Na Denis Chambi Tanga.
MKOA wa Tanga kupitia ofisi ya tume ya Madini kwa mwaka wa fedha 2025/2026 umefanikiwa kukusanya kiasi cha Shilingi Bilioni 13.9 sawa na asilimia 126 na kufanikiwa kuvuka lengo walilopangiwa la kukusanya Bilion 12 mafanikio ambayo yamechangiwa na wachimbaji kufuata sheria zinazotakiwa ikiwemo kuwa na Leseni rasmi.
Hayo yameelezwa na Kaimu Afisa Madini Mkazi wa mkoa wa kimadini Tanga, Laurent Bujashi wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake akieleza mafanikio hayo ambapo amesema kuwa miongoni mwa Mikoa ambayo inapatikana Madini ya aina zote yaliyopo hapa nchini Tanga ni moja wapo karibia wilaya zote zikihusisha shughuli za uchimbaji wa aina mbalimbali.
"Tanga ni moja wapo ya Mikoa ambayo ni tajiri kwenye upande wa Madini kwa takwimu zilizopo kwenye kipindi cha mwaka wa fedha 2025/2026 tumeweza kukusanya jumla ya Shilingi Milion 13.9 ambayo ni sawa na asilimia126 ya lengo tulilopewa la kukusanya Bilioni 12, asilimia kubwa ya Madini yakiwa ni Madini ya viwandani yakifwatiwa na Madini mengine yakiwemo ya Vito na dhahabu".amesema Bujashi
Aidha amesema kuwa mafanikio hayo yametokana na uwepo wa leseni za uchimbaji wa aina mbalimbali za Madini ikiwemo Madini ya viwandani pamoja na dhahabu ambapo hadi sasa mkoa huo umesajili jumla ya leseni 3090, nyingi zikiwa ni leseni za uchimbaji mdogo na wa kati.
Hata hivyo Bujashi ameeleza kuwa yapo baadhi ya maeneo ambayo hayajatengwa kwaajili ya shughuli za uchimbaji wa Madini na baadhi ya wananchi wamekuwa wakikiuka taratibu kwa kuyavamia maeneo hayo ambapo sheria mbalimbali zimekuwa zikichukuliwa dhidi yao huku wengine wakionyesha utayari wa kutafuta leseni baada ya kupatiwa elimu.
"Zipo changamoto za baadhi watu kutumia maeneo ambayo wanavamia maeneo wanaanzisha shughuli za uchimbaji ambazo haziruhusiwi tunaendelea kushirikiana na Mamlaka za Serikali kiwachukulia hatua ikiwemo kufanya ukaguzi wa mara kwa mara lakini pia tumekuwa tukiwapa elimu wale ambao wameonyesha utayari wa kuomba leseni ili waweze kufanya shughuli zao kwa mujibu wa sheria" amesema. Bujashi
Ameongeza kuwa ofisi ya Madini mkoa wa Tanga imekuwa ikikutana na wamiliki wa leseni mara kwa mara ikiwemo kiwatembelea kwa lengo la kuhakikisha kuwa wananufaika namba moja wa shughuli wanazozifanya wanakuwa ni wananchi wa maeneo yanayowazunguka hii ikilenga hasa kuwapatia kipato kupitia.
"Tume ya Madini mkoa wa Tanga Huwa mara ya tunakaa na wamiliki wa leseni na kuwashauri kuhakikisha kwamba shughuli zao za uchimbaji zinazingatia wananchi kunufaika na wanakuwa kipaumbele cha kwanza na sehemu ya kile wanachokipata sheria inawataka kurudisha kwa jamii na wanatakiwa wawasirishe mipango yao ya utekelezaji wa CSR kwenye kamati za kila wilaya na kuweza kupitishwa"
Ameongeza kuwa kutokana na ukuwaji wa mkoa wa Tanga unaendelea kumekuwa na uhitaji mkubwa wa Madini ujenzi yakiwemo, vifusi, kokoto na mchanga hivyo baadhi ya wananchi kuanzisha shughuli za uchimbaji holela ambao unaweza kuathiri mazingira hivyo kuwataka kufuata sheria ikiwemo kuomba vibali.
"Kuendelea kukua kwa mkoa wa Tanga hii inaenda sambamba na uhitaji mkubwa wa Madini ya ujenzi wito kwa wananchi ni kuwataka kuomba leseni ambazo zitawawezesha kujipatia kipato zaidi lakini wahakikishe kuwa maeneo ambayo wanachimba ni Yale ambayo yamekubalika ili kuhakikisha kwamba hakuna uharibifu wa mazingira ambao unaweza kutokea na kupelekea athari kwa jamii"amesisitiza.
Baadhi ya Madini mbalimbali yanayopatikana Mkoani Tanga yakiwa katika ofisi hiyo.
Kaimu Afisa Madini mkoa wa Tanga Laurent Bujashi akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi wa kituo cha uongezaji thamani wa Madini mkoa wa Tanga Naomi Mndambi.

Muongez thamani wa Madini ya Vito Amour Juma akiwa katika shughuli zake ndani ya kituo kilichopo ndani ya ofisi ya Mkoa huo Kaimu Afisa Madini mkoa wa Tanga Laurent Bujashi akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi wa kituo cha uongezaji thamani wa Madini mkoa wa Tanga Naomi Mndambi.

Mfanyabiashara na Mnunuzi mkubwa wa Madini (DIRA)Mkoa wa Tanga Said Salimu.





Post A Comment: