NA DENIS CHAMBI, TANGA.

Waziri wa elimu sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda ameridhishwa na mafunzo kwa vitendo yanayotolewa na kituo cha Sayansi cha Stem Park kilichopo jijini Tanga akipongeza hatua waliyofikia  ambayo inakwenda kujenga na kuzalisha na kuwaandaa wabunifu na wataalam wa maswala mbalimbali hapa nchini.

Waziri Mkenda ametoa pongezi hizo wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kujionea shughuli zinazofanyika na kituo hicho kinachotoa mafunzo ya ubunifu kwa vitendo kwa wanafunzi wa elimu ya msingi na sekondari waliopo ndani ya halmashauri ya jiji la Tanga ambapo amesema kuwa 

"Tunajua kwamba project inspire wanacho kituo kama hiki mkoani Dar es salaam lakini tutashirikiana nao waanzishe kituo kikubwa mkoani Dodoma  na wabunge nitapenda wakija watembelee pale waone nini kinachoweza kufanyika  na tujenge vituo kama hivi nchi nzima tuanzie na Dodoma  najua haitafikia  wanafunzi wote lakini utaanza kuhamasisha na kwenye mitaala mipya tutanzia na kata"

"Huko tunakoenda  mwalimu anatakiwa kujaribu kuwafikirisha watoto wa kuweza kufanya uvumbuzi kutokana na ubunifu wao uwepo wa kituo hiki ni muhimu sana kwaajili ya kuchochea ubunifu kwa vijana  wetu kwa sababu vitu vyote wanavyotengenezea vinapatikana  katika mazingira  yetu" alisema Profesa Adolf.

Akizungumza mkurugenzi  wa kituo hicho  cha Sayansi teknolojia na Mahesabu (Stem Park) kilichopo chini ya project inspire Dkt. Lwidiko Mhamilawa alisema kuwa  malengo yao makubwa ni kutaka kuona nchi inakuwa na wanasayansi mbalimbali wanaozalishwa ndani ya vituo vyao  wakiendana na mabadiliko ya teknolojia ya sasa katika kujenga vijana kuweza kujiajiri mwenyewe kupitia uwezo wao binafsi.

"Kazi yetu kubwa ni kuhakikisha kwamba  tunawalea watoto kutokana na  udadisi wao wa kiasili  wa kisayansi mpaka kuwatengenezea wawe wana sayansi  halisi kwa kutumia  mbinu mbalimbali ikiwemo kujifunza kwa miradi na kuwaangalia mazingira ya kuhamasa kusoma  tangu wakiwa wadogo na kupewa fursa mbalimbali" 

"Nchi zote zilizoendelea  duniani kwa asilimia 60-70 karibia mapato ya ndani  yanayokana na taaluma ya uhandisi , Teknolojia na Mahesabu  na Tanzania ili tuweze kufika huko  tunahitaji wana taaluma wengi  na ndio maana tumekuwa tukifanya hivyo kwa miaka nane sasa" alisema Dkt Mhamilawa.

Aliongeza kuwa  tangu kituo hicho kilipoanzishwa  kwa miaka mitatu zaidi ya wanafunzi 30,000 wa elimu ya msingi na sokondari wamepata mafunzo  na matokeo yamekuwa ni chanya ikiwa ni pamoja na  walimu kupata uzoefu wa namna bora ya kufundisha masomo ya sayansi kwa njia tofauti tofauti.

" Kwa hapa Tanga tumechukua wanafunzi wa kutoka jiji zima  tangu mwaka 2021 mpaka leo  tuna wanafunzi karibu 30,000 wamekuja kutembelea kwenye kituo  na matokeo ni mazuri mpaka sasa ikiwemo walimu ambao wamekuwa wakija hapa kujifunza namna bora ya kufundisha masomo ya sayansi na mahesabu na wamekuwa wakitupa mrejesho  hii inaonyesha kwamba hiki kituo kimekuwa  ni msaada kwa walimu kwenye ufundishaji wao" aliongeza

Kwa upande wake  mkurugenzi mkuu wa tume ya Taifa ya sayansi na teknolojia "Costec" Dkt Amos Nungu amesema  uwepo wa kituo hicho ni njia bora na ya kipekee katika kuwahamasisha vijana kupenda na kujifunza masomo ya sayansi hivyo ili kupata wataalam mbalimbali wa baadaye wanaendelea kuhamasisha na hatimaye nchi nzima kuwepo na vituo vya kufundishia masomo ya sayansi kwa vitendo.

"Hii ni project inayohamsisha kujifunza masomo ya sayansi Teknolojia na Mahesabu kwa ufanisi zaidi kwa wanafunzi kujenga uelewa tunakaribia kuhamasisha kusudi nchi nzima tuweze kupata vituo kama hivi vya watoto kujifunza masomo ya sayansi na teknolojia kwa sababu  vinasaidia kujenga umahiri na upenzi wa sayansi kwa watoto wadogo" alisema Dkt Nungu.
 
Waziri wa elimu sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akiwapongeza wanafunzi wanaojifunza masomo ya sayansi kwa vitendo katika kituo cha Stem Park Tanga mara baada ya kufika kituoni hapo katika ziara yake mkoani humo.
 

 Waziri wa elimu sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akizungumza jambo katika kituo cha stem park kilichopo jijini Tanga (kulia) kwake ni mkurugenzi wa kituo hicho Dkt.Lwidiko Mhamilawa
Mkurugenzi  wa kituo cha Sayansi ,teknolojia na Mahesabu (Stem Park) kilichopo chini ya project inspire Dkt. Lwidiko Mhamilawa akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kutembelewa na waziri wa elimu sayansi na teknolojia Profesa Adolf Mkenda july 11,2023.
Baadhi ya wafanyakazi wa kituo cha sayansi , teknolojia na mahesabu ( Stem Park) kilichopo jijini Tanga wakiwa katika picha ya pamoja na waziri wa elimu sayansi na teknolojia Profesa Adolf Mkenda wakati alipotembelea kituoni hapo.Share To:

Post A Comment: