Floraidi ni madini ambayo yanapatikana kwa kawaida katika udongo, hewa, na maji. Viwango vya Floraidi ambavyo ni kawaida vinatokea katika maji si kawaida sana vya kutosha kuwa na athari kwa kuoza kwa jino. Kwa hivyo, baadhi inasema au manispaa za mitaa huongeza fluoride kwa maji, ili kusaidia kuzuia kuoza na kupunguza hatari ya mizigo.

Uhusiano kati ya Floraidi na tezi ni mgongano ambao umeendelea kwa miongo kadhaa. Wakati jumuiya ya meno na mamlaka ya maji ya manispaa huleta faida ya maji ya fluoridated katika kupambana na kuoza jino, wataalam wengine wana wasiwasi juu ya athari ya Floraidi inaweza kuwa na afya ya tezi na kazi ya tezi, na kudai kwamba kutosha kwa fluoride yatokanayo inaweza kupunguza kazi ya tezi, au kwa baadhi ya kesi kusababisha hypothyroidism.

Kufuatia mikakati ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kujikita zaidi katika kupambana na  kutatua changamoto sugu zinazowakabili wananchi wake, Serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji, imetatua na kumaliza kero ya muda mrefu ya kuondoa kiwango cha madini ya Floraidi yaliyozidi  kwenye maji ya kunywa yanayoyatumia na wananchi wa kijiji cha Lemanda kata ya Oldonyosambu, halmashauri ya Arusha mkoani Arusha.

James Mbajo ni mkazi wa Kijiji cha Lemanda ambapo ameishukuru serikali ya Rais Samia kwa mradi huo, mradi ambao licha kuondoa kero ya upatikanaji wa maji, amekiri kuwa maji hayo ni tiba kwao, kwa kuwa yataondoa changamoto ya matumizi ya maji yenye floraidi iliyozidi inayoathiri afya za wananchi wa maeneo hayo.

"Tunamshukuru mama Samia kwa kutukumbuka na kuletea mradi wa maji, kinamama tunateseka sana, tunatumia punda na pikipiki kuagiza maji kwa gharama kubwa, huku hakuna maji na maji  yaliyopo yana madini ya floraidi ambayo inamadhara kwa afya ya binadamu na wanyama, watu wanapinda miguu, watoto wanazaliwa na vichwa vikubwa, tunashukuru sana na kumpongeza Rais wetu" Amesema Mbajo

" Madhara yatokanayo na Floraidi sasa yamefikia mwisho kwa wakazi wenzetu wa Lemanda, tunategemea sasa tutatumia maji safi na salama yasiyo na Floraidi kama ilivyokua hapo awali" aliongezea

Naye Diwani wa kata ya Oldonyosambu Raymond Lairumbe, ameipongeza serikali ya inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusikia kilio cha wananchi wa Lemanda,  ambao kimsingi wengi wao wamepata madhara makubwa sana kutokana na kutumia maji yenye kiwango kikubwa cha madini ya Floraidi huku watoto  wakiathirika zaidi mifupa ya miili yao kwa kupinda miguu na kuwa na vichwa vikubwa.

" Nichukue fursa hii kumpongeza Rais Samia kwa kuwaonea huruma wananchi wa Lemanda, na serikali ya awamu ya sita kwa ujumla, serikali inayowajali wananchi bila kubagua itikadi zao, leo Lemanda tumepata maji safi na salama kutoka kwa mamlaka ya maji safi na mazingira (AUSWA)  maji haya yalikuwa  kama ndoto kwa wananchi wangu " amesema Diwani huyo.

"Niwatake AUWSA kuhakikisha mnaweka vituo vya kuchotea maji vya kutosha kwa wananchi wote ambao hawana uwezo wa kuingiza maji ndani ya nyumba zao, wapate huduma karibu na makazi yao"  Amesema Lairumbe

Aidha sambamba na hilo amewataka wananchi wote wa kijiji cha Lemanda, kuhakikisha wanafika katika maeneo yote yaliyowekewewa vizimba kwa ajili ya kuchota maji kwa ajili ya matumizi ya kupikia na kunywa, kwa kuwa madhara ya Floraidi yanatokana na kula chakula kilichopikiwa maji yenye madini hayo pamoja na kunywa maji.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Lemanda,  Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Lemanda, Gaspa Mollel amesema kuwa imekuwa kama neema kwa  wananchi wa eneo hilo kutokana na ukweli kwamba, wananchi walikuwa wamekata tamaa ya kupata maji safi na salama, huku akiahidi kuongoza wananchi hao kutunza vyanzo vyote vya maji pamoja na kuendelea kuwahamasisha wananchi, juu ya umuhimu wa wananchi hao kutumia maji hayo safi na salama.

Naye Msimamizi Mkuu kutoka Maabara ya Ubora wa maji mkoa wa Arusha, Jovitus Kichumu amesema kuwa, kiwango cha madini ya Floraidi kwenye maji yanayopatikana Lemanda ni miligramu 18.7 kwa lita moja, kiwango ambacho ni kikubwa sana na kisichofaa kwa matumizi ya binadamu na kufafanua kuwa kwa sasa wananchi wameweza kutatuliwa kero hyo ya muda mrefu iliyo.

Katika mradi huu wa maji safi wa Oldonyosambu na ambao umefanikiwa kuondoa kero ya maji kwa wananchi 29,449 wa vijiji vya Oldonyosambu, Lemanda na Losinoni wenye  Tanki la lita efu 5, mradi wenye thamani ya shilingi bilioni 6.3 fedha kutoka serikali kuu, kupitia Mfuko wa maji wa Taifa na kutekelezwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Arusha '( AUWSA)

Hata hivyo wanufaika wa mradi huo, wameipongeza Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwaondolea kero ya muda mrefu ya ukosefu wa maji safi, kero iliyodumu kwa miaka nenda rudi inayozorotesha afya na uchumi wao.

Share To:

Post A Comment: