Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Paul Kijazi (Kulia), Akiwasalimia Wanachama wa Mfuko huo wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa wateja Ofisi za Makao Makuu ya PSSSF Dodoma, Oktoba 5, 2026

Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Paul Kijazi (Kulia), akimkabidhi cheti cha pongezi Afisa wa PSSSF, Bw. Dolphin Kaizer (katikati), kwa kutambua mchango wake katika kuhakikisha wanachama wanapata huduma bora. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa PSSSF, Bw. Hajji Khamis (kushoto). Cheti hicho amekabidhiwa leo Oktoba 5, 2026 wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja Ofisi za Makao Makuu ya PSSSF Dodoma.

Picha ya Pamoja ya Watumishi wa Mfuko wa PSSSF Makao Makuu Dodoma, wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja, Oktoba 5, 2026

Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa PSSSF, Bw. Hajji Khamis (kushoto) akimuhudumia mwanachama  wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa wateja Ofisi za Makao Makuu ya PSSSF Dodoma, Oktoba 5, 2026.

Afisa wa Huduma kwa Wateja Mwandamizi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Jimmy Kamasho, Kutoka Kanda ya Ziwa Magharibi mkoani Geita,  akimuhudumia mwanachama wakati wa Wiki ya Huduma kwa wateja iliyoanza leo oktoba 5, 2026.


Dodoma, Oktoba 5, 2026


Katika hali inayoashiria upendo, kuwajali na kutambua mchango wa waajiri mbalimbali, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umejumuika na baadhi ya Waajiri katika uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 na kuwaomba waendelee kuwa mabalozi wazuri wa PSSSF katika maeneo yao ya kazi.


Hayo yalisemwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu, Bw. Paul Kijazi alipokuwa akizindua Wiki ya Huduma kwa Wateja ambayo itaadhimishwa hadi Oktoba 9, 2026.


“Kwa namna ya kipekee napenda kutambua uwepo wa Waajiri mbalimbali na kuwashukuru kwa ushirikiano mkubwa mnaotupatia katika maeneo mbalimbali katika kuhakikisha wanachama wa PSSSF wanapata huduma bora na kwa wakati. Na sisi tunaahidi kuendeleza ushirikiano uliopo kwa maslahi makubwa ya wanachama wetu, asanteni sana kwa kutuunga mkono.” Alisema Bw. Kijazi


Bw. Kijazi alisema, kauli mbiu ya mwaka huu ya Wiki ya Huduma kwa Wateja ni Hatua Moja  Zaidi ( The Extra Mile), ambapo amewataka watumishi wa PSSSF kufanya  yasiyowezekana yawezekane na wajue kwamba kutoa huduma bora kwa wanachama ni wajibu wao wa kwanza, na aliongeza, “Hivyo, tuendelee kusikiliza zaidi wanachama wetu, tuwe wa kwanza kuwafikia wanachama wetu, tutoe elimu sahihi na kwa wakati na tuendelee kutekeleza majukumu yetu kwa uadilifu kama kawaida yetu”.


Akizugumzia utoaji huduma kwa wanachama, alisema kuna watumishi  wapo  katika madawati ya huduma, hao ni pamoja na wenzetu wa kituo cha huduma kwa wanachama, Call Center na Kitengo cha Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, ambao mara nyingi ndio wa kwanza kukutana na wanachama wetu, aliwapongeza  na kuwatia moyo waendelee kutoa huduma bora na aliwaomba watumishi wengine wawe tayari kuwasaidia pale wanapohitaji msaada wowote kwa lengo la kumhudumia vyema wanachama wa PSSSF.   


Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu, Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bw. Hajji Khamis alisema, “Tuwahudumie wanachama wetu kwa usawa, bila kujali nafasi zao, umri wao, eneo wanalotoka au aina ya huduma wanayohitaji. Siku zote tuzingatie muda wa huduma, usahihi wa taarifa,usiri wa taarifa za wateja na kufuata taratibu zetu tulizojiwekea ili tuweze kutoa huduma bora kwa wanachama wetu.

Mwisho

Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

OSCAR ASSENGA

Post A Comment: