Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM Taifa Bwana Ramadhan Mlao leo ametoa msaada wa vyakula na vitu mbalimbali kwenye kituo cha watoto wenye mahitaji maalum shule ya msingi Buhangija jumuishi iliyopo Manispaa ya Shinyanga.

Vitu vilivyotolewa leo April 21,2023  ni pamoja na Mchele, Mafuta ya kupikia,Juice pamoja na  Mbuzi wawili.

Msaada huo umekabidhiwa na Katibu wa Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Raphael Nyandi huku akiwa ameongozana na viongozi wengine akiwemo katibu wa mbunge wa jimbo la Shinyanga Bwana Samwel Jackson, Mjumbe wa Baraza kuu UVCCM Taifa Monalisa Daniel pamoja na katibu wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini Faraji Katalambula.

Akizungumza katibu wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Raphael Nyandi amesema lengo la msaada huo ni kuhakikisha wanafunzi wa shule ya msingi Buhangija kesho April 22,2023 wanaungana na waumini wa Dini ya Kiislam  ulimwenguni kusherehekea sikukuu ya Eid El-Fitri.

Bwana Nyandi ametumia nafasi hiyo kuwasihi wanafunzi wa shule ya msingi Buhangija kusoma kwa bidii ili kufikia malengo waliyojiwekea.

Kwa upande wake mlezi wa wanafunzi wa shule ya msingi Buhakija Mwalimu Mashinde Daud ameshukuru kwa kupokea msaada huo ambao umetolewa na mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Bwana Ramadhan Mlao

Nao baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Buhangija wamemshukuru mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Bwana Ramadhan Mlao kwa kutoa msaada wa vyakula na vitu mbalimbali.

Katibu wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Raphael Nyandi akizungumza leo April 21,2023 katika hafla ya kukabidhi msaada wa vyakula na vitu mbalimbali vilivyotolewa na mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Bwana Ramadhan Mlao kwa wanafunzi katika kituo cha watoto wenye mahitaji maalum shule ya msingi Buhangija Manispaa ya Shinyanga.

Katibu wa mbunge wa jimbo la Shinyanga Bwana Samwel Jackson akizungumza leo April 21,2023 katika hafla ya kukabidhi msaada wa vyakula na vitu mbalimbali vilivyotolewa na mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Bwana Ramadhan Mlao kwa wanafunzi katika kituo cha watoto wenye mahitaji maalum shule ya msingi Buhangija Manispaa ya Shinyanga.

Mjumbe wa Baraza kuu UVCCM Taifa Monalisa Daniel akizungumza leo April 21,2023 katika hafla ya kukabidhi msaada wa vyakula na vitu mbalimbali vilivyotolewa na mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Bwana Ramadhan Mlao kwa wanafunzi katika kituo cha watoto wenye mahitaji maalum shule ya msingi Buhangija Manispaa ya Shinyanga.

Katibu wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini Faraji Katalambula akizungumza leo April 21,2023 katika hafla ya kukabidhi msaada wa vyakula na vitu mbalimbali vilivyotolewa na mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Bwana Ramadhan Mlao kwa wanafunzi katika kituo cha watoto wenye mahitaji maalum shule ya msingi Buhangija Manispaa ya Shinyanga.

Katibu wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Raphael Nyandi akizungumza na mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Bwana Ramadhan Mlao kwa njia ya simu kabla ya kukabidhi msaada kwa wanafunzi katika kituo cha watoto wenye mahitaji maalum shule ya msingi Buhangija Manispaa ya Shinyanga.

Katibu wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Raphael Nyandi akiongoza zoezi la kukabidhi msaada kwa wanafunzi wa shule ya msingi Buhangija ambapo msaada huo umetolewa na mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Bwana Ramadhan Mlao kwa ajilia ya kusherehekea sikukuu ya Eid El-Fitri.

Katibu wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Raphael Nyandi upande wa kulia akiongoza zoezi la kukabidhi msaada huo kwa wanafunzi wa shule ya msingi Buhangija ambapo msaada huo umetolewa na mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Bwana Ramadhan Mlao kwa ajilia ya kusherehekea sikukuu ya Eid El-Fitri.

Share To:

Misalaba

Post A Comment: