Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, akizungumza wakati wa Warsha ya Kujenga Uelewa kwa Wadau  Juu ya  Mkakati na Miongozo ya Kitaifa kuhusu Matumizi ya Teknolojia za Kidijitali kwenye Sekta ya Elimu iliyofanyika leo Januari 14,2026 jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (Sekta ya Sayansi), Prof Daniel Mushi, akizungumza wakati wa Warsha ya Kujenga Uelewa kwa Wadau  Juu ya  Mkakati na Miongozo ya Kitaifa kuhusu Matumizi ya Teknolojia za Kidijitali kwenye Sekta ya Elimu iliyofanyika leo Januari 14,2026 jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo (hayupo pichani),wakati wa Warsha ya Kujenga Uelewa kwa Wadau  Juu ya  Mkakati na Miongozo ya Kitaifa kuhusu Matumizi ya Teknolojia za Kidijitali kwenye Sekta ya Elimu iliyofanyika leo Januari 14,2026 jijini Dodoma.

Wadau  wakichangia mada mbalimbali wakati wa Warsha ya Kujenga Uelewa kwa Wadau  Juu ya  Mkakati na Miongozo ya Kitaifa kuhusu Matumizi ya Teknolojia za Kidijitali kwenye Sekta ya Elimu iliyofanyika leo Januari 14,2026 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua  Warsha ya Kujenga Uelewa kwa Wadau  Juu ya  Mkakati na Miongozo ya Kitaifa kuhusu Matumizi ya Teknolojia za Kidijitali kwenye Sekta ya Elimu iliyofanyika leo Januari 14,2026 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imezitaka taasisi zote za elimu nchini kuongeza ubunifu na ufanisi katika ufundishaji na ujifunzaji kupitia matumizi bora, salama, na yenye uwajibikaji wa teknolojia za kidijitali.

Hayo yamesemwa   na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo,wakati wa Warsha ya Kujenga Uelewa kwa Wadau  Juu ya  Mkakati na Miongozo ya Kitaifa kuhusu Matumizi ya Teknolojia za Kidijitali kwenye Sekta ya Elimu iliyofanyika leo Januari 14,2026 jijini Dodoma.

Prof. Nombo amewataka wadau wa elimu kuzingatia mabadiliko ya kidijitali kama hitaji la lazima, huku akisisitiza kwamba ustawi wa baadaye wa Tanzania unategemea nguvu kazi yenye ujuzi wa kidijitali na ubunifu, kama inavyobainishwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

“Mkakati huu unalenga kuweka mfumo wa kitaifa wa kuratibu na kuongoza mageuzi ya kidijitali katika ngazi zote za elimu kuanzia shule, vyuo vya ualimu, taasisi za TVET, vyuo vikuu, hadi ujifunzaji wa mtandaoni,” amesema Prof. Nombo.

Aidha, Prof. Nombo amesisitiza umuhimu wa ufundishaji wa kidijitali na ujumuishaji wa TEHAMA, pamoja na uelewa wa Akili Unde  (AI) na stadi za data katika mafunzo ya walimu. Ameeleza kuwa maendeleo endelevu ya kitaaluma kupitia majukwaa ya kidijitali ni muhimu ili kuwawezesha walimu kutumia teknolojia kwa ubunifu na uwajibikaji.

“Nafasi ya walimu ni nguzo kuu ya mageuzi kidijitali. Teknolojia peke yake haiwezi kuleta mabadiliko bila walimu wenye ujuzi na utayari wa kutumia teknolojia za kufundishia na kujifunzia,” amefafanua.

Prof. Nombo pia amesisitiza umuhimu wa Miongozo ya Kitaifa ya Elimu ya Kidijitali na Mwongozo wa Matumizi ya Akili Unde  katika Elimu, ambayo inalenga kuhakikisha matumizi ya teknolojia hayaingilii maadili, ulinzi wa data, ujumuishi, na ubora wa kitaaluma. Vyuo vikuu na taasisi za utafiti wanahimizwa kuongeza ubunifu na utafiti unaozingatia AI na teknolojia nyingine zinazochipuka.

Aidha,ametoa wito kwa taasisi za udhibiti na uthibitishaji ubora kama TCU, NACTVET, COSTECH, TCRA na ICTC kushirikiana na wizara na kutoa elimu ili kuhakikisha mshikamano wa kisera, ulinganifu, na muingiliano wa mifumo sambamba na sera na miongozo ya kitaifa.

Prof. Nombo amewahimiza kutoa  ushirikiano na washirika wa maendeleo na sekta binafsi, wakihimizwa kuunda suluhisho zinazolingana na muktadha wa Tanzania na kuunga mkono ukuaji wa stadi, ubunifu, na uendelevu wa elimu ya kidijitali.

“Usambazaji ni hatua ya kwanza tu. Utekelezaji unahitaji uongozi, uratibu, rasilimali na uwajibikaji. Naomba taasisi zote kuingiza Mkakati wa Kitaifa wa Elimu ya Kidijitali na Miongozo yake katika mipango yao, kuteua waratibu, kutenga rasilimali, na kushiriki kikamilifu katika ufuatiliaji, tathmini na kujifunza kwa pamoja.”amesema Prof. Nombo

Kwa upande wake,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (Sekta ya Sayansi), Prof Daniel Mushi, amepongeza hatua ya Serikali kuandaa Mkakati na Miongozo ya Kitaifa ya Matumizi ya Teknolojia za Kidijitali katika Elimu, akisema juhudi hizo zinaweka msingi madhubuti wa mageuzi ya elimu yanayoendana na kasi ya dunia ya sasa.

 Prof Mushi amesema  hatua hiyo inalenga kuboresha ubora wa ufundishaji na ujifunzaji, kukuza ubunifu, na kuwaandaa walimu na wanafunzi kukidhi mahitaji ya zama za kidijitali.

Warsha hiyo ya siku mbili, inayofanyika Januari 14–15, 2026, inawakutanisha wataalam na viongozi mbalimbali wakiwemo makatibu wakuu, wakuu wa vyuo vikuu, viongozi wa VETA, wakuu wa vyuo vya ualimu, taasisi za maendeleo pamoja na wadau wengine wa elimu kutoka sekta za umma na binafsi.

“Huu ni mwendelezo wa jitihada za Serikali kujenga mfumo mmoja na shirikishi wa matumizi ya teknolojia za kidijitali kwenye elimu. Ushiriki wenu unaonesha dhamira ya dhati ya kuijenga Tanzania yenye elimu bora, jumuishi na inayoshindana kikanda na kimataifa,” amesema Prof Mushi.

Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Alex Sonna

Post A Comment: