Bertha Mollel, Arusha

Jumla ya walim 500 wa shule za sekondari nchini wameanza kupatiwa mafunzo ya matumizi sahihi ya Tehama na Vishkwambi ili kupata mbinu mpya ya kuzitumia kwenye kufundishia.

Mafunzo hayo yamekuja ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu aliyoyatoa siku ya Mei mosi 2023 baada ya kusoma moja ya bango la walimu walioomba kupatiwa mafunzo ya jinsi ya kutumia vishkwambi kufundishia.

Akifungua mafunzo hayo mkoani Arusha, Naibu katibu mkuu wizara yenye dhamana ya Elim, Dkt. Franklin Rwezimula alisema mafunzo hayo ya siku tano yanalenga kuwafundisha walimu 1500 walioko kazini mbinu mpya za matumizi ya Tehama na vishkwambi katika kufundishia ili nao wakafundishe wenzao.

"Mafunzo haya yako chini ya mradi wa miaka mitano unaolenga  'kuboresha mazingira ya ujifunzaji, ufundishaji kwenye shule zetu za sekondari' (SEQUIP) , ikiwa ni utekelezaji wa mapinduzi makubwa ya Elimu" 

Dkt. Rwezimula aliwataka walimu hao kuwa makini katika mafunzo hayo yakalete tija kusudiwa na wakawe mabalozi wazuri kwenye maeneo yao ya kazi.

"Dunia imezama kwenye sayansi na Teknolojia, hivyo wizara inaegemea kuwanoa ninyi msitumie tena analogi bali muenende na mabadiliko hayo, hivyo basi na nyie bebeni dhamana ya kwenda kuwasaidia wenzenu"

kwa upande wake mratibu wa SEQUIP, Dkt Mollel Meigaru alisema kuwa Mafunzo hayo yanayolenga kuimarisha Elim ya sekondari nchi nzima ulioko chini ya ufadhili wa benki ya dunia kwa mkopo wa dola milioni 500.

"Mbali na mafunzo haya, pia mradi umefanikisha walimu 18,000 namna bora ya kufundisha masomo ya sayansi, na kuhusisha na tehama, lakini pia unalenga kujenga miundo mbinu kwa shule za sekondari ambao unatarajia kujenga shule 1000 za mchanganyiko na zingine 26 za wasichana"alisema

Alisema mafanikio hayo kwa walimu wanatarajia kuongeza ufaulu kwa wanafunzi hasa wa masomo ya Sayansi nchini na kwenda kuwa msaada mkubwa kwa Taifa baadae.

Nae Afisa Elim mkoa wa Arusha, Shilei Swai aliishukuru serikali kuwapatia walimu wake mafunzo hayo ambayo wanatarajia yataenda kuongeza ufaulu kwa wanafunzi hasa wa masomo ya Sayansi nchini na kwenda kuwa msaada mkubwa kwa Taifa baadae.

kwa upande wake Mkurugenzi wa Elimu ya watu wenye mahitaji maalum, Dkt. Magreth Matonya aliwataka walimu wenye mahitaji maalum waliopata nafasi ya kuhudhuria mafunzo hayo wakawe wakufunzi wazuri kwa wenzao wanaokwenda kufanya nao kazi.

Share To:

Post A Comment: