📌Bilioni 7 kuwezesha maeneo 165 ya miji kupata huduma ya umeme Morogoro
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima ameipongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa utekekezaji wa miradi ya umeme maeneo ya Vijijini na Vitongoji hali iliyopelekea kuchochea uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.
RC Malima ametoa pongezi hizo leo Februari 26, 2026 mkoani humo wakati akizungumza na Bodi ya Nishati Vijijini (REB) pamona na Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ilipomtembelea ofisini kwake kueleza utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini inayoendelea na iliyokamilika mkoani humo.
"Nimeifahamu REA kwa mingi toka ilipoanzishwa rasmi. Hapa ilipofika leo hii lazima tujivunie sisi kama Watanzania kwa kuwa imeweza kufikisha umeme vijiji vyote na sasa utekekezaji unaendelea kwenye vitongoji vyote nchini," Amesema RC Malima.
Halikadhalika RC Malima ameipongeza Bodi ya REA na Menejimenti kwa kazi kubwa iliyofanyika kwa kusimamia miradi mbalimbali ya umeme katika mkoa huo ili Watanzania waweze kunufaika na nishati hiyo muhimu.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu ameeleza kuwa REA itaendelea kutekekeza miradi ya umeme vijijini wa weledi huku ikiwasimamia wakandarasi wa miradi hiyo ili waweze kuikamilisha miradi hiyo kwa wakati.
"Sisi kama Bodi tunauhakika miradi inayoendelea tutaikamilisha kwa wakati kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan tayari imetoa fedha nyingi ili kuwezesha na kukamilisha miradi hiyo, " Ameongeza Mhe. Balozi Kingu.
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa REA Mha. Hassan Saidy ameeleza kuwa kwa mkoa huo Wakala ipo mbioni kuongeza miradi ya ziada katika maeneo ya miji ambayo bado hayajafikiwa na huduma ya umeme ambapo takribani maeneo 165 yatapatiwa huduma hiyo na wateja wa awali 1,750 watapatiwa huduma ya umeme ambapo Serikali imetoa takribani shilingi bilioni 7 kwa mkoa wa Morogoro kutekeleza miradi hiyo.







Post A Comment: