Na Oscar Assenga,TANGA
MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga Mhandisi Mwanaisha Ulenge amekabidhi mchele kilo 200 na Mbuzi katika Kituo cha Kulea Watoto Yatima cha Goodwil Humanity Foundation cha Jijini Tanga ili kuwawezesha kusheherekea kwa amani na upendo sikukuu ya Eid El Firi itakapotangazwa.
Mhandisi Ulenge alikabidhi vitu
hivyo katika kituo hicho baada ya kumalizika kwa Iftari iliyoandaliwa na Mbunge
huyo ambapo imekuwa ikifanyika kila mwaka kwa lengo la kuileta jamii pamoja iliyokutanisha
wadau mbalimbali.
Alisema katika kuelekea kumalizika
kwa mwezi mtukufu wa ramadhani ameona aunge mkono kufuturisha jamii ikiwemo
kutoa sadaka hiyo ili kuwawezesha watoto hao kusheherekea sikuuu ya Eid El
Fitri kwa amani na upendo wakati itakapotangazwa.
“Nimeona nitoe ili watoto waweze
kusherehekea sikuuu ya Eid El Fitri kwa kupata chakula kile bora ambacho mwana
Mtume amesema kiliwe siku ya Eid Pilau na Birian name kimekabidhi Mbuzi huyu na
kilo 200 za Mchele kwa ajili ya kituo hiki hapo itapotangazwa”Alisema Mhe
Ulenge
Awali akizungumza katika Iftari hiyo Mkurugenzi wa Goodwil and Humanity Foundation Sayyed Muhdhari Idarus alimshukuru Mbunge Ulenge kwa kuweza kuandaa futari hiyo katika kituo hicho huku akimuomba Mwenyezi Mungu amfalie afya njema na mafanikio.
Hata hivyo aliwashukuru mashehe waliojitokeza katika futari hiyo kwa lengo la kuimarisha amani na upendo ikiwemo kuzishukuru asasi zote zilizoendelea kuunga mkono juhudi za taasisi hiyo ikiwemo ndugu zao wa nyumba ya furaha iliyopo Bombo wamekuwa wakishirikiana
nao kulea watoto.

Post A Comment: