Articles by "ELIMU"
Showing posts with label ELIMU. Show all posts

 


📌Asema mikutano ya kitaaluma  inachochea mageuzi ya kiuchumi  na ubunifu;


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo (Mb),  amekitaka Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kuhakikisha wanatumia tafiti kuchochea mageuzi ya kiuchumi  kuelekea  Dira 2050.

Amesema hayo wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Saba wa Kitaaluma wa Kimataifa wa Mwaka 2026 ulioandaliwa na Chuo cha CBE uliofanyika Mwanza.

Londo amesema mkutano huo unachochea mageuzi ya mifumo ya kibiashara, ubunifu, urasimishaji na matumizi ya takwimu kuelekea ukuaji endelevu wa uchumi ambapo inaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita za kutekeleza Dira ya Taifa ya 2050 kwa vitendo.

Mhe. Londo pia ametoa rai kwa Taasisi za Serikali na Sekta Binafsi kuanza kutumia kikamilifu matokeo ya tafiti kutoka vyuo vya elimu ya juu ili kuleta tija na matokeo chanya kwa maendeleo ya Taifa.

Aidha amekitaka Chuo hicho kuandaa changanuzi za kisera (policy briefs) zitakazosaidia maboresho ya sera na mipango ya kiuchumi na kuweka mikakati ya kurudisha mrejesho kwa jamii kwa kuwasilisha matokeo ya tafiti kwa lugha rahisi, kuendesha mafunzo maalumu kwa wajasiriamali na wafanyabiashara, na kutoa rai kwa vyuo vingine kuiga mfano wa CBE katika kuandaa mikutano ya kitaaluma.

Vilevile amekitaka Chuo hicho kuendelea kuboresha kozi zake za muda mfupi na mrefu ili kuzalisha wataalamu wa kutosha watakaofundisha somo hilo mashuleni na kuimarisha elimu ya biashara nchini kwa kuwa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2023 imefanya somo la Biashara kuwa la lazima kwa wanafunzi wa Kidato cha Kwanza hadi cha Nne kuanzia mwaka wa masomo 2025/2026.

 

Banda la Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) limekuwa kivutio katika Maonesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Nduwa, mjini Sumbawanga, mkoani Rukwa, kutokana na umahiri wa vijana wahitimu na wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya VETA, hususan wenye ulemavu, wanaoonesha ujuzi walioupata kupitia mafunzo ya ufundi stadi.


Maonesho hayo yaliyoanza Oktoba 8 na yanayotarajiwa kuhitimishwa Oktoba 14, 2026, yanafanyika chini ya kaulimbiu “Mazingira Tofauti, Fursa Sawa kwa Vijana,” ambayo imetafsiriwa kwa vitendo kupitia ushiriki wa vijana wenye ulemavu wanaotumia ujuzi wao kubuni na kutengeneza bidhaa mbalimbali.

Miongoni mwa vijana wanaovutia ni Francis Madanganya, mhitimu wa TEHAMA kutoka VETA Kipawa na Chuo cha Ualimu wa Ufundi Stadi Morogoro, mwenye ubunifu wa kifaa cha kuhifadhi na kusambaza umeme kwa kompyuta mpakato (laptop); Gonsalva Lungu na Riziki Ndumba, wahitimu wa Ubunifu, Ushonaji na Teknolojia ya Nguo kutoka VETA Songea; Imelda Kanyengele, mwanafunzi wa fani hiyo VETA Nkasi; pamoja na Ernest Mashiku Igobeko, mhitimu wa useremala kutoka VETA Tanga ambaye ana ulemavu wa uoni.

Umahiri wa vijana hao umevutia wadau mbalimbali, wakiwemo wawakilishi wa Benki ya CRDB, ambao wamenunua bidhaa zao na kuwachangia fedha kwa ajili ya kukuza mitaji ya shughuli zao. Meneja wa Mahusiano na Taasisi za Serikali wa benki hiyo, Paskalina Diu, amesema wataangalia namna ya kuwawezesha vijana hao kupata mikopo na huduma za kifedha zitakazosaidia kukuza shughuli zao za kiuchumi.

Amesema kupitia CRDB Bank Foundation, benki hiyo ina fursa za kuwawezesha vijana kiuchumi, ikiwemo mitaji wezeshi isiyo na riba, ameeleza kuwa kliniki ya taasisi hiyo itatumika kuangalia namna bora ya kuwasaidia vijana wenye ujuzi wa ufundi stadi kujiajiri na kuendeleza shughuli zao.

Kwa upande wake, Imelda Kanyengele amesema mafunzo anayopata VETA Nkasi yamemwezesha kushona aina mbalimbali za nguo na kutengeneza batiki, akiwahimiza vijana wenzake, hususan wenye ulemavu, kutokata tamaa katika kutafuta elimu na ujuzi utakaowawezesha kujitegemea. Maonesho hayo yanatarajiwa kufunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu

 

Na Mwandishi Wetu.

Washiriki wa mafunzo kwa Waandishi wa Habari kutoka Wasafi Media wameeleza kuwa mada zilizotolewa katika mafunzo hayo zimewasaidia kutambua makosa yaliyokuwa yakijirudia katika utekelezaji wa majukumu yao na kuwapatia mwongozo wa kuboresha utendaji.

Wakizungumza wakati wa tathmini ya mafunzo hayo yaliyofanyika Septemba 17 na 18, 2026, katika Ofisi za Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) jijini Dar es Salaam, Gerald Hando, Aggai Kifumu na David Rwenyagira wameeleza kuwa mafunzo yamewaongezea uelewa kuhusu sheria, maadili na uzalendo katika uandishi wa habari.
Wamebainisha kuwa miongoni mwa changamoto zinazowakabili Waandishi wa Habari na wazalishaji wa maudhui ni shinikizo la kuongeza idadi ya wafuasi katika majukwaa ya kidijitali, kukidhi matakwa ya hadhira pana na kasi ya mabadiliko katika mazingira ya kidijitali kuwa kubwa kuliko maboresho ya baadhi ya sheria zinazoongoza shughuli zao.

Kwa mujibu wa washiriki hao, mazingira hayo yanaweza kusababisha baadhi ya Waandishi wa Habari kufanya kazi kwa mazoea au kujikuta wakifanya makosa ya kisheria na kimaadili bila kuwa na uelewa wa kutosha.
Wamesema mafunzo hayo yamewajenga kitaaluma, yamewafungua kutoka katika utendaji wa mazoea na kuwapatia mwongozo wa kufanya maamuzi sahihi katika majukumu yao ya kila siku.

Aidha, wameiomba JAB kuendelea kutoa mafunzo hayo kwa Waandishi wa Habari kutoka vyombo vingine, huku kipaumbele kikitolewa kwa wanaofanya kazi na kuzalisha maudhui kupitia majukwaa ya kidijitali, ambako changamoto za uzingatiaji wa sheria na maadili zimeendelea kujitokeza.
Wamesema kasi ya uzalishaji na usambazaji wa maudhui katika majukwaa hayo imeongeza uwezekano wa kutokea kwa makosa ya kisheria na kimaadili, hivyo elimu endelevu inahitajika ili kuimarisha weledi na uwajibikaji.

Mafunzo hayo yalihusu Sheria ya Huduma za Habari, maadili ya uandishi wa habari na uzalendo, yakilenga kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari na watangazaji wa Wasafi Media kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, viwango vya taaluma na maslahi ya jamii.

 


UNESCO and Beijing Normal University (BNU) provide students from 10 schools with opportunities to explore ICT, innovation and pathways into STEM careers

MOROGORO, TANZANIA – 17 September 2026:

For a group of Form One girls from 10 secondary schools across Morogoro Region, technology is beginning to mean much more than simply using a smartphone or accessing the internet. It is becoming a space where they can learn, create, solve problems and imagine new possibilities for their future.

This shift in perspective is at the heart of a three-day girls’ Bootcamp being held at Kilakala Girls Secondary School from 16 to 18 September 2026, under the UNESCO–Beijing Normal University (BNU) project, “Closing the Digital Divide: Ensuring Gender-Transformative Digital Skills Education for Women and Girls.


The journey began on 15 September 2026 with a meeting held at Odema Hotel in Morogoro, before the students moved into the Bootcamp phase, which officially began on 16 September 2026 at Kilakala Girls Secondary School, where the training is continuing until tomorrow, 18 September 2026.

The project is implemented by UNESCO with funding support from Beijing Normal University (BNU), technical support from the UNESCO International Research and Training Centre for Rural Education (UNESCO-INRULED), and in collaboration with the Government of the United Republic of Tanzania.



The initiative seeks to strengthen girls’ digital skills, increase their interest and understanding of ICT education and careers, and challenge gender stereotypes and expectations that can discourage girls from pursuing technology-related fields.

Helping Girls See Their Place in Science and Technology

For many of the girls participating in the Bootcamp, the experience provides an opportunity to look at technology from a different perspective.

Rather than seeing ICT as something mainly associated with boys or as a tool for basic communication, the girls are being encouraged to see themselves as potential innovators, researchers, engineers, entrepreneurs and creators of digital solutions.

This approach responds directly to one of the challenges identified by the project: gender stereotypes and social expectations that may portray technology as a male-dominated field, affecting girls’ confidence, interest and sense of belonging in ICT-related education and careers.

By creating opportunities for girls to engage with digital skills and female role models, the project aims to help them recognise that their future can include technology—not only as users, but also as creators and problem-solvers.

When Technology Meets Real-Life Challenges

One of the sessions during the Bootcamp, “Gender, Technology and ICT in the Agriculture Sector,” delivered by Dr Lily Makalanga Bogohe, demonstrates how technology can be connected to everyday challenges facing communities.

The session highlighted the important contribution of women to food production while drawing attention to barriers that can limit women’s access to digital technologies, including the cost of smartphones and data, limited digital skills, and social and gender-related constraints.

At the same time, the session explored how digital technologies can create opportunities for women and girls, including access to market information, weather information, mobile financial services and other digital resources that can support livelihoods and decision-making.

The lesson for the girls is clear: technology is not separate from real life. It can be used to understand problems, develop solutions and improve the way people live and work.

Challenging the Idea That Technology Is “For Boys”

The Bootcamp also creates space to question one of the persistent barriers to girls’ participation in technology: the belief that science and technology are primarily for boys.

The project recognises that limited female role models and restricted exposure to ICT education and career pathways can influence how girls perceive their own possibilities.

Through practical learning, mentorship and exposure to technology-related opportunities, the girls are being encouraged to build confidence and develop a stronger understanding of where digital skills can take them.

The message is not simply about teaching girls how to use technology. It is about helping them understand that they can participate in shaping the technologies and solutions that respond to the needs of their communities.

Starting the STEM Journey Early

The Bootcamp comes at an important stage in the girls’ education. As Form One students, they are at an early point in their secondary school journey, when exposure to new fields of knowledge can help shape their interests and aspirations.

The project’s focus on digital skills, ICT education and career pathways provides an opportunity for girls to begin exploring fields related to science, technology, engineering and mathematics (STEM), while developing the confidence to consider ICT-related studies and careers.

The broader objective is to ensure that girls are not left behind as technology continues to transform education, employment and society.

By investing in girls’ digital skills today, the initiative contributes to a future in which more women can participate meaningfully in technology, innovation and digital transformation.

From Learning to Possibility

The Bootcamp is more than a three-day learning activity. It is an opportunity for girls to see possibilities that may not previously have been visible to them.

As the sessions continue at Kilakala Girls Secondary School, the experience is helping participants connect digital skills with real-world challenges, explore their interests and begin thinking about the role technology could play in their education and future careers.

Ultimately, the project seeks to create an environment in which girls can develop the skills, confidence and understanding needed to participate in the digital world on equal terms. Its communication approach also places emphasis on documenting girls’ experiences, achievements, role models and pathways into ICT education and careers.

For the girls of Morogoro, the journey is only beginning.

Science and technology are not only for boys. Girls, too, can learn, innovate, create solutions and help shape the digital future.

 

Kikao kinaweka msingi wa kuimarisha elimu kuhusu bahari, uhifadhi wa mazingira na uchumi wa buluu

ZANZIBAR: Tume ya Taifa ya UNESCO inafanya mashauriano na Menejimenti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kuhusu uanzishwaji wa Programu ya Shule za Bluu (Blue Schools Programme), inayolenga kuwajengea wanafunzi uelewa na maarifa kuhusu umuhimu wa bahari katika maisha ya binadamu, uhifadhi wa mazingira, mabadiliko ya tabianchi na fursa za uchumi wa buluu.

Kikao hiki kinaendelea Zanzibar, huku Tume ya Taifa ya UNESCO ikiwakilishwa na Naibu Katibu Mtendaji wa Tume, Dkt. Khamis Khalid Said. Majadiliano yanajikita katika kujenga uelewa wa pamoja kuhusu programu hiyo na kuweka msingi wa hatua zinazofuata kuelekea uanzishwaji wake Zanzibar.

Programu ya Shule za Bluu inalenga kukuza Elimu kuhusu Bahari (Ocean Literacy) kwa kuwawezesha wanafunzi kuelewa bahari, uhusiano wake na maisha ya binadamu na namna shughuli za binadamu zinavyoathiri mazingira ya baharini.

Kupitia mpango huo, shule zinapata fursa ya kuunganisha elimu ya bahari na mazingira, uendelevu na maisha ya jamii, huku wanafunzi wakijengewa uwezo wa kutambua thamani ya bahari na wajibu wao katika kuitunza.

Kwa Zanzibar, ambako bahari ni sehemu muhimu ya mazingira, maisha ya jamii na shughuli mbalimbali za kiuchumi, kuimarisha elimu kuhusu bahari katika shule kunatoa fursa ya kuwaandaa wanafunzi kuwa kizazi kinachotambua thamani ya rasilimali hizo na umuhimu wa kuzitumia kwa njia endelevu.

Elimu hiyo inagusa maeneo mbalimbali, yakiwemo uhifadhi wa mazingira ya baharini, mabadiliko ya tabianchi, uchafuzi wa bahari, matumizi endelevu ya rasilimali za bahari na fursa za uchumi wa buluu.

ELIMU YA BAHARI KUELEKEA TANZANIA YA 2050

Majadiliano kuhusu Shule za Bluu yanaendana na mwelekeo mpana wa Tanzania wa kuwekeza katika elimu, ujuzi, sayansi, teknolojia na ubunifu, pamoja na matumizi endelevu ya rasilimali kwa ajili ya maendeleo ya muda mrefu.

Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inaweka mkazo katika kujenga rasilimali watu yenye maarifa na ujuzi, kukuza ubunifu na kuimarisha matumizi endelevu ya rasilimali za Taifa.

Katika muktadha huo, elimu kuhusu bahari inatoa fursa ya kuwaandaa wanafunzi mapema kuelewa fursa na changamoto zinazohusiana na bahari, ikiwemo nafasi ya uchumi wa buluu katika maendeleo ya Tanzania.

Kujenga uelewa huo shuleni kunaweza pia kusaidia kuandaa kizazi chenye uwezo wa kutumia maarifa, sayansi na ubunifu kutafuta suluhisho la changamoto za mazingira na mabadiliko ya tabianchi.

KUJENGA KIZAZI CHENYE UFAHAMU WA BAHARI

Dhana ya Shule za Bluu inaweka mwanafunzi katika nafasi ya kuwa sehemu ya kujifunza, kutafakari na kuchukua hatua kuhusu mazingira yanayomzunguka.

Kupitia elimu hiyo, wanafunzi wanaweza kuelewa uhusiano kati ya bahari, mazingira, uchumi na maisha ya jamii, na namna maamuzi ya sasa yanavyoweza kuathiri rasilimali za bahari kwa vizazi vijavyo.

Kwa mtazamo huo, shule inaweza kuwa sehemu muhimu ya kujenga utamaduni wa kuhifadhi mazingira, huku walimu na wanafunzi wakishirikiana na jamii katika kukuza uelewa kuhusu bahari na matumizi yake endelevu.

TUME YA TAIFA YA UNESCO YAWEKA MSINGI WA HATUA ZINAZOFUATA

Akizungumzia kikao hicho, Dkt. Khamis Khalid Said anaeleza kuwa majadiliano yanawezesha kujenga uelewa wa pamoja kati ya Tume ya Taifa ya UNESCO na Menejimenti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kuhusu Programu ya Shule za Bluu.

“Kikao hiki kinatuwezesha kujenga uelewa wa pamoja kuhusu Programu ya Shule za Bluu na kuweka msingi wa namna nzuri ya kuendelea na hatua zinazofuata kuelekea uanzishwaji wa programu hii Zanzibar,” anasema Dkt. Khamis.

Kikao kinaendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Tume ya Taifa ya UNESCO na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar katika kuangalia namna elimu kuhusu bahari inaweza kuimarishwa katika mazingira ya shule na kuhusishwa na mahitaji ya maendeleo ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Hatua hii pia inaendana na juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuimarisha elimu na ujuzi, kukuza sayansi, teknolojia na ubunifu, pamoja na kuhimiza matumizi endelevu ya rasilimali katika kuchochea maendeleo ya Taifa.

Katika safari kuelekea Tanzania ya 2050, kuwekeza katika elimu kuhusu bahari kunaweza kusaidia kujenga kizazi chenye maarifa, ujuzi na ubunifu wa kutambua fursa za uchumi wa buluu na wakati huo huo kuwa na uelewa wa wajibu wa kulinda mazingira ya baharini.

Kwa kuanzia shuleni, elimu kuhusu bahari inaweza kuwa msingi wa kujenga kizazi kinachoifahamu bahari, kinathamini rasilimali zake na kinakuwa tayari kushiriki katika kuzitunza kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Tume ya Taifa ya UNESCO inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuendeleza programu zinazotumia elimu, sayansi, utamaduni na mawasiliano kama nyenzo za kuchangia maendeleo endelevu ya Tanzania.

 

Mratibu wa Mafunzo ya Kidijitali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Eng. Joyce Baravuga, amesema mafanikio ya Mradi wa Kuziba Pengo la Kidijitali: Kuhakikisha Elimu ya Ujuzi wa Kidijitali Inayozingatia Usawa wa Kijinsia kwa Wanawake na Wasichana (Closing the Digital Divide: Ensuring Gender-Transformative Digital Skills Education for Women and Girls) yatategemea kwa kiasi kikubwa utayari wa shule kuendeleza mafunzo na shughuli za Klabu za TEHAMA (ICT Clubs) baada ya kumalizika kwa Kambi ya Mafunzo (Boot Camp).

Eng. Baravuga amewapongeza wakuu wa shule zilizochaguliwa kushiriki katika programu hiyo, akisema utayari na uthubutu wa shule ni miongoni mwa vigezo vilivyozingatiwa katika uteuzi.

Amesema shule hizo zinapaswa kuwa wadau muhimu wa programu hiyo kwa kuhakikisha maarifa na ujuzi unaopatikana kupitia mafunzo unaendelea kutumika shuleni na kuwafikia wanafunzi wengine.

Amewataka walimu na wakuu wa shule kuhakikisha Klabu za TEHAMA zinaendelea baada ya wanafunzi kurejea shuleni, ili kuwapa wasichana nafasi ya kuendelea kujifunza, kufanya mazoezi na kuendeleza ubunifu wao katika teknolojia.

Aidha, amewataka walimu, hususan wanaohusika na TEHAMA, kushiriki kikamilifu katika mafunzo hayo na kuhakikisha maarifa yanayopatikana hayabaki kwa wanafunzi walioshiriki pekee, bali yanawafikia wanafunzi wengine shuleni.

Eng. Baravuga pia amesisitiza umuhimu wa kukusanya taarifa za utekelezaji wa shughuli za mafunzo kila siku, akisema taarifa hizo zitasaidia kupima mafanikio ya programu, kubaini changamoto na mapungufu, pamoja na kuweka msingi wa kuboresha utekelezaji katika hatua zijazo.

Amesema ukusanyaji wa taarifa kwa wakati utasaidia pia kutambua maeneo yanayohitaji kupewa msukumo zaidi na kuhakikisha malengo ya programu yanafikiwa.

Vilevile, amesisitiza umuhimu wa wanafunzi kuchaguliwa kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa bila upendeleo, ili kuhakikisha fursa zinazotolewa kupitia programu hiyo zinawafikia walengwa kwa usawa.

Eng. Baravuga amesema ushiriki wa shule, walimu na viongozi wa shule ni muhimu katika kuhakikisha Kambi ya Mafunzo haibaki kuwa tukio la muda mfupi, bali inakuwa mwanzo wa kujenga mazingira endelevu ya kujifunza, kutumia na kubuni kupitia TEHAMA miongoni mwa wanafunzi.

MOROGORO, September 14, 2026: The journey to equip girls with the digital skills, confidence and opportunities they need to participate in the technology-driven future has moved to Morogoro.

Following the official launch of the UNESCO-BNU ICT Clubs programme in Dodoma on September 7, 2026, UNESCO, in collaboration with Beijing Normal University (BNU) and the Government of the United Republic of Tanzania, today launched the Morogoro phase of the initiative, which will run from September 14 to 18, 2026.

The programme is being implemented under the UNESCO-BNU project, “Closing the Digital Divide: Ensuring Gender-Transformative Digital Skills Education for Women and Girls,” aimed at addressing the gender gap in digital education and expanding opportunities for women and girls to participate meaningfully in the digital economy and technology sector.

The Morogoro phase builds on the experience gained in Dodoma, where participating students were introduced to practical digital learning and innovation through ICT Clubs.

Rather than limiting technology education to theory, the programme gives girls opportunities to learn by doing—developing skills in coding, computational thinking, problem-solving, digital creativity, visual and audio content production, and the safe and responsible use of technology.

The experience in Dodoma demonstrated the value of creating spaces where girls can explore technology, ask questions, experiment with ideas and develop solutions to real-life challenges.

More importantly, the initiative seeks to nurture confidence and aspiration, enabling girls to see technology not simply as something they consume or use, but as a field in which they can create, innovate and build careers.

Speaking during the Morogoro launch, UNESCO Tanzania Head of Education Sector, Dr Faith Shayo, encouraged girls to take advantage of the opportunities provided through the ICT Clubs and to challenge perceptions that technology-related learning and careers are primarily for boys.

She emphasized the importance of creating learning environments where girls feel confident to experiment, make mistakes, ask questions and develop their abilities in technology.

The message is clear: girls should not only be users of technology; they should also be creators, innovators and future leaders in the digital world.

FROM LEARNING TO CREATING

Through the ICT Clubs, students are expected to gain practical experience while developing creativity, collaboration, problem-solving and leadership skills.

The programme will also connect girls with women ICT professionals through mentorship, giving them opportunities to learn from their experiences and gain a broader understanding of education, employment and career pathways in the technology sector.

For a girl writing her first line of code, developing a digital idea or using technology to solve a community problem, such experiences can represent more than a new skill.

They can be the beginning of a new ambition.

The ambition to become a programmer, engineer, developer, digital creator, entrepreneur, innovator—or a future leader in technology.

ICT INNOVATION BOOTCAMP STARTS TOMORROW

The Morogoro programme continues tomorrow, September 15, 2026, with an ICT Innovation Bootcamp at Kilakala Secondary School, a girls’ school.

The Bootcamp will provide participants with hands-on opportunities to strengthen their digital skills, develop innovative ideas and work collaboratively on technology-based solutions to real-life challenges in their communities.

The activities will reinforce the programme’s emphasis on practical learning, creativity and innovation, while encouraging girls to explore their potential in ICT.

The Morogoro activities will continue through September 18, 2026.

A SHARED COMMITMENT

The initiative is being implemented in collaboration with the Ministry of Education, Science and Technology (MoEST), the Prime Minister’s Office – Regional Administration and Local Government (PMO-RALG), and the Tanzania Institute of Education (TIE).

Across Dodoma and Morogoro, the programme is expected to strengthen ICT Clubs in 20 public schools, directly benefiting 500 girls and 40 teachers.

The ICT Clubs are intended to provide safe, inclusive and supportive learning environments where students can develop digital skills, creativity, leadership and collaboration, while gaining greater awareness of opportunities in ICT-related education and careers.

As the programme moves from Dodoma to Morogoro, the goal remains the same: to ensure that girls are not left behind in the digital transformation.

They must have the opportunity to learn technology.

They must have the confidence to use it.

They must have the freedom to create with it.

And they must have the opportunity to build their future through it.

From Dodoma to Morogoro, the journey continues—one girl, one skill and one digital opportunity at a time.

The future of technology needs girls. Let us give them the skills, confidence and opportunity to build it.

#UNESCO #BNU #GirlsInICT #ICTClubs #DigitalSkills #DigitalEducation #GirlsInTechnology #ClosingTheDigitalDivide #Morogoro #Tanzania

 1789036939464 (1).jpg



Technology is not only for boys.

Girls belong in technology too.

Inside the UNESCO–BNU Closing the Digital Divide Project Boot Camp, girls are gaining

hands-on experience with technology—learning, exploring, collaborating and building their

digital skills.

But this is about more than learning how to use computers.

It is about challenging the belief that technology is a space for boys.

When girls are given the opportunity to learn, participate and explore technology, they can

build confidence, discover their potential and begin to see themselves as creators,

innovators and future leaders.

Let’s break the stereotypes.

Let’s open equal opportunities.

Let’s empower girls to shape the digital future.

GIRLS BELONG IN TECH.

UNESCO–BNU: Closing the Digital Divide Project

#GirlsInTech

 

The room comes alive as the girls settle into their groups.

Around the tables, conversations begin.

One idea leads to another as the students share their views, listen to their colleagues and work together to understand the challenges they have been given.

As part of the UNESCO-BNU project, this is learning by participation.


The girls are not sitting back and waiting for answers.

They are thinking for themselves, exchanging ideas and challenging one another as they work towards a common solution.

You can see the teamwork taking shape.


Some students speak. Others listen carefully. Ideas are added, discussed and refined.

What looks like a simple classroom discussion is becoming something much bigger—a practical exercise in critical thinking, collaboration and confidence.


And gradually, each group begins to shape its ideas into something they can share.

The discussions continue, the ideas become clearer, and the girls prepare for the next moment.

It is time to stand up and let the whole class hear what they have created together.



 


DODOMA, TANZANIA — September 8, 2026.

Day One of the Bootcamp at Msalato Girls Secondary School in Dodoma began with the girls taking an active role in the learning process.


Working in groups, the students engaged in discussions, sharing ideas and exploring different challenges that could be addressed through technology.


The discussions gave the girls an opportunity to work together, listen to different perspectives and develop ideas as a team.

After the group discussions, the students came together for presentations.


Standing before the whole class, the groups presented the ideas they had developed during their discussions, giving each student an opportunity to participate and share what her group had explored.


Through this process, the girls were beginning to build important skills in teamwork, communication, confidence and problem-solving.


It was the first practical step of the Bootcamp—moving from discussion to presentation, and creating a foundation for the hands-on technology sessions that followed.


Day One had begun with an important lesson: ideas become more powerful when they are shared, challenged and developed together.