Mfuko
wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umeanza kupokea madai kwa
njia ya mtandao tangu Aprili Mosi, 2024, Meneja wa PSSSF, Kanda ya
Zanzibar, Amina Kassim.
Aidha, kufuatia mapinduzi hayo ya kidigitali katika
kutoa huduma, Bi. Amina amewataka waajiri kutumia mfumo huo ili kuwaondolea usumbufu
wastaafu watarajiwa.
"Dunia
ipo zama za teknolojia hivyo PSSSF nayo
haijaachwa nyuma, tumewarahisishia wanachama wetu kupata huduma mbalimbali
kupitia mtandao.” Amefafanua.
Akizungumza
na waandishi wa habari kwenye Maonesho ya miaka 60 ya Muungano yanayofanyika
katika viwanja vya Nyamanzi Wilaya ya Magharibi "A" Kisiwani Unguja,
Zanzibar, Amina ameeleza umuhimu wa
Maonesho hayo kwamba ni alama ya kudumisha Muungano wa pande mbili, Bara na
Visiwani.
“Kuna
kila sababu ya kuendeleza muungano wa Tanganyika na Zanzibar ili kudumisha
umoja na mshikamano ulioanzishwa na wasisi wetu. Kutokana na umuhimu huo ndio
mana tumeamua kushiriki maonesho haya
ili kutoa huduma kwa wanachama wetu na wananchi kwa ujumla.” Alifafanua.
Akizungumzia
huduma zitolewazo katika banda hilo, Amina alisema, pamoja na elimu ya hifadhi
ya jamii, pia wanawaelimisha wanachama wao namna ya kutumia huduma za PSSSF
Kiganjani.
“Huduma
hii inatoa fursa kwa mwanachama kupata huduma mbalimbali za Mfuko kupitia Simu
janja. Huduma hizo ni pamoja na kuangalia mwenedndo wa michango yake, mafao
yatolewayo na Mfuko lakini kwa wastaafi anaweza kuhakiki taarifa zake.”
Alifafanua.
Kaulimbiu
ya Maonesho hayo ni “Miaka 60 ya Muungano
tuna Shikamana, Tunaimarika kwa Maendeleo ya Taifa.”
“Sisi
kama Mfuko tunaamini ushiriki wewtu unaakisi moja kwa moja kauli mbiu hiyo.”
Alisema
Aidha
alisema PSSSF imekuwa ikiimarisha utoaji huduma kwa wanachama popote walipo.
“Mwanachama
wa PSSSF anaweza kufurahia mtandao wetu ambao ofisi zetu zimeenea nchi nzima
Bara na Visiwani.”
"Hivyo tunawakaribishwa wanachama wetu
kwenye ofisi zetu za Zanzibar kwa hakika huku ndiko kushikamana vizuri kwa
maendeleo ya taifa letu", alisema Amina.
Meneja wa Ofisi ya PSSSF Zanzibar, Bi. Amina Kassim akimuelekeza Mkuu wa Polisi Jamii Zanzibar, Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP. Jonas Mdyanko Mahanga, namna ya kujisajili kwenye App ya PSSSF Kiganjani. Anayeangalia ni Afisa TEHAMA, Bilal Mlendela.
Meneja wa Ofisi ya PSSSF Zanzibar, Bi. Amina Kassim akimuelekeza Mkuu wa Polisi Jamii Zanzibar, Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP. Jonas Mdyanko Mahanga, namna ya kujisajili kwenye App ya PSSSF Kiganjani. Anayeangalia ni Afisa TEHAMA, Bilal Mlendela.
Post A Comment: