Na Denis Chambi, Tanga. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mh. Dkt.Pillipo Mpango amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama mkoani wa Tanga kutokuwa sehemu ya washiriki wanaotekeleza vitendo mbalimbali vya kiuhalifu na uhujumu uchumi ambapo ameeleza kuwa kumekuwa na taarifa za baadhi ya watumishi wa vyombo hivyo wanaotajwa kushiriki kwa maslahi yao binafsi.

 Dkt. Mpango ametoa rai hiyo leo November 20 katika bandari ya Tanga wakati kipokea maelezo kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Tanga Omari Mgumba kufwatia tukio la ghala la kuhifadhia bidhaa za magendo lililoungua moto hivi karibuni ambapo ameeleza kuwa kumekuwa na ushirikiano mdogo wa kupatikana taarifa za kiuchunguzi kutoka kwa mamlaka husika ikiwemo mamlaka ya mawasiliano Tanzania 'TCRA'. 

Aidha Dkt. Mpango amemuagiza kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Tanga ACP Hendry Mwaibambe kuwakamata na kuwaweka ndani watumishi wawili mmoja TRA David Kisaka pamoja na Sophia Mwezimpya mkuu wa ghala hilo ambapo mara baada ya kutokea kwa tukio walishindwa kutoa ushirikiano.

 "Wakuu wetu wa vyombo vya ulinzi na usalama vyote katika mkoa huu wa Tanga kuna vitendo vya kihalifu ikiwemo magendo , biashara ya madawa ya kulevya , uvuvi haramu umeshamiri hapa, wahamiaji haramu na biashara ya binadamu na nyingime halafu vyombo mpo hapa hapa kunakuwa na dalili kwamba na nyinyi baadhi yenu ni washiriki haya yanaangamiza taifa letu" 

"Taifa hili linawategemea , natoa onyo kali asitokee mmoja wa watumishi wa vyombo , kama baadhi yenu wanafanya mambo ya hovyo semeni tutawaondoa na kuwachukulia hatua za kisheria msijihusishe kabisa na vitendo hivi vya kihalifu mkijihusisha nyinyi hamtutasaidia kuwakamata hawa wengine kwahiyo mtusaidie kuwatambua hawa amabao wanachafua majeshi yetu ili tuwatoe" 

"Mkuu wa Polisi wachukue hawa watusaidie katika uchunguzi tusiwaache wanadhurura huko mtaani, sisi tumepoteza mali huwezi kuchezea mali ya Tanzania hivi lakini pia fuatilia nyendo zao katika utendaji , na hizo taarifa za TCRA zije kwa mkuu wa mkoa na kwenye vyombo vya ulinzi na usalama mara moja " alisema Dkt. Mpango 

Aidha ameitaka mamalaka ya mapato Tanzania 'TRA' mkoa wa Tanga kuendelea kudhibiti mianya yote inayoikosesha serikali mapato huku akimtaka kamishna mkuu wa TRA nchini kuuangalia kwa ukatibu mkoa wa Tanga kutokana na kukithiri kwa ufujaji wa mapato. 

Awali akieleza juu ha tukio la kuugua moto ghala lililopo kayika eneo la Bandari ambalo pia ni mali ya TRA lililokuwa limehifadhia bidhaa zilizokamatwa kwa magendo pamoja na zile zilizoshindwa kulipiwa kodi mkuu wa mkoa Omari Mgumba alisema mara baada ya kutokea kwa tukio hilo waliunda kamati maalumu kwaajili ya kufanya uchunguzi wakina ambapo bado wanaendelea nao. 

"Tuliunda kamati kwaajili ya kufanya uchunguzi wa tukio hilo na walipokuja kwa mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi wa Gati katika eneo la Bandari hawakuweza kutoa ushirikiano na hata camera za siku ya tukio walisema zimefutika" alisema Mgumba.

 Aidha Makamu wa akiwa kwenye ziara yake ya siku mbili mkoani Tanga amefungua kiwanda cha kuzalisha vifungashio cha Yogi polypack sambamba na kuzindua rasmi  mashindano ya michezo mashirika taasisi binafsi na Makampuni 'Shimuta" yanayoendelea kwa michezo mbalimbali mkoani Tanga ambapo yanatarajia kufungwa november 29. 
.
Share To:

Post A Comment: