Articles by "Ikulu uteuzi"
Showing posts with label Ikulu uteuzi. Show all posts

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA),CPA Anthony Kasore,alipotembelea banda la VETA katika Maonesho ya uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo kwa mwaka 2014, toleo la 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Na.Alex Sonnna-DODOMA
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA),CPA Anthony Kasore, amesema kuwa asilimia 80 ya mafunzo yatolewayo na VETA ni ya ujuzi na kwa maana hiyo ni mojawapo ya utekelezaji wa sera mpya ya Elimu ya mwaka 2024 toleo la mwaka 2023.
CPA Kasore ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la VETA katika Maonesho ya uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo kwa mwaka 2014, toleo la 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma amesema kuwa sera hiyo ambayo inalenga kufungua uchumi wa kijana wa kitanzania tayari imeisha anza kutekelezwa na VETA kwa kutoa elimu ya ujuzi kwa asilimia 80.
Aidha ameeleza kuwa katika kuhakikisha sera hiyo inafanya kazi kwa kiwango cha juu kwa sasa nchi ina vyuo 65 ambavyo vipo kwa ngazi ya wilaya huku VETA ikiwa na vyuo 80 kwa sasa .
Haya hivyo CPA Kasore amesema kuwa katika kuhakikisha elimu ya ujuzi inatolewa VETA inazingatia utoaji wa elimu ya ujuzi ambayo itakuwa na viwango vya kupata kazi kwa ngazi ya ukanda,kitaifa na kimataifa.
" VETA haikuwaacha watu wenye makundi mbalimbali kwani sera inalenga kuyafikia makumdi yote kwa lengo la kumpatia ujuzi mtu mmoja mmoja ,jamii na makundi yote kwa lengo la makundi hayo kupata ufanisi wa kujiongezea kipato kwa mtu mmoja mmoja au taifa kwa ujumla wake."amesema CPA Kasore
Pia ameelezea umuhimu wa sera mpya ya elimu na mitaala iliyoboreshwa amesema kuwa itasaidia vijana wa kitanzania kuingia katika soko la ajira na kwa kutumia teknologia kwa haraka tofauti na ilivyokuwa sasa .
" Sera hiyo ambayo Rais Samia ameizindua ni chachu ya maendeleo kwa taifa la Tanzania pamoja na mtu mmoja mmoja kwani kila atakayekuwa amemaliza elimu ya lazima atakuwa na ujuzi wa kumfanya aingie katika soko la ajira au kujiajiri mwenyewe."amesema
Katika kutoa ufafanuzi wa umuhimu wa kuwepo kwa sera hiyo amesema kuwa VETA itahakikisha kunakuwepo vyuo vya kutosha nchini ambavyo wananchi watapata fursa mbalimbali ya ufundi stadi na ujuzi kwa kusoma na kwa vitendo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA),CPA Anthony Kasore,alipotembelea banda la VETA katika Maonesho ya uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo kwa mwaka 2014, toleo la 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma leo tarehe 16 Januari, 2025.




 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa Hundi kama Gawio na Michango kutoka kwa Mashirika mbalimbali na Taasisi za Umma kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa Hundi kama Gawio na Michango kutoka kwa Mashirika mbalimbali na Taasisi za Umma kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Juni, 2024.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Viongozi wa Serikali, Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma pamoja na wageni mbalimbali mara baada ya kupokea Gawio na Michango kutoka kwa Mashirika na Taasisi hizo, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Juni, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye hafla ya kupokea Gawio na Michango kutoka kwa Mashirika na Taasisi za Umma, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Juni, 2024.
Viongozi wa Serikali, Wakuu wa Mashirika na Taasisi za umma pamoja na Wageni mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya kupokea Gawio na Michango kutoka kwa Mashirika na Taasisi za Umma

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili Kigongo, Wilayani Misungwi kwa ajili ya kukagua Daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi km 3) ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 75, Mkoani Mwanza tarehe 14 Juni, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS ) Eng. Pascal Ambrose wakati akikagua Daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi km 3) ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 75. Mhe. Rais Samia amekagua Daraja hilo ambalo Ujenzi wake unatarajiwa kukamilika Februari, 2024.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza mmoja wa Wataalamu wa Ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi km 3) Eng. Abdulkarim Majuto wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wake Mkoani Mwanza Februari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoka kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi km 3) ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 75. Mhe. Rais Samia amekagua Daraja hilo ambalo Ujenzi wake unatarajiwa kukamilika Februari, 2024.

 Viongozi mbalimbali wa Serikali wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati alipokuwa akiwasalimia Wananchi wa Sengerema na Buchosa Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza tarehe 14 Juni, 2023.

Wananchi wa Sengerema na Buchosa wakishangilia mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwasili Sengerema mkoani Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Kigongo Ferry Wilayani Misungwi mara baada ya kukagua Daraja la JP Magufuli Mkoani Mwanza  Tarehe 14 Juni, 2023.

Muonekano wa Daraja la Daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi km 3) linalounganisha Wilaya za Misungwi na Sengerema Mkoani Mwanza ambalo Ujenzi wake umefikia  asilimia 75 na unatarajiwa kukamilika mwezi Februari, 2024. 




Na Denis Chambi, Tanga. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mh. Dkt.Pillipo Mpango amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama mkoani wa Tanga kutokuwa sehemu ya washiriki wanaotekeleza vitendo mbalimbali vya kiuhalifu na uhujumu uchumi ambapo ameeleza kuwa kumekuwa na taarifa za baadhi ya watumishi wa vyombo hivyo wanaotajwa kushiriki kwa maslahi yao binafsi.

 Dkt. Mpango ametoa rai hiyo leo November 20 katika bandari ya Tanga wakati kipokea maelezo kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Tanga Omari Mgumba kufwatia tukio la ghala la kuhifadhia bidhaa za magendo lililoungua moto hivi karibuni ambapo ameeleza kuwa kumekuwa na ushirikiano mdogo wa kupatikana taarifa za kiuchunguzi kutoka kwa mamlaka husika ikiwemo mamlaka ya mawasiliano Tanzania 'TCRA'. 

Aidha Dkt. Mpango amemuagiza kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Tanga ACP Hendry Mwaibambe kuwakamata na kuwaweka ndani watumishi wawili mmoja TRA David Kisaka pamoja na Sophia Mwezimpya mkuu wa ghala hilo ambapo mara baada ya kutokea kwa tukio walishindwa kutoa ushirikiano.

 "Wakuu wetu wa vyombo vya ulinzi na usalama vyote katika mkoa huu wa Tanga kuna vitendo vya kihalifu ikiwemo magendo , biashara ya madawa ya kulevya , uvuvi haramu umeshamiri hapa, wahamiaji haramu na biashara ya binadamu na nyingime halafu vyombo mpo hapa hapa kunakuwa na dalili kwamba na nyinyi baadhi yenu ni washiriki haya yanaangamiza taifa letu" 

"Taifa hili linawategemea , natoa onyo kali asitokee mmoja wa watumishi wa vyombo , kama baadhi yenu wanafanya mambo ya hovyo semeni tutawaondoa na kuwachukulia hatua za kisheria msijihusishe kabisa na vitendo hivi vya kihalifu mkijihusisha nyinyi hamtutasaidia kuwakamata hawa wengine kwahiyo mtusaidie kuwatambua hawa amabao wanachafua majeshi yetu ili tuwatoe" 

"Mkuu wa Polisi wachukue hawa watusaidie katika uchunguzi tusiwaache wanadhurura huko mtaani, sisi tumepoteza mali huwezi kuchezea mali ya Tanzania hivi lakini pia fuatilia nyendo zao katika utendaji , na hizo taarifa za TCRA zije kwa mkuu wa mkoa na kwenye vyombo vya ulinzi na usalama mara moja " alisema Dkt. Mpango 

Aidha ameitaka mamalaka ya mapato Tanzania 'TRA' mkoa wa Tanga kuendelea kudhibiti mianya yote inayoikosesha serikali mapato huku akimtaka kamishna mkuu wa TRA nchini kuuangalia kwa ukatibu mkoa wa Tanga kutokana na kukithiri kwa ufujaji wa mapato. 

Awali akieleza juu ha tukio la kuugua moto ghala lililopo kayika eneo la Bandari ambalo pia ni mali ya TRA lililokuwa limehifadhia bidhaa zilizokamatwa kwa magendo pamoja na zile zilizoshindwa kulipiwa kodi mkuu wa mkoa Omari Mgumba alisema mara baada ya kutokea kwa tukio hilo waliunda kamati maalumu kwaajili ya kufanya uchunguzi wakina ambapo bado wanaendelea nao. 

"Tuliunda kamati kwaajili ya kufanya uchunguzi wa tukio hilo na walipokuja kwa mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi wa Gati katika eneo la Bandari hawakuweza kutoa ushirikiano na hata camera za siku ya tukio walisema zimefutika" alisema Mgumba.

 Aidha Makamu wa akiwa kwenye ziara yake ya siku mbili mkoani Tanga amefungua kiwanda cha kuzalisha vifungashio cha Yogi polypack sambamba na kuzindua rasmi  mashindano ya michezo mashirika taasisi binafsi na Makampuni 'Shimuta" yanayoendelea kwa michezo mbalimbali mkoani Tanga ambapo yanatarajia kufungwa november 29. 
.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshuhudia utiaji saini wa Mikataba na Hati za Makubaliano ya kimkakati 15 akiwa pamoja na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Xi Jinping.

Miongoni mwa mikataba hiyo iliyolenga kuimarisha ushirikiano, biashara na uwekezaji wa baina ya nchi hizo mbili umeshuhudia China ikiipunguzia Tanzania sehemu ya deni lake la thamani ya Shilingi Bilioni 31.4.

Miongoni mwa mikataba na makubaliano yaliotiwa saini ni kuhusu mahitaji ya kuwepo na soko kubwa la usafirishaji wa maparachichi kutoka Tanzania kwenda China.

Pia wametia saini Mkataba unaohusu msaada wa RMB milioni 100 za ushirikiano wa kiuchumi na kitaalamu baina ya nchi hizo mbili.

Vile vile, kumetiwa saini makubaliano kuhusu mahitaji ya kuwepo na soko kubwa la Usafirishaji wa Mabondo ya Samaki pamoja na bidhaa nyingine za uvuvi kutoka Tanzania kwenda China.

Aidha, China imetoa mkopo wa thamani ya dola za Kimarekani milioni 56.72 wenye masharti nafuu kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa uwanja wa ndege wa Zanzibar, Terminal II.

China inaongoza kwa uwekezaji nchini Tanzania. Hadi kufikia Mwezi Oktoba 2022, Jumla ya miradi 1,098 yenye thamani ya Dola za Kimarekani Bilioni 9.6 ilisajiliwa katika kituo cha uwekezaji cha TIC.

Miradi hiyo imezalisha ajira 131,718. Uwekezaji huo umefanyika katika sekta za viwanda, kilimo, mawasiliano, madini na uvuvi.

Rais Samia yupo nchini China kwa ziara ya Kiserikali kufuatia mwaliko kutoka kwa Rais wa nchi hiyo ambapo pia alikutana na kuzungumza na Waziri Mkuu wa China pamoja na Spika wa Bunge la nchi hiyo.

Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

 


Rais Samia Suluhu Hassan amewaagiza mawaziri ambao amekuwa akiwateua kutekeleza majukumu yao huku wakizingatia mambo makubwa matatu.

Mambo hayo ni kuheshimu katiba ya nchi, kufahamu mipaka yao na kuwa na siri.

Rais Samia ameyasema hayo Ikulu mkoani Dar es Salaam, wakati wa hafla ya kuwaapisha mawaziri watatu kufuatia mabadiliko madogo aliyoyayafanya katika Baraza la Mawaziri hapo jana.

Amesema kwa Mawaziri ni muhimu kuheshimu katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kutoa maamuzi ya mambo mbalimbali, kwani bila kufanya hivyo watakua wanakiuka baadhi ya mambo.

Pia amesema lazima wajue mipaka yao iwe ni kwenda juu au chini, jambo linatalosaidia kutoa maamuzi ambayo wakati mwingine hawastahili kuyatoa.

Jambo lingine ambalo Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza ni Mawaziri kuwa na siri, hasa mambo yanayojadiliwa ndani ya serikali na kwenye Baraza la Mawaziri.

Mawaziri walioapishwa hii leo na Rais
Samia Suluhu Hassan ni Angellah Kairuki ambaye ameapishwa kuwa waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Wengine ni
Dkt. Stergomena Tax ambaye ameapishwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Innocent Bashungwa aliyeapishwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza wakati wa ziara ziara ya kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akitoa maelezo wakati wa ziara ziara ya kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma

Jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais lililopo Mtumba jijini Dodoma ambalo liko katika hatua za ujenzi leo Juni 22, 2022 ambalo limekaguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo.

  

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika ziara ya kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo Juni 22, 2022.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo Juni 22, 2022.

Akizungumza mara baada ya kukagua jengo hilo Dk. Jafo alionesha kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa jengo akimtaka mkandarasi Kampuni ya SUMA JKT kuongeza kasi ya ujenzi ili likamilike na hatimaye lianze kutumika.

Dkt. Jafo aliishukuru Kampuni ya SUMA JKT ambayo imepewa kazi ya kutekeleza mradi huo kwa hatua iliyopiga pamoja na kamati iliyoteuliwa kuusimamia ujenzi huo. 

“Pamoja na kuwa mradi huu tunatakiwa tuukamilishe Novemba tisa mwakani ya miaka miwili lakini ikiwezekana hata ukamilike haraka zaidi na, ijapokuwa mkataba unasema kazi inaisha mwaka mmoja lakini ikiwezekana by mwanzoni mwa mwakani iwe imekamilka,” alisema Jafo.

Hata hivyo waziri huo alitoa maelekezo kwa wakandarasi wote wanaojenga majengo ya Serikali katika maeneo mbalimbali kuweka mfumo kuvunia maji ya mvua ili kunusuru athari za mafuriko pamona kuwa na hifadhi ya maji.

Awali akiwasilisha taarifa ya mradi huo Karani wa Mradi wa Ujenzi Bi. Philomena Bango alisema kazi mbalimbali zinaendelea kutekelezwa kulingana na mpango kazi (master program) uliowekwa.

Bi. Philomena aliongeza kwa kusema kuwa hadi kufikia sasa mkandarasi ameshakamilisha kazi ya ujenzi wa mradi kwa asilimia 33 na kuwa wana matumaini ya utakamilika kwa wakati.

Hata hivyo, alisema kuwa mkandarasi huyo anakabiliwa na changamoto ya kupanda kwa gharama za vifaa vya ujenzi vikiwemo ndondo.

Ofisi ya Makamu wa Rais ilisaini mkataba wa sh. bilioni 18.8 na Kampuni ya SUMA JKT wa kuanza ujenzi huo Oktoba 13, 2021 na kukabidhi rasmi eneo la ujenzi kwa Mkandarasi baada ya kushinda zabuni ambapo ujenzi wake unasimamiwa na Msimamizi Elekezi Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).