Articles by "CCM"
Showing posts with label CCM. Show all posts

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CPA Amos Makalla amesema kuwa Julai 26 2025 ndiyo siku ambayo Halmashauri Kuu ya CCM Taifa itafanya kikao chake cha kawaida, badala ya jana au leo kama ilivyotarajiwa hapo awali. 

Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchakato wa uchaguzi wa ndani ya chama cha Mapinduzi CCM.

"Wagombea ni wengi sana, kwa hiyo kazi ya kuchambua ni kubwa na sisi tunataka tutende haki na tuifanye kwa umakini. Kwa hiyo uteuzi wa mwisho utafanyika tarehe 28 na baada ya hapo kwenda kwenye kura za maoni." Alisema

Aidha, amesema kikao hicho cha kawaida kitatanguliwa na kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kitakachofanyika siku hiyo hiyo ya Julai 26, 2025. 

Makalla amesema kuwa, baada ya vikao hivyo kitafanyika kikao kingine cha Kamati Kuu ya CCM Taifa Julai 28, 2025 ambacho ni mahususi kwa ajili ya uteuzi wa wagombea wa chama hicho ngazi ya ubunge na udiwani watakaopeperusha bendera ya CCM.




NA DENIS MLOWE IRINGA

KATIKA kuhakikisha ushindi wa kishindo kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Iringa imefanya mafunzo maalum kwa makatibu wenezi wa kata 28 zilizoko katika wilaya hiyo.

Mafunzo hayo yameongozwa katika ilani ya chama hicho 2025-2030 yenye vipaumbele ambavyo makatibu wenezi wa wilaya hiyo kutumia katika kukinadi chama cha mapinduzi kwa wananchi yenye kuwaletea maendeleo chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kuweza kuibuka na ushindi.

Akizungumza katika mafunzo hayo Katibu wa Sasa na Uenezi wilaya ya Iringa Vjijini Anold Mvamba alisema Ilani ya uchaguzi inawahusu wanachama na viongozi wa CCM hivyo wanaumuhimu mkubwa wa kuisoma na kuelewa pindi wakienda kwa wananchi watoe elimu faida ya ilani hiyo katika kuelekea maendeleo ya wananchi kwa ujumla kutokana na ubora wake.

Mvamva alisema kuwa mafunzo hayo kwa wenezi yamefanyika kwa kuwa ilani hiyo waisome na kuielewa vizuri kwani imegusa nyanja mbalimbali ikiwemo sekta ya Kilimo, Afya,Elimu,Nishati.

"Naomba sana mkasome ilani hii iwafikie wananchi na kujipa ushindi wa kishindo chama cha mapinduzi CCM kuelekea uchaguzi mkuu wa October 2025 kwani chama cha mapinduzi chini ya Mwenyekiti wake Taifa Rais Samia mambo makubwa yamefanyika kwa miaka michache tangu aliposhika serikali na kuwaletea maendeleo wananchi na ilani hii ni funga kazi." Alisema

Naye Katibu wa CCM wilaya ya Iringa vijijini  Sure Mwasanguti alisema makatibu wenezi wanapaswa kufahamu katiba ya chama na maelekezo ya chama hasa katika kuelekea uchaguzi mkuu huku akiwakumbusha kutimiza wajibu wao na kuhakikisha chama cha Mapinduzi kinashinda kwa kishindo kwani ilani imetekelezwa vizuri na ilani ya 2025-2030 imejielekeza kutatua changamoto za wananchi.

Mgeni wa heshima katika mafunzo hayo Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa vijiji Ndugu Constantino Kihwele amewataka  wenezi hao kutambua nafasi zao na kutobeba wagombea kwani
chama kinakwenda kupata wagombea wenye sifa ambao watapeperusha bendera ya CCM katika nafasi zote.

Kihwele amewataka wenezi hao kueleza mambo ya maendeleo yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita huku akiahidi kura za kishindo kwa wagombea wote wa CCM kwani kazi iliyofanywa na Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Samia yatapeperusha bendera ya CCM kwa kura za kishindo.

Baadhi ya wenezi walisema kuwa watahakikisha ilani hiyo inasambazwa kwa nguvu zote kwa wananchi waelewe kwani imewagusa wananchi wa matabaka yote na vipaumbele vinavyogusa wananchi.

Aidha wamepongeza uongozi wa wilaya kwa kuwapatia mafunzo ambayo yataleta chachu katika kuleta ufahamu, nia na malengo ya CCM katika kuwaletea vipaumbele wananchi kupitia ilani ya 2025- 2030.


 Wadaia kugawa hongo kati ya Sh.5000 na Sh.50,000 ,Mbunge mwenyewe atoa majibu


Na Shomari Binda,Rorya

WAKATI joto la uchaguzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), likianza kupanda kwa baadhi ya majimbo imeelezwa katika Jimbo la Rorya

mkoani Mara wajumbe waliokuwa wakipatiwa mafunzo ya utendaji ndani ya Chama hicho wamedaiwa kupewa fedha kati ya Sh.5000 hadi Sh.50,000 kama sehemu ya kuwashawishi wajumbe hao kuelekea uchaguzi mkuu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo zinaeleza kwamba juzi katika mafunzo ya watendaji ndani ya Chama Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rorya, Ongujo Wakibara kwa kushirikiana na mbunge wa Jimbo hilo, Jafari Chege wanadaiwa kuyavuruga kwa kumwaga hongo kwa wajumbe wa mafunzo hayo.

Wakati wa mafunzo hayo inadaiwa Mbunge Chege na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rorya, Ongujo Wakibara waliingilia katika semina ya makatibu wa matawi na kata iliyofanyika Februari 20, 2025 ambapo wanadaiwa kugawa posho kiasi cha Shilingi 50,000 kwa kila katibu aliyehudhuria mafunzo hayo.

Tuko hilo ambalo liliibua mjadala katika makundi sogozi ya ya WhatsApp ya CCM Mkoa wa Mara ambapo yameeleza utaratibu huo unakiuka maelekezo kutoka makao makuu ya CCM Taifa.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa mafunzo hayo ya watendaji yasiingiliwe na viongozi au wanasiasa kwa sababu ni mafunzo ya kiutendaji na chama kilisema kitagharamia kila kitu ikiwemo chakula na posho.

“Lengo la chama kufanya hivyo ilikuwa ni kuondoa urasimu wa wagombea kutumia nafasi hiyo kutoa rushwa kinyume chake Mwenyekiti wa chama na mgombea wake ambaye ndiye mbunge kwa sasa wamevamia ukumbi na kutoa posho hizo.

“Jambo hili halijawafurahisha hata wakufunzi haswa kauli za Mwenyekiti na Mbunge baada ya kuzuiwa na wakalazimisha kufanya kwa nguvu,” imesema sehemu ya taarifa katika makundi hayo sogezi ya WhatsApp

Hata kupitia Gazeti tando la George Marato Tv, imefatilia taarifa hiyo na kuzungumza na Mbunge wa Jimbo la Rorya, Jafar Chege kwa njia ya simu na kudai yupo msibani toka asubuhi na hajaudhuria kikao hicho na kushangazwa na taarifa hiyo.

Hata hivyo Chege alikiri kuiona taarifa hiyo kwenye makundi sogozi ya CCM lakini hajui lengo lake.”Nimeshangazwa na taarifa hiyo,nipo msibani na nimeambiwa kikao hicho kimeenda vizuri na kimalizika salama hizo taarifa ni za uongo,” amejibu Chege alipokuwa akielezea taarifa hiyo.

Alipotafutwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rorya, Ongujo Wakibara hakupatikana kwenye simu yake ya mkono hivyo jitihada za kumtafuta kuzungumzia jambo hili zinaendelea ili kupata ukweli wa madai ya taarifa hizo.

Hata hivyo pamoja na hali Mwenyekiti huyo wa CCM anadaiwa kuwa amekuwa akiwasimamisha viongozi hovyo hovyo na hivi karibuni katika Kata za Mkoma, Kirogo, Kinyenche, Nyathorogo, Goribe na Tai aliwasimamisha vongozi wa matawi bila kuihusisha kamati ya siasa.

Wakati kwa Mbunge Chege amekuwa akizunguka katika baadhi ya kata na matawi na kukutana na wajumbe moja kwa moja na kugawa fedha kiasi cha Shilingi 5,000 hadi Sh.50,000 kulingana na uwezo na hadhi ya mjumbe.

 



Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemteua rasmi Mwenyekiti na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa mgombea wa urais kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Uamuzi huu wa kihistoria unaonyesha imani kubwa na matumaini makubwa ambayo CCM inayo kwa uongozi thabiti na wa kimkakati wa Rais Samia, pamoja na dhamira yake isiyotetereka ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.

Katika kipindi chake cha uongozi, Tanzania imeshuhudia mafanikio makubwa katika ukuaji wa uchumi, ujenzi wa miundombinu, maboresho ya huduma za afya, na kukuza demokrasia kupitia falsafa yake ya “4Rs.”

Akiwa Rais wa kwanza mwanamke katika historia ya Tanzania, Rais Samia si tu kwamba amevunja vikwazo vya kijinsia, bali pia ameweka viwango vipya vya uongozi shirikishi na wa maono.

Uteuzi wa CCM ni hatua muhimu ya kuhakikisha maendeleo yanayoendelea na mustakabali wa neema kwa Watanzania wote.











 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ameongoza Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa kutembelea Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma ili kukagua maendeleo ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaotarajiwa kufanyika tarehe 18 na 19 Januari 2025.


Ukumbi huo, wenye uwezo wa kuchukua takriban watu 3,000, unakarabatiwa kwa kiwango cha juu ili kuhakikisha mazingira bora kwa mkutano huo muhimu. Mkutano huu utakuwa na agenda kadhaa, ikiwemo kumchagua Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), kufuatia kujiuzulu kwa Komredi Abdulrahman Kinana mwaka jana.

Balozi Nchimbi, akiwa ameambatana na Manaibu Katibu Mkuu wa CCM, John Mongella (Bara) na Dkt. Mohamed Said Dimwa (Zanzibar), pamoja na wajumbe wa Sekretarieti, alishuhudia kasi kubwa ya maandalizi hayo, huku akiwapongeza wahusika kwa jitihada zinazofanywa kuhakikisha kila kitu kinakuwa tayari kwa wakati.

Kwa mujibu wa Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla, maandalizi ya mkutano huo yamefikia hatua nzuri. Alitangaza rasmi kuanza kwa maandalizi hayo jana, tarehe 7 Januari 2025, akibainisha kuwa mkutano huo utaongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan.




 

Katibu siasa na uenezi wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Geita Ndg Gabriel Nyasilu  ameitaka jamii ya wana kijiji cha Chankolongo kata ya Bukondo Wilayani Geita kukemea na kufichua waharifu wanaojihusisha na ukatili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) kwa kuwafichua kwenye vyombo vya Dola Kabla hawajatekeleza ukatili huo ambao umekuwa ukidhurumu haki za kuhishi kwa Watu wenye ulemavu huo.


Nyasilu Ameyasema hayo wakati wa Hafra ya kuzindua nyumba ya kuishi ya Mzee Mussa Kabaka  ambaye pia ni Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Chankolongo kilichopo Kata ya Bukondo Wilayani Geita.

Amesema walemavu wa ngozi wana haki yakuishi ,Mungu kawaumba ili wafurahie maisha hivyo ni wajibu wa jamii nzima kuhakikisha wanawalinda watu hao.
"Mtu kuzaliwa Mlevu wa ngozi akupanga ni Mungu ndiye amepanga lakini kuna Watu Ambao wamekuwa Awana hofu ya Mungu wamekuwa wakiwadhuru wa madai watapata mali niwaombe tupinge vikali dhana hizi potofu"Alisema Gabriel Nyasilu.


Katika hatua nyingine Mwenezi Gabriel Nyasilu amewataka wanachi wa kijiji hicho kujitokeza kwa wingi wakati wa kujiandikisha kwenye Daftari la makazi ili waweze kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliopo mbele yetu Mwaka huu 2024.

Huku akiikumbusha jamii ya kata ya Bukondo na Geita kwa ujumla kuwa uchaguzi huu unaotokana na Mfumo wa vyama vingi usitumike kuwagawa na kuwagombanisha , Kwani
Wote ni watanzania kamwe wasikubali na kugawanywa na kugombana kwa sababu ya vyama vyao.

 "Niwaombe Sana twende tukashiriki Uchaguzi wa Serikali za mitaa,Vijiji na Vitongoji kwa Amani ,upendo huku tukiilinda Amani ya nchi yetu"Alisema Gabriel Nyasilu .


Kwenye Ufunguzi huo Nyasilu  ameongoza  Harambee na kuwezesha upatikanaji wa Tsh 9,000,400/= Kwa ajiri yakusaport ujenzi wa Nyumba hiyo huku yeye Mwenyewe akichangia kiasi cha Tsh 500,000/=

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa kijiji cha Chankolongo Mzee Mussa Kabaka  amempongeza na Kumshuru katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Geita kwa kukubari wito wa kuwa Mgeni Rasmi katika hafra ya uzinduzi wa Nyumba yake.

Mwisho..


Na Joel Maduka,Geita..

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM ,Mkoa wa Geita,Nicholaus Kasendamila amefunga rasimi mafunzo ya itikadi kwa vijana wa CCM ,huku akisisitiza  suala zima la vijana  kuzingatia usalama wao wenyewe na usalama wa Nchi.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita ametoa Wito huo wakati akizungumza na zaidi ya vijana mia sita ambao walikuwa kwenye mafunzo ya itikadi ambayo yamefanyika Kata ya Nyakagomba Wilayani Geita.

Amesema wao kama vijana wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kujilinda na vitendo viovu ambavyo vinaweza kuhatarisha maisha yao ya sasa na baadae.

“Natambua vijana nyie bado Taifa linawaitaji na bado mnanguvu Kubwa kwa Taifa letu lakini niwaombe sana zingatieni suala la usalama wenu na wa Nchi vijana wengi wamepotea sababu ni kukosa nidhamu na kujikuta wakijiingiza kwenye makundi ambayo yameendelea kugharimu maisha yao ya kila siku”Amesema Nicolaus Kasendamila.

Naye Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Geita Manjale Magambo amesema uwepo wa makambi ya vijana yamekuwa na faida nyingi kwa vijana kutokana na kuwajengea uwezo wa kujitegemea na kujikwamua kiuchumi na kusaidia kukijua chama zaidi kutokana na mafunzo ya Historia ambayo yanatolewa.

 






Na Joel Maduka ,Geita

Mjumbe wa Halmashuri kuu ya CCM Taifa ,  MNEC Chacha Wambula (WAJA) akiwa wilayani Bukombe Mkoani Geita amewataka vijana kutojiingiza katika Makundi yasiyofaa kwani yanaweza kuleta athari Kubwa  kwenye Jamii.

 Hayo ameyasema wakati alipokuwa akifunga Makambi ya Umoja wa Vijana  wa CCM (UVCCM)  wilaya ya Bukombe yaliyodumu kwa kipindi cha siku sita Wilayani humo huku akiwataka vijana hao kuzingatia  yale yote waliyofundishwa yaweze kuwa na  tija kwa Jamii na pamoja na chama cha Mapinduzi(CCM).

 Aidha Mnec Chacha amewataka vijana kuzingatia suala zima la uzalendo kwa Nchi na kutangaza matendo mema ambayo yamefanywa na Serikali ya awamu ya sita(6),huku akisisitiza uwajibikaji na uchapakazi kwa vijana.

 “Niwaombe vijana wangu najua hapa mmefundishwa mambo mbalimbali yakiwemo ya ujasiriamali nendeni mkatumie yale ambayo mmefundishwa kwenda kuanzisha miradi ya kiuchumi mimi nipo tayari kuwasapoti wale ambao wataitaji msaada wangu”Amesema Chacha Wambura.

 “Mimi nimaamini katika vitu vitatu uchapakazi,kuwa mwaminifu na kuwa muwazi kama unavitu hivi leo hii uwezi kukosa kazi lakini kama wewe kitu kimoja wapo kinakosekana hata ukifanya kazi utaondolewa kazini,Elimu ni kitu kingine unaweza kuwa na elimu na ukakosa hivi vitu elimu yako isikusaidie”amesema Chacha Wambura.

 Aidha Mnec Chacha amewaomba vijana kujifunza desturi ya utii  kwani sio utumwa kwa kijana kuwa mtii na kuheshimu mamlaka muhimu ambazo zimewekwa na Nchi pamoja na serikali.



 


Mjumbe kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Singida  Ndg Ahmed Misanga ambae pia ni mratibu wa shughuli za wazazi ikungi  ametoa Vifaa Vya ujenzi wa nyumba ya Mtumishi wa Jumuiya hiyo

Misanga Ametoa Vifaa hivyo  alipo tembelea na kujionea maendelo ya ujenzi huo.

"Nimetoa vifaa hivii ikiwa ni muendelezo wa Michango yangu katika  ujenzi wa nyumba ya Mtumishi wa wazazi  wilayani ikungi leo nimeleta Saruji , nondo , pesa ya ufundi kwa ajili ya kufunga lentha katika jengo hili" Misanga

" Pia tutaendelea kutoa michango yetu ili jengo hili liweze kukamilika kwa wakati na mtumishi aweze kuingia ndani,"

" Na tunamipogo wa kununua fenicha za ndani ili mtumishi akijaa  aje na mabegi  tu ili asipate tabu siku ya kuhama kama atakuwa amepata uhamisho wa kwenda mkoa mwingine,".

Huku katibu wa Jumuiya ya  wazazi walaya ya ikungi Bi HAWA GIDABUDAYI ameshukuru Mjumbe kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Singida  Ndg Ahmed Misanga kwa kujitowa kwake kwa ajili ya jumuiya hiyi kwa kutoa Vifaa vya  ujenzi wa nyumba hiyo ya  mtumishi.

" Kwani hili zoezi la kujenga nymba za watumishi ni agizo la kutoka makao makuu na sisi tumeadha kulitekeleza kwa vitondo na kwa sasa tupo hatua ya Kufunga Lentha paka ifikapo mwezi wakumi kila kitu kitakuwa kimekamilika na mtumishi ataingia ndani," Amesema 

Huku mwenezi wa chama cha mapinduzi wilaya ikungi Ndugu .NASSORO ISSAH Amesema chama kinawajubu wa kusimamia jumya zake ili ziweze kutimiza malengo yake.

 "Hizi nyumba zitasaidia sana watumishi wetu wanaokuja huku wilayani kwani akifika tu  anasehemu ya kulala, namini atafnyakazi zake kwa utulivu na kwa umakini kwasababu anasehemu ya uhakuka ya kuishi,".

" Sasa mtumishi wa wilaya ya ikungi akae tayari kuhamia baadaa ya lentha tunakwenda kupaua na kumalizia nyumba hiyo, " Ameongeza






 MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndg. Abdulrahman Kinana, amesema msaada mkubwa wa haraka unahitajika kwa wananchi walioathirika na mafuriko wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani.


Amesema hayo baada ya kupokea taarifa na kushuhudia hali ilivyo wilayani humo, ambapo kata 12 kati ya 13 zimeathirika, na kutaka serikali kuharakisha misaada kikiwemo chakula na malazi kwa zaidi ya watu 88,000 walioathirika.

Kinana ametoa wito huo leo, Aprili 9, 2024, alipokuwa akizungumza na wananchi wa vijiji vya Muhoro na Chumbi, baada ya kuwatembelea na kuwapa pole wananchi waliokumbwa na mafuriko hayo, yaliyotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha Mto Rufiji kufurika katika makazi ya watu.

"Nimezungumza na Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa), kwa namna nilivyojionea na nimemweleza uharaka wa Mahitaji, sina shaka hata kidogo na yeye atakuja kujionea. Haraka ameitisha kikao na mawaziri wote wanaohusika na maswala ya maafa, nina hakika akishakuja hapa kasi ya kutoa huduma itaongezeka ” amesema.

Amesisitiza kuwa, kutokana na hali hiyo anaihimiza serikali kuongeza juhudi za kutoa huduma kwa wananchi waliopatwa na maafa hayo ambayo yameathiri pia shule na zahanati.

“Nimekuja kuwapa pole kwa niaba ya Rais, kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Nimekuja kujionea hali ilivyo, lakini niendelee kutumia fursa hii kuihimiza serikali kuleta misaada haraka kwa wananchi walioathirika," amesisitiza Makamu Mwenyekiti Ndg. Kinana.








 Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahmani Kinana, amesema kuwa, Waziri Mkuu Mstaafu Edwar Lowassa ni kiongozi wa mfano hususan katika uwajibikaji na kuwaunganisha Watanzania bila ya kujali imani zao.

Kinana ameyasema hayo katika ibada ya Shukrani ya Hayati Edward Ngoyai Lowassa Waziri Mkuu Mstaafu iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Monduli Mjini Mkoani Arusha, marchi 24, 2024.

“Ndugu Lowassa tutamkumbuka kama kiongozi mzalendo kwa taifa hili. Alikuwa mzalendo,alikuwa mchapakazi, alikuwa mtu aliyetufundisha uwajibikaji, mtu aliyefahamika akiamua jambo lake anatimiza.

“Kuna jambo leo hii linazungumzwa hapa nchini, jambo linaitwa uwajibikaji, kama kuna darasa la uwajibikaji basi darasa hilo litakuwa Edward Ngoyayi Lowassa,” amesema.

Mbali na hilo, kinana amesema kuwa hayati Lowassa atakumbukwa kwa namna alivyowaunganisha Watanzania bila ya kujali itikadi zao.

“Baba askofu umezungumza sana  juu ya umoja wa Watanzania na ukasisitiza kwamba tofauti zetu za kiimani tofauti zetu za kikabila, za kimaeneo ziwe ni tofauti zinazotuunganisha kutufanya tuwe kitu kimoja.

“Ukaongeza kusema kwamba siku hizi kuna utamaduni mzuri zaidi unaoimarisha umoja wetu, dini zote zinashirikiana, mimi ni shahidi, ndugu Lowassa amechangia misikiti mingi sana nchini, na ni muhimu kumuogopa Mungu, kumuabudu Mungu,” ameeleza.

Amesema kinachowaunganisha Watanzania ni kushikamana, kuwa wamoja, kuwa ndugu bila ya kujali dini, vyama, itikadi wala makabila.

“Ninawaomba Watanzania wote tuendelee kushirikiana, tuendelee kuimarisha umoja na amani, ya nchi yetu kwani bila ya amani, bila ya umoja, undugu na mshikamano mambo mengine hayawezekani, kila mmoja wetu kwa imani yake tuendedelee kumtanguliza Mungu na wote tukimtanguliza Mungu nchi yetu itakuwa nchi ya baraka” ameeleza.











  


Na Joel Maduka ; Geita

Kufuatia kuondoka kwa aliyekuwa mhasibu wa kanda ya ziwa wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA ,Upendo Furaha Peneza  na kurudi chama cha mapinduzi CCM , wanachama  481 wa vyama vya upinzani ambao walikuwa ni wafuasi wake wameamua kuungana naye pia na kujiunga na chama cha CCM.

Wanachama hao wamepokelewa na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Geita , Barnabas  Mapande kwenye viwanja vya Kata ya Kasamwa ambapo ndipo ulipofanyika Mkutano wa kuwapokea.

Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa CCM wilaya Barnabas Mapande amewataka wanachama hao kuwa na moyo wa uvumilivu na kuepukana na siasa za matusi ambazo zimekuwa aziwajengi watanzania.

“Ndugu zangu niwaambie ukweli kuwa Upendo Peneza anakuja na watu aliokuwa nao na mimi niwaambie ndugu zangu mchungaji mwema wa kondoo umfuata mchungaji wao sasa kwanini wengine wasimfuate Upendo Peneza”Barbabas Mapande Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Geita.

“Wale ndugu zetu wamekuwa na wasi wasi kuwa wataanikwa maovu yao nataka kuwaondoa shaka kuwa Peneza ajakulia kwenye familia ya matusi awezi kuwatukana wala kuwakashifu wao wawe na amani tu aliondoka amerudi Nyumbani sasa kwanini sisi tusimfanyie sherehe wao wawe wavumilivu tu Chama kipo kazini”Barnabas Mapande Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya geita

Naye Upendo Peneza ambaye alijiunga na CCM Tar 22 January 2024 ,amesema kuwa yeye hayupo tayari kushiriki siasa za kuwadanganya watu na kwamba amekuwa siku zote akisimamia ukweli na kuachana na uongo.

“Niliona kundi nililokuwepo siliwezi na sikuwa tayari kuwaragai watanzania na kuonekana natumika kwenye kundi ambalo linasiasa zisizo za ukweli mimi ni mwanachama wa ccm nimechagua kundi hili sababu limekuwa likisimamia ukweli na mimi nitasema ukweli siku zote wala sitakaa kimya kwa hofu ya  kumuogopa mtu yoyote”Upendo Peneza Mwanachama wa CCM.

“Ninajua wengi watasema maneno mengi mimi kuhamia ccm nataka niwaambie mimi sikuongwa na mtu kuingia CCM ukweli wa dhati mimi ndio niliwatafuta viongozi wa Chama cha Mapinduzi na kuwaomba wanikaribishe CCM sasa mtu umeomba kweli utakuwa tena umeongwa tuachaneni na maneno ya uragai ambayo yanasemwa”Upendo Peneza Mwanachama wa CCM.

Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Chacha Wambura ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi kuwa tayari katika uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa kukichagua chama cha mapinduzi CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa,vijiji na vitongoji.