
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Mwigulu Nchemba amepongeza kiwanda darasa cha kubangua korosho kilichoanzishwa na kituo cha zana za kilimo na teknolojia vijijini (CAMARTEC) wilayani manyoni mkoani singida na kuitaka sekta binafsi kuchangamkia fursa ya kuanzisha viwanda vipya vya kubangua korosho ili kuwawezesha wakulima kupata bei nzuri na kuongeza fursa za ajira kwa vijana.
Akizungumza mara baada ya kutembelea Kiwanda Darasa cha Kubangua Korosho kilichoanzishwa na CAMARTEC ambapo amejionea shughuli za ubanguaji wa korosho.Dr.Mwigulu Nchemba amesema kiwanda hicho ni utekelezaji wa Ilani ya CCM pamoja na Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050 hivyo ameitaka sekta binafsi kuanzisha viwanda vya kubangua korosho.
Kaimu mkurugenzi Mkuu wa CAMARTEC Mhandisi Godifrey Mwinama amesema iwapo korosho zitabanguliwa nchini zaidi ya ajira 36000 zitazalishwa na pia ameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dr.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa kiwanda darasa hicho kwa ajili ya kuwasaidia wakulima wa korosho na wananchi kwa ujumla.
kwa upande wake mbunge wa jimbo la manyoni Dr.Pius Chaya ameitaka serikali kuanzidha kongani ya viwanda huku meneja wa bodi ya korosho tawi la manyoni wanaeleza hali ya uzalishaji ilivyo











Post A Comment: