Articles by "Magazeti CCM CHADEMA"
Showing posts with label Magazeti CCM CHADEMA. Show all posts

 

Uongozi wa umoja wa wanawake Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi UWT Mkoa wa Arusha  umefanya kikao  cha baraza la  mkoa ili kutoa utatuzi  wa changamoto walizokutana nazo katika ziara ya siku tatu iliyofanyika katika wilaya  ya Arumeru  mkoani humo ikiwemo   sekta ya afya ,ukatil  kijinsia na mikopo kwa wanawake. 

Miongoni  Mwa changamoto  zilizotolewa fafanuzi ni  pamoja na Zahanati ya  kata ya Maruvango   kukosa  vifaa tiba  na vitanda vya kujifungulia  wakina mama wajawazito  naseikali imekwisha andaa bajeti katika kutatua changamoto  hiyo katika vituo vyote vya  afya ambavyo vimekuwa na changamoto  kubwa.  amesema  DMO  Mganga mkuu wa wilaya ya  Arumeru Dr Maneno Focus 

Pia amesema  serikali unania njema na watu wake hususani kwa wakinamama kwa  kuendelea  kupambana na vifo vya mama na mtoto kwa kuboresha huduma  bora ya afya  

Afsa maendeleo  ya jamii wilaya ya meru frola  Msilu  amewataka maafisa maendeleo ya jamii wakata kuwana ushirikiano wakutosha  katika kufanya kazi huku akiwataka wakina mama ambao vikundi   vyao havirejeshi mikopo  kwa wakati warudishi ili wengine waweze

Ili kupinga swala la ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru  imeanzisha  vikundi mbalimbali  mashuleni vinavyotoa elimu  kwa wanafunzi  itakayo saidia kupunguza  ukatili wa kijinsia  kwa watoto huku wakishirikiana na wazazi kiwachukukia hatua wahusika. Amesema  frola Msilu. 

Nae Mkuu wa   wilaya  ya Arumeru Emmanuela Mtatifikolo Kaganda ameupongeza  uongozi wa UWT  kwa kazi wanazozifanya kwa manufaa ya wananchi huku akiahidi kuzifanyia kazi changamoto  zote zilizotolewa  na wananchi kufikana na fedha zilizotolewa na serikali katika sekta  ya Elimu bilion moja na million miasaba arobaini,  afya bilioni mbili na milioni miasaba na mikopo  isiyo nariba bilioni moja na milioni  mia moja sabini na sita. 

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Arusha Flora Zelothe  akiwa Mgeni rasmi katika baraza hilo amezungumzia swala la ukatili  linazidi kukua Siku baada ya Siku hivyo juhudi zi nahitajika. 

"Ukatili wa kijinsia Umekuwa ukifanyika asilimia 66.6 majumbani hii inatokana na  wamama kuwa bize na kutafuta kipato mda mwingi wanakuwa  makzini na katika biashara wakirudi nyumbani usiku wakiwa wamechoka nakupelekea kukosa  mda wa kumkagua mtoto wake. 

Pia amewataka wanawake  kuhamasishana kugombea   nafasi mbalimbali  katika uongozi  ili kufanikisha jambo hilo ni lazima wanawake  wawe  na umoja kwa kushikamana na kupendana. 

Nae mwenyekiti  wa UWT  Wilaya hiyo  Juliet Maturu ameushukuru uongozi wa mkoa kwa kutembelea katika wilaya yake na kuwataka viongozi  wa ngazi zote kuanzia vijiji mpaka tarafa kufanya kazi kwa kushirikiana na kujitoa. 



Sisi Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi, CCM (UWT) tumepokea kwa furaha kubwa kitendo cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kumtunuku Shahada ya Udaktari wa Heshima Rais na Mwenyekiti wa Chama chetu cha Mapinduzi, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Umoja wetu wa UWT tunampongeza Dkt Samia tukitambua juhudi zake zisizomithilika za kuleta maendeleo maridhawa nchini katika muda mfupi wa miaka miwili Ikulu.

Mwenyekiti wetu Dkt Samia, kama ambavyo amekuja na Falsafa yake ya  (4R) ya uongozi bora; Reconciliation (Maridhiano), Resiliency (Ustahamilivu), Reforms (Mabadiliko) na Rebuilding (Kujenga Upya), ameleta Mapinduzi makubwa katika kila Sekta nchini na hivyo anastahili kupongezwa. 

Ni dhahiri sasa kupitia falsafa hii ameirejesha Nchi katika uimara wake kiuchumi, kisiasa na kijamii tukizingatia ameipokea Nchi yetu katika wakati mgumu wa kuondokewa ghafla na Mtangulizi wake Rais Magufuli, gonjwa la Corona na Vita ya Urusi na Ukraine ambavyo kwa pamoja vimesababisha kushuka kwa uchumi si Tanzania pekee bali pia dunia kote.

Leo hii mahusiano ya Kitaifa na Kimataifa, Diplomasia ya kiuchumi, Haki za Binadamu, Demokrasia ya vyama vingi, Maendeleo ya watu, Umoja wa Kitaifa, Utu, amani, Usalama na Ulinzi wa wananchi na Nchi, Maslahi ya makundi yote nchini; wakulima, wafanyakazi na wafanyabiashara ni baadhi ya vitu vilivyoboreshwa kwa kiwango kikubwa ndani ya miaka miwili tu ya Dkt Samia madarakani. 

Dkt Samia kama Mwanamke wa kwanza kuwa Rais wa Tanzania tangu tupate Uhuru mwaka 1961, kupitia Uongozi wake makini ameithibitishia Tanzania na dunia kwamba kwa hakika Mwanamke akipewa nafasi anaweza. UWT tunajivunia sana Kiongozi wetu huyu mwanamke.

UWT tunaziomba Taasisi zote duniani zenye hadhi ya kutoa tuzo zimpatie tuzo za heshima Rais wetu bila kusita kwani ana kila sababu na hadhi hiyo. 

Mwisho UWT tunawaomba WaTanzania wote waendelee kumpa ushirikiano wa kutosha Rais wetu Dkt Samia ili aendelee kutuletea maendeleo lukuki WaTanzania wote na kupata moyo wa kuendelea kuiheshimisha Nchi yetu duniani.


Imetolewa na:

MCC Mary Pius Chatanda, 

Mwenyekiti wa UWT Taifa. 

Novemba 30, 2022.


 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo akifurahia jambo wakati akizungumza katika mkutano wa wanachama wa shina namba 1 katika kijiji cha mwambise kata ya Fubu, leo 12, julai 2021.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo  akizungumza katika mkutano wa wanachama wa shina namba 1 katika kijiji cha mwambise kata ya Fubu, leo 12, julai 2021.


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo akitoa Vitendea kazi kwa Balozi wa  shina namba 1 katika kijiji cha mwambise kata ya Fubu Ndg  Seth S Mwambandile, leo 12, julai 2021.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo  akikagua kikundi cha ngoma alipowasili katika ukaguzi  wa utekelezaji wa Ilani ya CCM  2020-2025 wa ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha mwambise kata ya Fubu, leo 12, julai 2021.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo  akizungumza na Wananchi na wanachama wa CCM  katika ukaguzi  wa utekelezaji wa Ilani ya CCM  2020-2025 waujenzi wa Zahanati ya kijiji cha mwambise kata ya Fubu, leo 12, julai 2021.

 Mwanachama Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bi Sambina Igende akifurahi wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM katika kikao Cha Wanachama wa Shina No 1 kata ya Ikama.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo (aliyevaa Barakoa)  akikagua  Ujenzi wa  Mabweni ya Wanafunzi wa kike katika Shule ya Sekondari Kafundo katika kata ya Ipinda , leo 12, julai 2021.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya Ndg Jacob Mwakasole pamoja na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kyela Ndg Patrick Mwampele  akitoka kugagua  Ujenzi wa  Mabweni ya Wanafunzi wa kike ( pichani nyuma) katika Shule ya Sekondari Kafundo katika kata ya Ipinda , leo 12, julai 2021. (Picha Zote na CCM Makao Makuu)

 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo akimtwisha Ndoo Kichwani ,Binti Beatrice Masasi katika Kijiji Cha Asweketa (kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Omari Mgumba mara baada ya kutembelea Mradi wa mamlaka ya Maji ya Mji Mdogo wa Vwawa wilayani Mbozi.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo akisaidia shuhuli ya Ujenzi wa daraja la idiwili kwenda idunda linalojengwa kwa gharamia kiasi cha shilingi Milioni90 hadi kukamilika kwake,julai 9 2021.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo akitoka kukagua ujenzi wa daraja la idiwili kwenda idunda linalojengwa kwa gharamia kiasi cha shilingi Milioni90 hadi kukamilika kwake,julai 9 2021
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo (kushoto) akizungumza katika mkutano wa Wanchama wa Shina no2 tawi la hasamba kitongoji cha senya (kulia) ni balozi wa Shina hilo ndg Edea Samuel (kulia) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Songwe, Ndg. Elynico Mkola julai 9 2021 wilayani Mbozi.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo akizungumza katika mkutano wa Wanchama wa Shina no5 tawi la Idogo kata ya Idiwili wilayani Mbozi julai 9 2021.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo (pili kulia) akigawa kadi ya CCM kwa Mwanachama mpya Ndg Rafael Sarawe Siwila,(kulia) ni balozi wa Shina Namba 2 Hasanda ndg Edea Samwel tonya kitongoji cha Senya, wilayani mbozi julai 9 2021.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo (pili kulia) akigawa kadi ya CCM kadi Mwanachama mpya Ndg MteniNzundwa Mwamlemela ,(kulia) ni balozi wa shina Namba 2 Hasanda ndg Edea Samwel tonya kitongoji cha Senya, Wilayani Mbozi julai 9 2021.

Wanachama wa Shina no 2 zaid ya 100 wakila kiapo mara baada ya kukabidhiwa kadi za CCM
Ndg. Fanuel Mkisi aliyekuwa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Vywawa kupitia CHADEMA mwaka 2020 akionesha kadi ya CCM mara baada ya kukabidhiwa na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkutano wa shina Namba 2 lililopo katika kitongoji cha Senya, Wilayani Mbozi julai 9 2021.

Mbunge wa Viti Maalum kutokea Mkoa wa Songwe Ndg Juliana Shonza akizungumza na Wanachama na Viongozi wa shina Namba 2 lililopo katika kitongoji cha Senya, Wilayani Mbozi julai 9 2021.


Mbunge wa Jimbo la Vywawa ndg Joseph Hasunga akizungumza na Wanachama na Viongozi wa shina Namba 2 lililopo katika kitongoji cha Senya, Wilayani Mbozi julai 9 2021.


Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Omari Mgumba akizungumza na Wanachama na Viongozi wa shina Namba 2 lililopo katika kitongoji cha Senya, Wilayani Mbozi julai 9 2021.

Bibi Anna Siwila Mwanachama wa Shina namba 5 kitongoji cha Senya, akifurahi Wilayani Mbozi julai 9 2021.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo (kulia) akisikiliza maelezo ya Mganga mkuu wa mkoa wa Songwe Dkt Nyembea Hamadi alipotembelea maabara ya Hospitali rufaa ya mkoa inayojengwa kwa gharama za shilingi milioni 997 ,wilayani mbozi julai 9 2021.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo akizungumza na viongozi wa serikali pamoja na watumishi wa hospitali ya rufaa ya mkoa mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali rufaa ya mkoa inayojengwa kwa gharama za shilingi Bilioni 4.5 ,wilayani mbozi julai 9 2021.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Songwe, Ndg. Elynico Mkola akipunga mkono kwa wanachama wa Shina no5 tawi la Idogo kata ya Idiwili wilayani Mbozi julai 9 2021.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo akizungumza na Wazee wa wilaya ya Mbozi jimbo la vywawa , julai 9 2021

 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Godfrey Chongolo pamoja na wajumbe wengine wa Sekretarieti ya CCM Taifa tarehe 9 Julai, 2021 ameendelea na ziara ya kuimarisha Chama Mashinani mkoani Songwe baada ya kumaliza mkoa wa Rukwa.

Katibu Mkuu akizungumza katika kikao cha mapokezi Wilayani Momba amewakumbusha wanaCCM majukumu makubwa mawili ikiwa ni kuendelea kukijenga na kukiimarisha Chama, pamoja na kufanya kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Katibu Mkuu ameongeza kuwa kuna vyama kazi zao ni kuikumbusha CCM na kuwafanya kuwa na bidii zaidi ya kuwahudumia wananchi, hivyo wanaCCM tuendelee kutimiza jukumu letu la msingi la kuongoza nchi, na wao tuwaache watimize jukumu lao.

Akianza ziara hiyo mkoani Songwe wilaya ya Mbozi, Katibu Mkuu amefanya mikutano ya Mashina na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ikwemo mradi wa Maji Kata ya Ihanda, Ujenzi wa Hospitali ya Mkoa wa Songwe pamoja kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Idiwila.

Aidha, Katibu Mkuu akiwa katika mkutano wa shina namba 02 Kata ya Hasamba, amepokea wanachama wa vyama mbalimbali vya upinzani zaidi ya 100 waliohamia CCM, wakiongozwa na Ndg. Fanuel Mkisi aliyekuwa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Vywawa kupitia CHADEMA mwaka 2020.