Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Dkt Amandus Chinguile akifurahia jambo baada kusikia kuwa Wananchi wameaandaa sherehe ya kumpongeza kwa kutatua changamoto zao


Na Fredy Mgunda, Nachingwea


WANANCHI wa Kijiji cha Mchangani kata ya Stesheni Jimbo la Nachingwea mkoani Lindi wameandaa sherehe kwa ajili ya kumpongeza mbunge wa Jimbo hilo Dkt Chinguile kutokana na kutatua changamoto za maji,elimu, barabara na afya.

Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa mbunge huyo,wananchi walisema kuwa walikuwa wanateseka na tatizo la maji kwa miaka mingi lakini alipoingia mbunge huyo wamepata maji na wanafuraha zote za kumpongeza mbunge.

Wananchi walisema kuwa wanampongeza sambunge wa Jimbo la Nachingwea Dkt Amandus Chinguile kwa jitihada za kutatua changamoto za wananchi waliompa kura.

Walisema kuwa walikuwa wanatatizo kubwa la kukosa maji Safi na salama katika Kijiji hicho na kupeleka kuamka usiku kwenda kutafuta maji umbali mrefu na kufifisha shughuli za kimaendeleo kupeleka migogoro ya ndoa ila kwa sasa ardha hiyo haipo na Wananchi wote wanafuraha.

Aidha Wananchi hao walisema kabla ya kutatua changamoto ya barabara kulikuwa hakuna gari lolote lilokuwa linafaika Kijiji cha Mchangani kata ya Stesheni.

Aidha wananchi hao walisema kuwa kujengwa kwa zahanati ya Kijiji cha Mchangani kumesaidia wananchi kupata huduma kwa karibu na kuwapunguzia gharama za wananchi kuifuata huduma hiyo mbali.

Walisema kuwa bado wanachangamoto nyingi ila kwa alichokifanya mbunge Dkt Amandus Chinguile wanaandaa siku maalumu ya kufanya sherehe ya kumpongeza mbunge huyo kwa kazi za kimaendeleo anazozifanya jimboni hapo.


Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: