UTEPE wa michauano ya Kombe la ulinzi Cup umekatwa rasmi jana kwa mchezo mmoja kupigwa katika dimba la Magomeni ambapo timu ya Magomeni Star dhidi Edo Combine kutoka Mwakidila zilikutana na mchezo uliamuliwa kwa mikwaju ya Penati 4-2 baada ya dakika 90  kumalizika milango ya timu zote mbili ikiwa migumu kufunguka

Michauano hiyo iloliyoandaliwa na kudhaminiwa na jeshi la Polisi mkoa wa Tanga itazikitanisha timu 20 kutoka katika mitaa mbalimbali ya jiji la Tanga ikiwa na lengo hasa la kuhamasisha vijana kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya.

Akizindua michano hiyo  ya mpira wa miguu kwa vijana Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Tanga Henry Mwaibambe  alisema michezo  kwa sasa ni furaha na ajira lakini lengo lao hasa ni kipenyeza ujumbe kwa jamii kupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya.

Aidha alisema sambamba na ujumbe wa  michauano hiyo kwa mwaka huu bado jeshi hilo linaendelea kusistiza usalama wa maisha ya watu na mali zao  hivyo kuwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano pale wanapoona Kuna  viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani

Michauano hiyo itakayozihusisha timu 20  itachezwa kwa mfumo wa mtoano  mpaka bingwa apatikane kwenye fainali huku zawadi mbalimbali zikiwa zinazidi kuvutia timu kuzidi kujipanga zaidi.
Share To:

Post A Comment: