Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga imeanza kutoa huduma ya upasuaji wa mifupa mirefu kwa wagonjwa wenye changamoto hiyo inayotolewa na Madaktari bingwa.

Akizungumza na waandishi wa habari mganga mfawidhi Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dkt. Luzila John amesema huduma hiyo imeanza kutolewa  tangu April 17 Mwaka huu 2023

Dkt. Luzila ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongonzwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku akisema tayari hospitali hiyo imepokea seti moja ya vifaa vyenye uwezo wa kuhudumia wagonjwa 28,  ambavyo ni ufadhiri kutoka hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma

"Vifaa hivi tulivyopata tumepata seti moja ambayo ina uwezo wa kuhudumia wagonjwa 28 kwa sasa hivi na kadri vifaa vitakavyokuwa vikitumika tutakuwa tunaomba vingine kwa ajili ya kuendeleza huduma hii ya upasuaji wa mifupa".

"Kupitia huduma hii tulipata madaktari bingwa wawili kutoka Hospitali ya Rufaa Dodoma ambao tumekuwa nao tangu Aprili 17,2023 mpaka leo kwa ajili ya kuona wagonjwa wenye shida au changamoto ya mifupa na wengine pia wamefanyiwa Operesheni lakini pia kuwajengea watumishi wenzetu wa Hospitali ya Rufaa Shinyanga kuwa na uwezo wa kufanya hizo Oparesheni za mifupa”. amesema Dkt. Luzila.

Mwakilishi kutoka Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dkt. Lusekelo William, ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga wenye uhitaji wa huduma hiyo, kufika katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ili kupata matibabu hayo

Daktari bingwa wa upasuaji, mkuu wa idara ya upasuaji Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dkt. Hamis Mpigahodi ambaye ni mtaalamu  wa upasuaji wa mifupa naye amesema wananchi wa Mkoa wa Shinyanga watanufaika na huduma ya upasuaji wa mifupa badala ya kutumia muda mwingi na gharama kusafiri kwenda Bugando jijini Mwanza kupata huduma hiyo.

Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Shinyanga waliopata matibabu hayo, wameishukuru serikali kuwasogezea huduma hiyo muhimu ambapo wamesema itasaidia kuondoa gharama ya kufuata huduma hiyo nje ya Mkoa wa Shinyanga.

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga imeanza  kutoa huduma mpya ya Upasuaji wa mifupa ambayo kwa muda mrefu wananchi wa Shinyanga wamekuwa wakihangaika wanapopata changamoto ya kuvunjika kwa mifupa na kulazimika kusafiri kwenda katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Jijini Mwanza.

Mganga mfawidhi Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dkt. Luzila John akizungumzia juu ya upatikanaji wa vifaa vya kufanyia upasuaji mifupa mirefu katika Hospitali hiyo ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Mganga mfawidhi Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dkt. Luzila John akizungumzia juu ya upatikanaji wa vifaa vya kufanyia upasuaji mifupa mirefu katika Hospitali hiyo ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.



Vifaa vya kufanyia upasuaji wa mifupa mirefu vilivyopo katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga

Mganga mfawidhi Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dkt. Luzila John upande wa kulia akipokea Vifaa vya kufanyia upasuaji wa mifupa mirefu leo April 21,2023

Mmoja wa wanufaika wa vifaa vya kufanyia upasuaji wa mifupa mirefu akiwa katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Mmoja wa wanufaika wa vifaa vya kufanyia upasuaji wa mifupa mirefu Bi. Sinzo Ongalla akiwa katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.


Mmoja wa wanufaika wa vifaa vya kufanyia upasuaji wa mifupa mirefu Bw. Lotih Nkango akiwa katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.


Share To:

Misalaba

Post A Comment: