Na Elizabeth Joseph, Monduli.


Katika kuadhimisha Miaka 61 ya Uhuru Tanzania Serikali Wilaya ya Monduli yamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa maendeleo ikiwemo Afya na Elimu wilayani humo.


Shukrani hizo zimetolewa Disemba 9 na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mh,Frank Mwaisumbe katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Barafu Mto wa Mbu ambayo pia yalihudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali,Dini,Chama Cha CCM na viongozi wa Mila.


Mwaisumbe alibainisha kuwa serikali ya Mama Samia imesaidia kutekeleza miradi mingi ya maendeleo wilayani humo kwa kipindi kifupi na kusema wao kama serikali wanajivunia Uhuru ulioleta maendeleo yenye kasi zaidi.


"Wana Monduli hatuna kazi kubwa kuelekea 2025 sababu tuna ushahidi wa maendeleo ndani ya Wilaya yetu ambayo yamefanywa na Mama yetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambayo tungependa na vizazi vyetu vije kufaidi haya maendeleo kwa kumpa ushirikiano Rais wetu"alibainisha Mwaisumbe.


Aidha aliwataka watanzania kuwa wazalendo na kudumisha Umoja na Amani iliyoanzishwa na waasisi wa Taifa la Tanzania  ikiwa ni pamoja na kuyaenzi na kuyatekeleza kwa vitendo yote mazuri yaliyofanywa toka kupata Uhuru.


Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli Mh,Isack Copriano aliwaomba watanzania kuadhimisha siku hiyo kwa kueleza maendeleo yanayofanywa na serikali iliyopo madarakani na kuongeza kwa Kipindi cha miaka mitatu Halmashauri hiyo imepokea bajeti ya Bilioni 2.6 kwenye miradi ya maendeleo.


Kwa upande wake Bi,Sarah Lomayani ambaye ni moja wa mashuhuda wa Tanzania ilipopata Uhuru aliwataka watanzania kudumisha Mila na tamaduni ikiwa ni pamoja na kuwa na maadili mema katika jamii.


"Tuenzi Desturi zetu nzuri za zamani kwa kuwaheshimu na kusikiliza wakubwa wanasema nini pamoja na kuwaenzi viongozi wetu waliotutoa mbali hadi hapa tulipo hili jambo la kujivunia sana"aliongeza Bi,Lomayani.


Katika maadhimisho hayo vikundi mbalimbali vya burudani vilitumbuiza pamoja mchezo wa kukimbiza kuku na mpira wa miguu.

Share To:

Post A Comment: