NA DENIS CHAMBI, TANGA.

IDADI ya watanzania wanaotembelea hifadhi mbalimbali zilizopo hapa nchini  zinzo simamiwa na shirika la hifadhi ya Taifa 'TANAPA' inazidi kuongezeka kadiri siku zinavyokwenda hii ikichangiwa zaidi na a elimu inayotolewa sambamba na  hamasa iliyopatikana kufwatia uzinduzi wa Royal tour uliofanywa na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan nchini Marekani mwaka 2022..

Hayo yamebainishwa na afisa utalii kutoka hifadhi za Taifa  'TANAPA' Athumani Mbae wakati akizungumza katika maonyesho ya biashara na utalii yanayofanyika kila mwaka mkoani Tanga ikiwa ni ya 10 yakihusisha taasisi na makampuni ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali wajasiriamali wakubwa, wa kati na wadogo wadogo , yakiwa na lengo la kutangaza biashara na huduma zinazotolewa kwa wananchi.

Mbae lisema hifadhi zote zinazosimamia na TANAPA zimekuwa zikipata watalii wengi wa ndani na nje hii ikisadifu matokeo na hamasa kubwa iliyopatkana kupitia filamu ya Royal tour iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa ni jitihada za serikali ya awamu  ya 6 kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia sekta ya utalii.

"Kwa kweli utalii unakuwa siku hadi siku na hii inayokana na juhudi kubwa ambazo zinafanywa na shirika la hifadhi za Tanzania  "TANAPA" lakini pia kupitia Royal tour ambayo alizindua Rais Samia Suluhu Hassan  amefanya juhudi kubwa kuzitangaza hizi hifadhi tangu ametoa  filamu hiyo utalii umekuwa na tumejulikana sana  kimataifa tunapata wageni wengi kutoka nje  lakini pia na watalii wa ndani na hata watanzania wenyewe  wamekuwa na muamko  kwa kuona kwamba Rais wetu anaweka juhudi kubwa katika sekta ya utalii" alisema Mbae.

Aliongeza kuwa  licha ya ongezeko la watalii wa ndani na nje katika hifadhi zilizopo kumekuwa na changamoto ya miundombinu mibovu hasa kipindi cha mvua barabara zimekuwa hazipitiki kiurahisi  hata hivyo serikali iliona hilo   ambapo ilitoa fedha kwaajili ya ukarabati wa barabara zote ili kuhakikisha zinapitika kiurahisi.

" Changamoto kama ya miundombinu wakati wa masika inakuwa na shida kwamba ufikikaji wa maeneo ya hifadhi kidogo  barabara  zinaleta shida lakini serikali inaleta fedha nyingi za kurekebisha hizo barabara  kwa sasa hivi barabara  zote zinapitika kwa muda wote"alisema mhifadhi huyo.

Alisema kupitia maonyesho ya biashara na utalii yanayofanyika kila mwaka mkoani Tanga  kumekuwa na tija kwa upande wa TANAPAambapo wanayatumia  kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kuvijua vivutio vilivyopo sehemu mbalimbali hapa nchini na faida ya kuvitembelea.

"Ni fursa  ya kipekee  kupitia maonyesho haya kuzitangaza  hifadhi ya Taifa ya Saadani kwa wakazi wa Tanga lakini pia kwa watanzania wote kuvijua vivutio mbalimbali vilivyopo  kuwafanya kuzielewa hizi mbuga ziko wapi , vivuyio vilivyopo , shughuli zinazofanyika, huduma zinazopatikana  na faida zake " aliongeza.

Shirika la hifadhi ya Tanzania 'TANAPA'  linalosimamia hifadhi takribani 22  hapa nchini zikiwemo  Mkomazi, Mikumi , Saadan, hifadhi ya Nyerere, na nyinginezo linaendelea kuwakaribisha  watanzania (watalii wa ndani ) kwenda kutembelea na kujifunza na kujionea vivutio mbalimbali vinavyopatikana  ambapo oiinhilio ni shilingi elfu tano Mia nne(5,900) kwa watalii wa ndani..

 

 

 

Afisa utalii kutoka hifadhi za Taifa  'TANAPA' Athumani Mbae akiwaelekeza wanafunzi wa shule za  sekondari na msingi waliotembelea banda hilo katika maonyesho ya biashara na utalii yanayofanyika kila mwaka mkoani Tanga.
 


Share To:

Post A Comment: