Askofu mkuu wa Kanisa takatifu katoliki la ORTHODOX,  Dkt. George Odhiambo Jamba akimsimika Askofu mkuu mteule Francis Laurent Bukombe (Bludah) kuwa Askofu mkuu wa Kanisa la Orthodox nchini Tanzania.

Na Mapuli Kitina Misalaba

Askofu mkuu wa Kanisa takatifu katoliki la ORTHODOX,  Dkt. George Odhiambo Jamba amemsimika Askofu mkuu mteule Francis Laurent Bukombe (Bludah) kuwa Askofu mkuu wa Kanisa la Orthodox nchini Tanzania.

Askofu Bukombe amesimikwa jana Jumamosi Aprili 27,2024 kwenye ibada maalum iliyofanyika katika Kanisa la Orthodox Jimbo la Shinyanga lililopo kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga.

Ibada hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Dini, serikali vyama vya kisiasa, wadau pamoja na waamini ambapo mgeni rasmi ni naibu Waziri ofisi ya Waziri mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Mhe. Paschal Patrobas Katambi.

Akizungumza Askofu mkuu wa Kanisa takatifu katoliki la ORTHODOX,  Dkt. George Odhiambo Jamba amemkumbusha Askofu Bukombe kuendelea kutoa huduma hiyo kwa watu wote huku akimsisitiza kutokukata tama.

“Kila mtu amepewa talanta yake na mwenyezi Mungu kiongozi yoyote awe wa Dini au wa serikali huwa ni kionmgozi wa wote na wewe uendelee kuwa kiongozi wa wote utoe huduma sawa kwa kila mja kwa wakristo wote ujue ya kwanza wote si sawa utapata ambao wataitikia wito wako kuna wengine ambao hawataitikia hao wote ni wako, kuna wale ambao utawahudumia wako na hela na kuna wale ambao utawahudumia hawana kitu chochote hao wote ni watoto wako usije kuwakatia tama wala kukataa tama kutoa huduma ya Mungu lakini huduma yetu si ya utajili huduma hii niya kusaidia na kuponya watu wenye shida na matatizo kwahiyo usiogope bwana wetu Yesu kristo awe pamoja nawe”.amesema Askofu mkuu Dkt. Jamba

Akizungumza  baada ya kusimikwa kuwa Askofu wa kanisa la Orthodox nchini Tanzania, Askofu mkuu Dkt. Francis Laulent Bukombe ameahidi kuitumikia vema nafasi hiyo ambapo amesema ataendelea kushirikiana na serikali katika kupambana na vitendo vya ukatili unaoendelea kwa wanawake, wanaume na watoto huku akikemea na kupinga ndoa za jinsia moja.

“Pamoja na kutimiza utume huu kanisa litaendelea kusimama na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Mhe. Rais wetu Samia Suluhu Hassan moja wapo ya mambo ambayo kanisa hili litasimamia n ni pamoja na kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake, wanaume na watoto kwahiyo kanisa hili tutasimama na kutetea kwa nguvu zetu zote kuhakikisha tunapinga ukatili kwa watoto ubakaji na ulawiti lakini pia vipigo vya aina zote na kuhakikisha malezi bora katika familia yanaonekana lakini pia kanisa hili linapinga na litaendelea kupinga ndoa ya jinsia moja mapenzi ya watu wa jinsia moja katika kanisa hili hatutafungisha ndoa ya jinsia moja”.amesema Askofu mkuu Bukombe

Askofu Bukombe ametumia nafasi hiyo kuwashukuru viongozi mbalimbali, wadau na waumini waliohudhulia ibada hiyo ambapo ameeleza kwa ufupi historia katika safari yake ya utumishi pamoja na changamoto alizopitia katika maisha yake.

“Mwaka 2003 tulianza huduma kama kituo cha huduma ya maombi na maombezi huduma hii ilifanyika sehemu mbalimbali ambapo kwa mara ya kwanza ni nyumbani kwa Baba Deo Majengo mapya (Diwani Mhe. Shagihilu) na badae uwanja wa Sabasaba chini ya mti Ndala, kupitia huduma hii Mungu alinipa uwezo mkubwa wa kuwahudumia watu miujiza ya uponyaji ilifanyika tulirudisha vitu vya watu vilivyochukuliwa na vilivyoibiwa na mwovu mfano waliofukuzwa kazi, waliorudishwa kazini, waliokuwa na kesi Mahakamani wengi walifutiwa na wengine kushinda kesi”.

 “Muujiza mkubwa ambao utaendelea kukumbukwa ni watu wengi kwa utukufu wa Mungu ni ule uliofanyika uwanja wa Sabasaba Mwaka 2004 ambapo mtumishi wa Mungu niliweze kuita Mvua ikakata kunyesha pia niliweza kusimamisha Jua likatii katikati ya mkutano kwa jina la Mungu Baba kupitia Yesu kristo mwanaye”.

“Huduma hii haikuishia hapo tarehe 28,12,2012 huduma ya kinabii Elia Kizazi cha nne (4) ilishuka kwa maono makubwa na nguvu ya Mungu itendayo kazi ilionekana kwa Macho na watu kubarikiwa, kuponywa, kurejeshwa kwa upya na wengine kupokea huduma za kinabii na mpaka leo wanamtumikia Mungu wakiwa ni manabii kwa msaada wa Mungu tukajenga kituo cha maombi kwa kutumia Maturubai na kazi ya Mungu kuendelea ambapo tulipata waumini wengi waliopokea baraka za Mungu Baba hadi leo hii  ndani ya Mkoa wa Shinyanga nan je ya Mkoa wetu na hata mataifa ya nje hivyo huduma hii kujulikana kimataifa” amesema Askofu mkuu Dkt. Bukombe.

“Kwa msaada wa Mungu tulijenga kanisa dogo na tukaanza huduma ya Orthodox mpaka kufikia sasa tunakanisa hili ambalo leo tumefanyia ibada hii yote ni juhudi za wakristo, wadau wa kanisa walio nje ya kanisa letu (Marafiki)amesema Askofu mkuu Dkt. Bukombe.

“Mwaka 2015 Baba Askofu Gregoly wa Jerusaremu na Askofu mkuu wa Alexandra wa Misri walitumwa na Patriaka wa Jerusalemu na Patrika wa Alexandra wa Misri kuniomba kuingia na kuongoza kanisa la Orthodox ili kuliimarisha katika nchi za Afrika Mashariki hasa Tanzania”.

“Kutokana na kujua wito wangu katika huduma hii na mimi kwa msaada wa Mungu Baba nilizungumza naye sirini pa sirini pake na kunipa kibali na maelekezo ya kutumika katika utumishi huu kwa Mungu na utakatifu wake ndipo nililipoti na kukubali wito huu nilioiyiwa”.

“Tarehe 3,8,2019 nilipatiwa daraja la ushemasi nchini Uganda katika kanisa la Orthodox Kasese Bwelana Baba Askofu mkuu Rev. Dkt. Kiiza Thomas na daraja la upadre nilipewa tarehe 29,12,2019 na Baba Askofu mkuu Rev. Dkt. George Odhiambo Jamba kutoka Kenya hapa kanisa la Orthodox Ndala nchini Tanzania”.amesema Askofu mkuu Dkt. Bukombe

Askofu mkuu wa Kanisa takatifu katoliki la ORTHODOX,  Dkt. George Odhiambo Jamba akimsimika Askofu mkuu wa Kanisa la Orthodox nchini Tanzania Dkt. Francis Laurent Bukombe (Bludah) akizungumza katika ibada hiyo ambapo amewashukuru viongozi, wadau na waamini waliohudhuliwa.

Askofu mkuu wa Kanisa takatifu katoliki la ORTHODOX,  Dkt. George Odhiambo Jamba akimsimika Askofu mkuu wa Kanisa la Orthodox nchini Tanzania Dkt. Francis Laurent Bukombe (Bludah) akizungumza katika ibada hiyo ambapo amewashukuru viongozi, wadau na waamini waliohudhuliwa.

Ibada maalum ya kusimikwa uaskofu Baba Askofu mteule Francis Laurent Bukombe (Bludah) katika kanisa takatifu katoliki la Oxthodox Tanzania ikiendelea Ndala Manispaa ya Shinyanga.

Askofu mkuu wa Kanisa takatifu katoliki la ORTHODOX,  Dkt. George Odhiambo Jamba akimsimika Askofu mkuu mteule Francis Laurent Bukombe (Bludah) kuwa Askofu mkuu wa Kanisa la Orthodox nchini Tanzania.

Askofu mkuu wa Kanisa takatifu katoliki la ORTHODOX,  Dkt. George Odhiambo Jamba akizungumza katika ibada hiyo.

Askofu mkuu wa Kanisa takatifu katoliki la ORTHODOX,  Dkt. George Odhiambo Jamba akiwa katika zoezi la kumsimika Askofu mkuu mteule Francis Laurent Bukombe (Bludah) kuwa Askofu mkuu wa Kanisa la Orthodox nchini Tanzania.

Askofu mkuu wa Kanisa takatifu katoliki la ORTHODOX,  Dkt. George Odhiambo Jamba akiwa katika zoezi la kumsimika Askofu mkuu mteule Francis Laurent Bukombe (Bludah) kuwa Askofu mkuu wa Kanisa la Orthodox nchini Tanzania.



















 

Share To:

Misalaba

Post A Comment: