kwa moja katika ofisi kulipia huduma.

Naye Mhasibu Mkuu wa Serikali, Francis Mwakapalila, alisema kuwa Mifumo ya Fedha iliyoanzishwa na Serikali ukiwemo Mfumo wa Usimamizi na Udhibiti wa Matumizi na Malipo ya Serikali (MUSE), umeokoa takribani Shilingi bilioni tano zilizokuwa zikitumika kununua leseni za mifumo iliyokuwa ikitengenezwa nje ya nchi.

Kwa upande wa wanufaika wa mifumo hiyo akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Willium Erio, alisemakuwa Mfumo wa Ukusanyaji wa Mapato ya Kodi, Maduhuli, Tozo na Huduma Mbalimbali za Serikali (GePG), umesaidia kuongeza mapato kutoka Sh. bilioni 994 kwa miaka miwili iliyopita hadi takribani Sh. trilioni 1.1 kwa sasa.

Alisema kuwa ongezeko la mapato hayo umetokana na mifumo kuondoa mianya ya mapato kuvuja na kupungua kwa gharama za miamala.