Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Haruni Mapesa amempongeza Dkt. Rose Mbwete aliyekuwa Mkurugenzi wa kamapsi ya Karume –Zanzibar kwa kufanya kazi nzuri iliyozingatia kanuni, taratibu na miongozo ya utumishi wa umma kwa kipindi cha miaka saba (2018- 2025) akiwa Mkurugenzi wa kampasi ya karume Zanzibar.

Profesa mapesa ameyasema hayo leo wakati wa kikao kazi cha Menejimenti cha kumuaga Dkt. Mbwete na Kumkaribisha Mkurugenzi mpya Dkt. Sifuni Lusiru, ambapo pamoja na mambo mengine Dkt Mbwete amepongezwa kwa kujenga mahusiano mazuri kati ya Chuo na Taasisi nyingine za Serikali zilizopo Zanzibar, pia amekuwa mvumilivu , amejenga umoja na mshikamano miongoni mwa Wafanayakazi wa kampasi ya karume.

Prof. Mapesa amemsihi Mkurugenzi mpya Dkt. Lusiru kuhakikisha anayaendeleza  na kudumisha yale yote ambayo Dkt. Mbwete aliyasimamia kwa maslahi mapana ya Taasisi, ametakiwa pia kushirikisha Menejimenti ya Chuo na Watumishi anawaowasimia pale inapobidi.

Naibu Mkuu wa Chuo anaesimamia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Richard Kangalawe amesema kwa sasa Kampasi ya karume imekuwa huwezi kulinganisha na miaka ya nyuma kwa maana  kozi zinazofundishwa zimeongezeka, idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa imeongezeka, idadi ya wanafunzi wanaohitimu imeongezeka na  hata idadi ya Watumishi imeongezeka.

Kwa upande wa Naibu Mkuu wa Chuo, Mipango, Fedha na Utawala Prof. Evaristo Haulle amesema ni jambo la kufurahia pamoja kumpongeza Dkt. Mbwete kwa utumishi wake mwema, ulioleta tija kwa Taasisi hivyo kukutana pamoja na kumpongeza anaponaliza muda wake kunatoa fursa kwa viongozi wengine kufanya tafakuri ya kina ya namna bora ya kuendeleza Taasisi.

Dkt.Rose Mbwete Mkurugenzi aliyemaliza muda wake amekiri kuwa kufanikiwa kwake kutimiza majukumu ya taasisi ni pamoja na ushirikiano wa dhati aliupata kutoka kwenye bodi ya Chuo, Menejimenti na Watumishi aliokuwa anawasimami, hivyo anaamini kuwa ushirikiano ni jambo la muhimu, Uvumilivu, Hekima na kuzingatia Tamaduni za aneo husika.

Mbwete amesema changamoto zipo lakini lazima kuwe na namna bora ya kuzitatua. Kwa kuweka maslahi ya Taasisi mbele Umoja Ndiyo nguvu yetu na umoja ni ushindi.

Naye Dkt. Sifuni Lusiru ameahidi kuendeleza yale yote ambayo Dkt Mbwete aliyasimamia kwa mustakbali wa Taasisi, ameahidi kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni, taratibu, sheria na miongozo ya Utumishi wa umma.

Imetolewa na ;

Kitengo cha mawasiliano na Masoko

CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE

26.01.2026

Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post A Comment: