Na Joel Maduka,Geita..

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM ,Mkoa wa Geita,Nicholaus Kasendamila amefunga rasimi mafunzo ya itikadi kwa vijana wa CCM ,huku akisisitiza  suala zima la vijana  kuzingatia usalama wao wenyewe na usalama wa Nchi.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita ametoa Wito huo wakati akizungumza na zaidi ya vijana mia sita ambao walikuwa kwenye mafunzo ya itikadi ambayo yamefanyika Kata ya Nyakagomba Wilayani Geita.

Amesema wao kama vijana wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kujilinda na vitendo viovu ambavyo vinaweza kuhatarisha maisha yao ya sasa na baadae.

“Natambua vijana nyie bado Taifa linawaitaji na bado mnanguvu Kubwa kwa Taifa letu lakini niwaombe sana zingatieni suala la usalama wenu na wa Nchi vijana wengi wamepotea sababu ni kukosa nidhamu na kujikuta wakijiingiza kwenye makundi ambayo yameendelea kugharimu maisha yao ya kila siku”Amesema Nicolaus Kasendamila.

Naye Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Geita Manjale Magambo amesema uwepo wa makambi ya vijana yamekuwa na faida nyingi kwa vijana kutokana na kuwajengea uwezo wa kujitegemea na kujikwamua kiuchumi na kusaidia kukijua chama zaidi kutokana na mafunzo ya Historia ambayo yanatolewa.

 
Share To:

JOEL MADUKA

Post A Comment: