Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu leo ameongoza watumishi, mawakili na wananchi kumuaga aliyekuwa mtumishi wa Ofisi hiyo, marehemu Wakili Msomi Charles Boaz Swai aliyefariki jana jijini Dodoma.
Tukio hilo la Ibada na kisha kutoa heshima za ilifanyika nyumbani kwa marehemu eneo Chaduru Mei 29, 2026 ambapo Waziri Sangu alieleza kuwa mchango wa Marehemu Wakili Swai utaendelea kukumbukwa na kwamba Ofisi yake inamshukuru Mungu kwa maisha ya Wakili Swai kutokana utumishi wake .
Akieleza kuhusu namna Marehemu Swai alivyotoa mchango wake, Waziri Sangu aliwaeleza waombolezaji kuwa ni wiki moja imepita alifanya kazi ofisini kwake na Wakili Swai ambapo walikubaliana kuendelea kukamilisha jambo hilo lakini ghafla Mwenyezi Mungu amemchukua na kuwataka watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kuendelea kuenzi mchango wa marehemu Wakili Swai.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Evaline Munisi aliyeambatana na Waziri aliwashukuru wananchi na watumishi wote wa serikali na sekta binafsi walishiriki kwenye Ibada hiyo ya kumuaga Wakili Charles Swai .
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania Dr. Addo Mwasongwe akitoa salamu zake alisema marehemu Swai alikuwa mwanachama mahili na aliyetumia taaluma yake kusaidia jamii ya kitanzania kupata haki zao mujibu wa Sheria.
Kwa upande wake Chapter Convern wa Mkoa wa Dodoma Wakili Msomi Mary Munissi akitoa salamu kwa niaba ya Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS) alieleza kuwa marehemu Wakili Swai kabla ya kuajiliwa serikalini alikuwa mwanachama wao ambapo alishiriki kukijenga chama hicho kusaidia upatikanaji haki kwa wananchi.
Marehemu Wakili Charles Swai alizaliwa mwaka 1989 mbapo katika utumishi wake alifanikiwa kuanzisha kampuni binasfi ya uwakili ya Competency International . Hadi umauti unamkuta alikuwa Afisa Sheria katika Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi,Ajira na Mahusiano ambapo ameacha mke na watoto watatu. Marehemu atazikwa kesho Kigamboni Dar es Salaam.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.






Post A Comment: