Articles by "9MKUTANO"
Showing posts with label 9MKUTANO. Show all posts

 


Kamishna wa Madini Nchini Dkt. Abdul Rahmani  Shaban Mwanga kwa mara ya kwanza tangu alipoteuliwa amefanya ziara ya kikazi Kituo cha Jemolojia Tanzania  (TGC) na kukutana na timu ya Menejimenti ya Kituo hicho huku akielezea madhumuni ya ziara hiyo ikiwa ni kujitambulisha.

Dkt.Mwanga amekipongeza kituo hicho kwa kuendelea kutoa mafunzo ya uongezeaji thamani madini nchini na kuhamasisha watanzania kuendelea kupeleka wanafunzi kujiunga na kituo hicho.

Sambamba na hilo Dkt. Mwanga ameagiza uongozi wa Kituo hicho kuongeza juhudi katika kukifanya Kituo hicho kuzidi kutambulika Kimataifa na kuvutia wateja na wadau wa sekta ya madini kutoka ndani na nje ya nchi.

Pia amekitaka Kituo cha Jemolojia Nchini (TGC) kuendelea kutoa huduma zinazoendana na soko la madini Duniani kama vile huduma za Kimaabara za utambuzi wa madini ya vito pamoja na bidhaa za usonara.

Kwa upande wake Mratibu wa Kituo cha Jemolojia Daniel Kidesheni
amesema kuwa, Kituo hicho kinatoa huduma mbalimbali za uongezaji thamani madini kwa wadau ikiwa ni pamoja na utambuzi wa madini ya vito, usanifu madini pamoja na uchongaji wa vinyago vya miamba.

 

 

 

Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Jiji la Arusha katika uwanja wa Shekhe Amri Abeid ambapo amewataka vijana kutambua kuwa anawahangaikia kwani wao Ni nguvu kazi ya Taifa.



Rais wa jamburi ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemuagiza mkuu wa wa mkoa wa Arusha John Mongela kwenda wilaya ya Ngorongoro kuangalia tofati zilizopo Kati ya wananch wanaoishi  ndani ya hifadhi  na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ili kuangalia namna ya kutatua

Mhe.Rais alisema kuwa  huko awali kulikuwa na migogoro mingi Sana, kwani vijiji vingi vimeingia kwenye hifadhi ,lakini wakaangalia migogoro hiyo kwa undani zaidi ya vijiji 100 wameamua kuviacha vilipo, kwani wakivihamisha hakuna pa kuvipeleka

Aidha alimshukuru Leigwanani Kisongo kwa kumwambia kwamba Serikali ikikaa pamoja na wafugaji wanaoishi ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, mgogoro huo utatatulika,hivyo Rais wameahidi kumtuma mkuu wa mkoa kutafuta Suluhu.

"Vijiji zaidi ya Mia moja tumeviacha vibakie vilipo ,tukiviahamisha hatuna pa kuvipeleka,Ila nakushukuru Sana Leigwanani Kisongo kwamba umetuambia tukikaa na sisi mgogoro utatatuta,nataka nikuahidi namleta mkuu wa mkoa aje kukaa na ninyi yakimshinda nitaingia mwenyewe" Alisema Rais.

Wakati huohuo Mhe.Rais amempa miezi 3 Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya karatu Rajabu Karia Magara kuhakikisha anakamilisha  ujenzi wa hospital hiyo ili kumaliza tatizo la wqgonjwa kukosa huduma ya matubabu 

  Karatu Kuna hospitali ya wilaya ambayo imeanzwa kujengwa kuanzia mwaka 2019 fedha yote umetolewa ipo pale iqna hospitali haijaisha, nakupa miezi mitatu kwasababu fedha yote unayo sioni kwanini hospital haijaisha Ina mwaka wa pili Sasa haijaisha"Alisema Mhe.Samia

Amemtaka kuhakikisha kuwa  hospitali hiyo inamalizika kwa muda alioutoa ili akienda  Karatu nikute imemalizika nije niifungie na wannachi wapate huduma 
 tukiviahamisha hatuna mahali pa kuvipeleka

Akizungumza juu ya ujenzi wa Stendi Jiji la Arusha Mhe.Rais Alisema kuwa hlmshauri Jiji ipeleke mchoro kwani Serikali inamradi wanaandaa wa kuomba fedha hivyo zikipatikana watazileta kwaajili ya ujenzi wa Stendi hiyo

Kuhusu suala la machinga. Alisema kuwa hawawezi kuruhusu sir za mjini kuharibiwa Ila utatafutwa utaratibu Maalum ili kuhakikisha wanpatiwa maeneo ya kufanya biashara zao

Kuhusiana na masuala ya mikopo kwaajili ya kuinua uchumi alisema kuwa mikopo yenye masharti nafuu kwaajili ya manufaa ya Taifa ataiileta Ila mikopo kichefuchefu hatoweza kunichukua kwasababu inawasogeza watanzania inaleta Maendeleo hivyo hataogopa kuichukua

Nataka kuwaahidi watanzania nitaangalia mikopo yenye unafuu kwa nchi yetu, inayoleta faida kwa nchi yetu hiyo nitaichukua, mikopo chechefu sitaichukua lakini ile ambayo inaleta nafuu kwa nchi yetu, inatusogeza watanzania inaleta maendeleo hiyo sitaogopa nitaichukua,”- Rais Samia Suluhu Hassan.

 


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo(katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya wizara hiyo alipotembelea leo Mpaka wa Namanga unaotenganisha nchi ya Tanzania na Kenya ikiwa ni ziara ya kusisitiza umuhimu wa kuimarisha doria na misako ili kudhibiti wimbi la wahamiaji haramu wanaoingia na kukamatwa nchini.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi



Afisa Uhamiaji Mfawidhi wa Kituo cha Namanga,Mrakibu wa Uhamiaji, Prolimina Tairo akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Khamis Hamza Chilo, juu ya udhibiti wa uingiaji na utokaji nchini kwa wageni na wenyeji wakati wa ziara ya kuimarisha doria na misako ili kudhibiti wimbi la wahamiaji haramu wanaoingia na kukamatwa nchini.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi



Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo akizungumza na Afisa Uhamiaji Mfawidhi wa Kituo cha Namanga,Mrakibu wa Uhamiaji, Prolimina Tairo(kulia),Afisa Uhamiaji Mkoa wa Arusha,Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji,Hosea Kagimbo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Kamishna Msaidizi wa Polisi,Justine Masejo alipotembelea leo Mpaka wa Namanga unaotenganisha nchi ya Tanzania na Kenya ikiwa ni ziara ya kusisitiza umuhimu wa kuimarisha doria na misako ili kudhibiti wimbi la wahamiaji haramu wanaoingia na kukamatwa nchini.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi



Afisa Uhamiaji Mfawidhi wa Kituo cha Namanga,Mrakibu wa Uhamiaji, Prolimina Tairo akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Khamis Hamza Chilo, juu ya sehemu ya kupimia afya kwa wageni wanaoingia na kutoka nchini wakati wa ziara ya kuimarisha doria na misako ili kudhibiti wimbi la wahamiaji haramu wanaoingia na kukamatwa nchini.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi



Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo (wapili kushoto) akiongozana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya wizara yake wakati wa ziara ya kutembelea Mpaka wa Namanga unaotenganisha nchi ya Tanzania na Kenya ikiwa ni ziara ya kusisitiza umuhimu wa kuimarisha doria na misako ili kudhibiti wimbi la wahamiaji haramu wanaoingia na kukamatwa nchini.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi



Na Abubakari Akida, Arusha

Idara ya Uhamiaji imetakiwa kuongeza kasi,kulinda na kuwa na uadilifu katika ukusanyaji wa mapato yanayotokana na shughuli za kiuhamiaji ili kuweza kulisaidia Taifa katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Khamis Hamza Chilo wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli mbalimbali katika Kituo cha Namanga ikiwa ni kukagua maeneo yanayotumika kwa uingiaji na utokaji wa wageni na wenyeji lengo ikiwa kudhibiti wimbi la wahamiaji haramu wanaokamatwa mikoa mbalimbali nchini.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia anawategemea sana, kwanza katika ulinzi wa nchi, ulinzi wa raia na mali zao, ikifika sehemu tukasema Tanzania ina amani basi nyie askari wetu ndio mmefanya kazi hiyo,mnalinda mipaka yetu usiku na mchana, pili anawategemea katika ukusanyaji wa mapato, nawaomba mapato yote yanayotokana na shughuli za kiuhamiaji muyadhibiti ili yatumike katika kujenga Taifa hili,jiepusheni na rushwa,”alisema Naibu Waziri Chilo

Pia aliwataka askari hao kuongeza kasi ya misako na doria kwa usalama wa nchi yetu ili wananchi waweze kushiriki shughuli zao za kimaendeleo kwa amani na salama ikiwa ni adhma ya serikali kuona wananchi wanafanya shughuli zao kwa amani na usalama.

Akisoma taarifa mbele ya Naibu Waziri,Afisa Uhamiaji Mfawidhi wa Kituo cha Namanga,Mrakibu wa Uhamiaji, Prolimina Tairo amesema kumekuwepo kushuka kwa mapato kulikosababishwa na janga la Korona ambako idadi ya wageni wanaoingia nchini imeshuka.

“Kuanzia mwezi Januari mpaka Mei Idara ya Uhamiaji katika Kituo cha Namanga tumekusanya jumla ya Dola za Kimarekani 180,780 tofauti mwaka jana kipindi kama hiki tulikua tumekusanya Dola za Kimarekani 450,000 na kushuka huko kunasababishwa na janga la Korona ambalo linaathiri shughuli za uingaiji na utokaji kutokana na vizuizi vilivyowekwa kwa raia wa nchi mbalimbali wanaopitia katika mpaka huu wa Namanga” alisema Tairo

Jumla ya wahamiaji haramu 11 wamekamatwa katika Wilaya ya Longido wakati wa operesheni ya kukamata wahamiaji inayoendelea katika mikoa yote iliyopo mpakani mwa Tanzania nan chi Jirani.

 


Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia Mhandisi Kundo Andrea (mwenye suti nyuma) akipata maoni ya wananchi katika kata ya Ipitimbi  katika Jimbo la Peramiho wilayani Songea mkoani Ruvuma.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea akizungumza katika mnara uliyojengwa na Vodacom kwa Zabuni Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote(UCSAF.)
Mkuu wa Nyanda za Juu Kusini wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Asajile John akitoa mikakati waliojiwekea katika utoaji huduma za mawasiliano wakati wa Ziara ya Naibu Waziri Mhandisi Kundo Andrea.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea  akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Nyanda za Juu Kusini wa Mamlaka ya Mawasiliano  Tanzania (TCRA) Mhandisi Asajile John wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara mkoani Ruvuma.
Wananchi wa Kata ya Ipitimbi wakiwa katika mkutano wa Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea wakati alipofanya ziara ya  kujua changamoto ya mawasiliano katika katika kata hiyo.
Mkazi wa kijiji wa Ipitimbi Jimbo la Peramiho Silvanus Njovu akiuliza swali kwa Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea   alipofanya ziara katika Jimbo hilo.


*TCRA waelezea maendeleo makubwa ya huduma za Internet Ruvuma.

Na Chalila Kibuda,  Songea

 NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea amesema kuwa Jimbo la Peramiho lina fursa za kibiashara za mawasiliano na kutaka watoa huduma wa kampuni za simu kujenga minara.

Kundo aliysema wakati alipofanya ziara katika Jimbo hilo na kutembelea sehemu zenye changamoto za Mawasiliano katika kijiji vilivyo  Kata za Mpitimbi pamoja na Ndokosi 

Mhandisi Kundo amesema kuwa kufika katika Jimbo  hilo ni kutaka wananchi wafurahie huduma za mawasiliano ambazo katika kufikia asilimia 80 mwaka 2025.

Kundo amesema jimbo la Peramiho linahitaji minara ya 3G na 4G kwa mahitaji ya mawasiliano yamekua na kuhitaji matumizi ya data.

Amesema Rais Dkt.John Pombe Magufuli ameanzisha Wizara ikiwa ni kutaka kutatua matatizo ya mawasiliano.

Kundo amesema kuna miradi mingi ya mawasiliano inayoendelea ni pamoja na mfumo postal code ambapo huduma ya vifurushi zitakuwa kiganjani.

Nae Mkuu wa Nyanda za Juu Kusini wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Asajile John ameeleza namna huduma za mawasiliano ya internet zilivyozidi kuenea mkoani Ruvuma ambapo Wilaya ya Songea peke yake ina jumla ya minara 71 ya mawasiliano ya simu, ikiwepo ya 4G inayopatikana katika baadhi ya maeneo ikiwepo Peramiho, Mpitimbi na Litapwasi. 

Mhandisi John amesema huduma ya 4G katika kijiji cha Litapwasi ni ishara kuwa wananchi wa vijijini wanaendelea kuunganishwa kwenye mawasiliano ya data kuelekea kutimizwa lengo la zaidi wa watumiaji wa Internet asilimia 80 ifikapo mwaka 2025.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Ave Maria Semakafu akizindua Kamusi ya kwanza ya Lugha ya Alama ya kidijitali ya Tanzania na Mwongozo wa Utekelezaji wa Mtaala wa Elimu ya Sekondari kwa wanafunzi viziwi wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya viziwi  yaliyofanyika Mkoani Tabora.
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imezindua Kamusi ya kwanza ya lugha ya alama ya kidijitali yenye lengo la kupunguza changamoto ya mawasiliano katika ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi viziwi.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Ave Maria Semakafu akionesha kishkwambi chenye kamusi huku Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt. Magret Komba akionesha Mwongozo wa Utekelezaji wa Mtaala wa Elimu ya Sekondari kwa wanafunzi viziwi mara baada ya kuzinduliwa katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya viziwi yaliyofanyika Mkoani Tabora.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Ave Maria Semakafu, Kamisha wa Elimu Dkt. Lyabwene Mutahabwa, Makamu Mwenyekiti CHAVITA wakicheza  na washiriki  ambao ni viziwi  wakati wa  kikele cha maadhimisho ya wiki ya viziwi yaliyofanyika Mkoani Tabora.
Wanafunzi viziwi wa shule ya sekondari  Kazima iliyopo Tabora wakiimba kwaya mbele ya Mgeni rasmi Dkt. Ave Maria Semakafu (hayupo pichani)wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Viziwi yaliyofanyika mkoani Tabora

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imezindua Kamusi ya kwanza ya lugha ya alama ya kidijitali yenye lengo la kupunguza changamoto ya mawasiliano katika ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi viziwi. 

Akizindua kamusi hiyo Mkoani Tabora, katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya viziwi yenye kauli mbiu “Kuhakikisha upatikanaji wa haki za binadamu kwa Viziwi”, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Ave Maria Semakafu amesema serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa makundi yote yenye ulemavu kupata elimu na huduma nyingine za kijamii. 

Dkt Semakafu amesema pamoja na maboresho makubwa yaliyofanyika katika sekta ya elimu, kundi la viziwi lilikuwa limeachwa nyuma huku changamoto kubwa ikiwa ni mawasiliano na kutokuwepo kwa walimu wa kutosha hasa katika ngazi ya sekondari ndio maana imeandaa kamusi hiyo kuwe na lugha moja ya alama na kutoa mafunzo kwa walimu wanaofundisha katika shule zinazopokea watoto viziwi. 

“Serikali inatambua umuhimu wa kuwa na lugha moja ya alama kwa ajili ya kuwezesha mawasiliano ya watumiaji wa lugha hiyo, hivyo itaendelea kusimamia uendelezaji na usanifishaji wa lugha ya alama ili kuwezesha utoaji elimu, kurahisisha ujifunzaji na kuboresha mawasiliano katika jamii.,”alisema Naibu Katibu Mkuu huyo.

Nae Kamisha wa Elimu 
Dkt. Lyabwene Mtahabwa amesema kilele cha maadhimisho ya wiki ya viziwi duniani ndio mwanzo wa mafanikio katika mchakato wa ujifunzaji na ufundishaji nchini kwani ni siku ambayo kamusi ya lugha ya alama ya kwanza nchini tena ya kidijitali inazinduliwa pamoja na mwongozo wa utekelezaji wa mtaala wa elimu ya sekondari kwa wanafunzi viziwi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET)Dkt. Aneth Komba  anasema Taasisi anayoisimamia ndio walipewa jukumu la kuandaa Kamusi hiyo  na kwamba imeandaliwa kwa kufata taratibu zote ikishirikisha wadau wote na kwamba itatumiwa na wanafunzi viziwi kutoka Tanzania Bara na Visiwani. 

Mkurugenzi wa Kitengo cha Elimu Maalum kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Magret Matonya amesema uzinduzi wa Kamusi hiyo ni muendelezo wa jitihada za Serikali kuhakikisha wanafunzi wenye mahitaji maalum nchini wakiwemo viziwi wanapata elimu bora. Aidha ameongeza kuwa  Wizara imeanza ujenzi wa shule ya mfano ya viziwi  katika Halmashauri ya Masasi Mkoani Mtwara ikiwa ni jitihada za kuboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji wanafunzi viziwi ambapo ujenzi wake utagharimu bilioni 1.5.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Taifa (CHAVITA) Selina Mlemba amesema wanaishukuru Serikali kwa hatua hiyo na kwamba wanaamini miaka michache ijayo watapata wataalamu wengi katika maeneo mbalimbali wakiwemo madaktari kwa kuwa sasa wamepata kamusi itakayowawezesha kusoma bila changamoto.

Mtaalamu elekezi wa uandaaji wa Kamusi ya lugha ya alama kutoka Archbishop Mihayo University College (AMUCTA) Profesa Henry Muzale amasema uaandaji wa kamusi hiyo umezingatia changamto zote za viziwi na hii ni kutokana na utafiti uliofanyika katika shule zenye watoto viziwi ikiwemo Njombe viziwi ambao  ufaulu wao uliendelea kushuka.


Kilele cha maadhimisho ya wiki ya Viziwi duniani kitaifa yamefanyika mkaoni Tabora ikiwa ni hatua ya kuenzi historia ya chimbuko la elimu kwa viziwi kwani shule ya kwanza ya viziwi nchini Tanzania ilianzishwa katika mkoa huo.



 Daktari akionyesha stika atakayobandika kwenye hospitali anakotoka kuonyesha huduma za WCF zinapatikana kwenye hospitali husika, wakati wa kufungwa kwa mafunzo hayo
 Baadhi ya madaktari wakionyesha stika watakayobandikwa kwenye hospitali wanakotoka kuonyesha huduma za WCF zinapatikana kwenye hospitali hizo, wakati w akufungwa kwa mafunzo hayo
 Dkt. Nancy Shuma (kushoto) kwa niaba ya washiriki wenzake akikabidhiwa stika itakayobandikwa kwenye hospitali anayofanyia kazi kuonyesha huduma za WCF zinapatikana kwenye hospitali husika. Anayemkabidhi ni Mkuu w akitengo cha Mahusiano na Uhusiano wa umma WCF, Bi. Laura Kunenge.
 Dkt. Omar Chande (wapili kushoto), kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha akikabidhio vyeti kwa washiriki.
 Dkt. Peter S. Mabula akizungumza kwa niaba ya washiriki wenzake wakati wa kufunga mafunzo hayo.
Dkt. Omar Chande, akitoa hotuba ya kufunga mafunzo kwaniaba ya mganga mkuu wa mkoa wa Arush
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary
Dkt. Pascal M agesa, Afisa madai na tathmini WCF
Dkt. Ali Mtulia, Meneja anayeshughulikia madai na Tathmini WCF
Na
mwandishi wetu, Arusha-
MADAKTARI
waliokuwa wakishiriki mafunzo ya siku tano ya uelimishaji wa tathmini za
ulemavu utokanao na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi kutoka mikoa ya Kanda
ya Kaskazini, wamefurahishwa na elimu waliyoipata na kwamba itasaidia kutenda
haki kwa pande zote mbili, wanufaika na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).
Mafunzo
hayo yaliyoanza Juni 22, 2020 kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC)
jijini Arusha yaliandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ambapo zaidi
ya madaktari 100 kutoka mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga
walijifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Sheria iliyoanzisha Mfuko,
jinsi Mfanyakazi aliyeumia au kuugua kutokana na kazi anavyoweza kuwasilisha
madai, jinsi ya kufanya tathmini ya ulemavu uliotokana na ajali au ugonjwa
utokanao na kazi.
“Katika mafunzo haya
nipende kusema kwamba wakufunzi wamekuwa makini sana na wamefundisha kile
ambacho kilistahili na kila mmoja amekiri kuwa wakufunzi wamefanya kazi nzuri
na hata mazoezi ya vitendo kwa washiriki hakuna aliyepwaya.” Alisema Dkt. Peter
S. Mabula ambaye ni mwenyekiti wa washiriki.
Alisema
mafunzo hayo yamewaandaa kwenda kufanya kazi nzuri kuliko ile ambayo walikuwa
wakifanya hapo kabla.
“Mafunzo haya
yametuandaa kwenda kutenda haki kwa wagonjwa wetu na kwa Mfuko, wale wagonjwa
wanaokuja kwetu hatimaye wanakuja kupata fidia hivyo tumejifunza umakini wa
kufanya tathmini kwa umakini na ubora ili kutouibia mfuko au kumuibia
wateja  na hivyo sisi tunasimama katikati
ya wateja na mfuko ili tuweze kutenda haki.” Alisema Dkt. Mabula.
Akitoa
hotuba ya kufunga mafunzo hayo Dkt. Omar Chande kwa niaba ya mganga mkuu wa Mkoa
wa Arusha alipongeza hatua ya Mfuko kuongeza idadi ya wataalamu watakaoweza
kuwahudumia wagonjwa wanaohitaji kulipwa fidia.
“Fursa
hii ya utoaji mafunzo imekuja wakati muafaka na ni imani yangu kile
kilichofundishwa hapa ndicho kitakachokwenda kuondoa changamoto za watu ambao
hapo awali walipata shida inapofikia wakati wa kudai fidia.” Alisema Dkt.
Chande.
Naye
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi
(WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary alisema mwaka 2015 Mfuko kupitia usaidizi wa
Shirika la Kazi Duniani uliweza kutoa mafunzo kama haya kwa madaktari 346 na
hadi kufikia Ijumaa Juni 26, 2020 madaktari wanaokaribia 1,000 tayari
wamepatiwa mafunzo.

Na Woinde Shizza, Arusha 

Wanachama Wa chama cha mapinduzi  nchini wametakiwa kuondoa tofauti zao na kivunja makundi haswa katika kipindi hichi wanapoelekea katika uchaguzi Mkuu ili kukiwezesha chama hicho kupita kwa kishindo.

Hayo yamebainishwa na mjumbe Wa kamati kuu CCM  Taifa ambaye pia ni Mwenyekiti Wa jumuiya ya wazazi  Edmund  mundolwa alipokuwa akiongea na viongozi Wa chama hicho mkoani Arusha Jana (Leo)kabla ya kuanza ziara ya siku tano ya kutembelea miradi mbalimbali  inayotekelezwa na chama hicho kupitia ilani

Alisema alisema kuwa katika kuelekea katika uchaguzi Mkuu Wa mwaka huu ni vyema wanachama na viongozi Wa Ccm kuacha makundi ya vyama Mara moja na iwapo kama kunaambao wamegombana ni vyema wapatane na waungane katika kukiletea chama cha mapinduzi ushindi katika uchaguzi ujao Wa Rais ,wabunge na madiwani.

"Mwaka huu tutajitaidi kuleta majina matatu maana majina matatu ni rahisi  kuvunja kuliko kuwa na makundi mengi ambayo ayana maana na ambayo yatatuletea makundi ,makundi matatu ni rahisi sana kuziniti kuliko kuwa na mandi mengi yatakayo tuchanganya" alibainisha mundolwa. 

Alisema kuwa wanaitaji viongozi Wazuri ambao ,ambao rais atakapo ingia madarakani katika kipindi cha awamu ya pili ,aweze kupata kupata viongozi Waziri Wa kuongeza serikali ,Hulu akibainisha kuwa Rais anataka viongozi wabovu waenguliwe tangu chini wasisubiri mpaka wakakatwe katika ngazi za huu Bali wawashulikiw mapema.

Alisema kuwa mradi huu Wa ufugaji wa Nyuki utasaidia kuwatoa vijana kwenye vijiwe na utawapeleka kwenye uzalishaji ,pia watatengeneza  wazazi Hale ambao utatufikisha mahali pazuri.

Aidha pia alimpongeza Mkuu Wa mkoa Wa Arusha Mrisho gambo kwa namna anavyofanya Kazi ya kutekeleza ilani ya chama hicho ,ambapo alisema katika mradi mbalimbali aliyoitembelea  ikiwemo ya barabara baipass ,mradi mkubwa Wa maji unaojegwa ndani ya jiji la Arusha ambao utagaeimu kiasi cha shilingi bilioni 520 ,pamoja na mradi Wa Nyuki ambao umebuniwa na Mwenyekiti Wa wazazi mkoa Wa Arusha na unaotekelezwa katika wilaya zote za mkoa Wa Arusha ambapo jumla ya mizinga 700 imwkabidhiwa .


Kwa upande wake Mwenyekiti Wa Ccm mkoa Wa Arusha alisema kuwa baadhi ya wanaccm mkoa Wa Arusha bado wanamakundi lakini akiwa kama Mwenyekiti  makundi ayapendi ,na hayataki ,na hata hivyo kuna baadhi ya mambo ambayo hayajakaa sawa ila wameshaanza kuyashulikia .

Aliwaambia wananchi Wa mkoa Wa Arusha wasirilihusu Mbu akaingia  katika chama na kuwavuruga na wakimbaini hawatamfumbia macho Bali watamchukulia sheria .

Kwa upande wake Mwenyekiti Wa jumuiya ya wazazi mkoa Wa Arusha ambaye ndio ametoa mizinga hii ya Nyuki kwa jumuiya ya wazazi alisema kuwa hii ni moja ya ahadi yake aliyoiadi kipindi akigombea nafasi ya Mwenyekiti Wa wazazi mkoa Wa Arusha 

Alisema kuwa mizinga hii itagawiwa katika wilaya zote zilizopo mkoani Hapa na kila wilaya imepatiwa mizinga 100kwa ajili ya wilaya yake,alibainisha kuwa mizinga hii itasaidia kutoa ajira kwa wananchi .

Nae Mkuu Wa mkoa Wa Arusha Mrisho gambo Alisema kuwa ataendelea kushirikiana na chama ili kuahakikisha wananchi wanapata maendeleo ,na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.



Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeitisha kikao cha dharura cha Kamati Kuu leo Alhamisi Novemba 7, 2019 kutoa msimamo kuhusu mchakato wa uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Kuanzia Jumanne Novemba 4, 2019 Chadema kimekumbana na kilio cha wagombea wake wengi kuenguliwa katika mchakato wa uchaguzi  wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019.


 Katibu  Mkuu Wizara ya Maji,  Profesa Kitila Mkumbo (katikati) akizungumza na Mameneja wa RUWASA wa Wilaya, Waganga Wakuu wa Wilaya, Maofisa Afya, Maofisa Elimu (SWASH), Maofisa Ustawi wa Jamii, TAMISEMI na Maofisa Wakaguzi wa Ndani wakati akifunga warsha ya mafunzo ya uelewa wa pamoja katika utekelezaji wa .mradi wa maji utakaokwenda sambamba na malipo kulingana na matokeo ya kazi (PforR) mjini Singida leo. Kulia ni Kiongozi  wa Timu ya  mradi huo kutoka Benki ya Dunia  (Task Team Leader), Iain Menzies na kushoto ni Mratibu wa mradi huo, Mhandisi Mashaka Sitta. 
 Mratibu wa mradi huo, Mhandisi Mashaka Sitta, akizungumza katika ufungaji wa warsha hiyo.
 Kiongozi  wa Timu ya  mradi huo kutoka Benki ya Dunia ( Task Team Leader), Iain Menzies akizungumza mbele ya washiriki wa warsha hiyo.
 Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Agnela Nyoni akizungumza kwenye ufungaji wa warsha hiyo.
 Washiriki  wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu Prof. Kitila Mkumbo (hayupo pichani) wakati akifunga warsha hiyo.
Washiriki  wakiwa kwenye warsha hiyo.
Mamia ya washiriki wa Mkutano wa Mawaziri wa sekta ya Mazingira, Maliasili na Utalii kutoka nchi za SADC wamewasili katika Ukumbi wa Mikutano wa kimataifa Arusha (AICC) tayari kuanza mkutano huo ambao unatarajiwa kuhudhuriwa na Mawaziri wa sekta husika, wataalamu pamoja na wadau mbalimbali.

Mkutano ambao utafunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Tayari baadhi ya Mawaziri wameanza kuwasili akiwepo Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Hamis Kigwangalla, Naibu Waziri wa Wizara hiyo Constantine Kanyasu, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima, pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara zinazohusika na mkutano huo.





Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Mkutano wa Sita Jukwaa la Uongozi la Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam, Tanzania. Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam. Rais John Magufuli wa Tanzania amesema masalia ya fikra za kikoloni walizonazo Waafrika wengi ni miongoni mwa sababu zinazofanya Bara la Afrika kushindwa kusimamia rasilimali zake ili kuleta mabadiliko ya kijamii na kiuchumi. Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa akihutubia kongamano la viongozi la 2019 akisema dhana ya uhuru haiwezi kutenganishwa na kujitegemea. “Kama hujitegemei huwezi kuwa huru, kwani uhuru wako utakuwa mikononi mwa unayemtegemea.” “Maana hasa ya kupigania uhuru ni kurejesha rasilimali zetu na hasa rasilimali zetu, lakini pia kuwa na uamuzi kamili wa namna ya kuzisimamia na kuzitumia wa kuzitumia ili kuleta ukombozi wa kiuchumi,” amesema Rais Magufuli. Amesema kutokana na kutoelewa dhana kamili ya uhuru, nchi za Afrika zinadhani watawala wa zamani ndiyo wenye uwezo wa kusimamia na kusaidia na kuendeleza rasilimali. Ametaja pia sababu ya kushindwa kusimamia rasilimali na kuleta mageuzi ya kiuchumi, akisema fedha siyo msingi wa rasilimali. “Fedha ni matokeo ya mwisho kabisa ya matumizi ya rasilimali zetu na siyo msingi wa maendeleo. Hata hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alisema ili tuendelee tunahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora. Hakutaja pesa, alijua itakuja tu kama yale tutayatimiza,” amesema. Ametaja pia ukosefu wa ubunifu na teknolojia ya viwanda akisema Afrika haitaweza kusimamia na kutumia rasilimali zake kiuendelevu bila kuwa na viwanda. Mbali na viwanda, ametaja kukithiri kwa migogoro na hali tete ya siasa barani Afrika akisema inasababishwa na mabeberu wanaotaka kuendelea kutumia maliasili za Afrika kwa manufaa yao. “Wakati sisi tunapigana wao wanakula na kamwe hawatataka tuwe na amani, kwani migogoro ndiyo mtaji wao,” amesema. Ameendelea kutaja pia tatizo la mikataba na makubaliano yanayoingiwa na wawekezaji katika kutumia rasilimali akisema, “Na hapa nchi yetu imeliwa sana kutokana na mikataba mibovu na hasa kwenye madini.” Kuhusu uharibifu wa mazingira, Rais Magufuli amesema unasababishwa na ukataji hovyo wa msitu kwa ajili ya nishati ya majumbani kutokana na gharama kubwa za umeme na gesi asilia. “Chanzo kingine ni uchafuzi wa mazingira unaofanywa na mataifa mengine yaliyoendelea na yenye viwanda vingi, lakini Afrika ndiyo inayoathirika zaidi a machafuko hayo,” amesema. Akizungumzia hatua zilizochukuliwa na Serikali, Rais Magufuli amesema imetungwa sheria ya kulinda utajiri na rasilimali na maliasili ya 2017 na kupitiwa upya na kurekebisha mikataba ya uchimbaji na madini isiyo na manufaa kwa Taifa. “Tumeweka msukumo mkubwa kwenye ujenzi wa viwanda na ukuzaji wa teknolojia ya viwanda ili mazao yanayotokana na rasilimali zetu yasindikwe kwanza kabla ya kuuzwa nje,” amesema Alitaja pia uanzishwaji wa mradi wa bwawa la Nyerere utakaozalisha MW 2115 kwenye bonde la mto Rufiji kama njia ya kutunza mazingira, kudhibiti nidhamu za watumishi wa umma na kupamba na rushwa na ufisadi. Wageni maarufu waliohudhuria mkutano huo walikuwa marais wastaafu kutoka baadhi ya nchi za Afrika akiwemo Thabo Mbeki wa Afrika Kusini, Olusegun Obasanjo wa Nigeria, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete wa Tanzania.