Na Denis Chambi Tanga.

MBUNGE wa Jimbo la Tanga mjini Kassimu Mbaraka (Makbel) amesema kuwa ofisi yake inaratibu uandikishaji wa majina ya vijana kwaajili ya kuwapatia fursa ya ajira zaidi ya elfu 3,000 zilizopatikana kupitia zao la Mkonge  ambapo amewataka kuchangamkia fursa hiyo ili kuweza kujipatia kipato..

Makbel Amesema hayo wakati akiwa katika Kata ya Maweni jijini Tanga ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za mtaa kwa mtaa jimboni humo  zenye lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi wa Jimbo hilo ambapo ameeleza kuwa kupitia zao la Mkonge vibarua hao wanahitajika kwaajili ya kukata Mkonge mashambani pamoja na uchakataji wake kwa kutumia Korona.

"Mpaka sasa hivi  tuna ajira elfu tatu za vijana  ambao wanatakiwa kuja kuandikisha vijana kwenye ofisi ya Mbunge, vijana wanatakiwa waende  kufanya kazi ya kulisha Korona na kukata Mkonge na mshahara wanaolipwa ni kima kizuri cha  mshahara wa Serikali, mpaka sasa tunaendelea na zoezi la kuandikisha vijana  na ajira hizi ziko ndani ya jiji letu la Tanga" amesema Makbel.


Amebainisha kuwa alifanya ziara kwenye viwanda vyote vilivyopo jijini Tanga lengo hasa ni kujua ni kwa jinsi gani wananchi hususani wanaozungukwa na uwekezaji huo wananufaika ambapo aliwaelekeza wawekezaji kuzingatia wakazi waliopo karibu na maeneo yote ya viwanda hususani vijana ili viweze kuwa na tija kwao.

"Moja ya malengo ya kufanya ziara katika viwanda vyote vilivyopo jiji la Tanga ni kuhakikisha kuwa ajira zinapotokea ziletwe kwenye ofisi ya Mbunge  ili vijana waweze kunufaika kupitia Diwani wa kata husika tuweze kirstibu vizuri na kuwabaini walengwa"amesema Mbunge huyo.

Hayo yanakuja baada ya  wananchi waliiopata fursa ya kuzungumza mbele ya Mbunge huyo alipokuwa katika kata ya Maweni ambapo wameweza kutokunufaika na viwanda vilivyopo licha ya kuwa vimewazunguka katika maeneo yao ambapo wameomba kupatiwa vibarua ili waweze kujipatia kipato na hatimaye kuendesha familia zao.

"Sisi vijana tatizo kubwa lililopo kwa sasa ni ajira katika kata yetu ya Maweni kuna viwanda vingi vimetuzunguka lakini fursa kwa wakazi wa kata husika imekuwa ni changamoto na sisi tupo tayari kufanya hata vibarua lakini wanapata watu wa kutoka mbali" amesema mmoja wa kijana kwenye ziara hiyo..




Share To:

Post A Comment: