Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo,akizungumza  na Wajumbe wa  Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kisarawe,kikao kilicholenga kuwashukuru wajumbe kwa mchango wao katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuwashukuru kwa kuchaguliwa tena kuwa Mbunge wa jimbo hilo.

Na.Alex Sonna-KISARAWE

MBUNGE wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo, amewaomba wananchi wa Kisarawe na watanzania kwa ujumla kumuombea Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa ana maono makubwa ya kuwatumikia Watanzania na kulisukuma Taifa mbele kimaendeleo.

Dkt. Jafo ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza katika kikao maalum cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kisarawe, kilicholenga kuwashukuru wajumbe kwa mchango wao katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuwashukuru kwa kuchaguliwa tena kuwa Mbunge wa jimbo hilo.

“Niwaombe wajumbe wa Halmashauri Kuu kuhakikisha tunamuombea Rais Dkt. Samia kwa kuwa ana kazi kubwa ya kuwaletea maendeleo Watanzania na kuhakikisha Taifa letu linaendelea kusonga mbele,” amesema Dkt.Jafo

Ameongeza kuwa amani na usalama ni nguzo muhimu za maendeleo ya kiuchumi, hivyo ni wajibu wa kila Mtanzania kumuombea Rais na Taifa kwa ujumla.

“Bila amani na usalama, nchi yetu haiwezi kupata mafanikio ya kiuchumi. Nawaomba wananchi wa Kisarawe na Watanzania kwa ujumla tuendelee kumuombea Rais wetu na Taifa letu, kwa sababu kiongozi wetu mwenye maono ni Rais Samia, na lazima tumuombee ili nchi yetu iendelee kusonga mbele,” amesema Dkt. Jafo

Awali, amesema baada ya ushindi huo, chama na serikali vimeanza rasmi awamu mpya ya kazi kwa kipindi cha miaka 5, huku akiendelea na utekelezaji wa majukumu ya maendeleo jimboni kupitia mkakati wao wa ‘Chaka kwa chaka’.

“Tumeanza kazi kwa mara nyingine katika msimu wa 2025–2030. Tumeendelea na kazi za jimboni, tukikutana na viongozi wa kada mbalimbali wakiwemo viongozi wa kisiasa, watendaji wa halmashauri, madiwani pamoja na wenyeviti wa vijiji na vitongoji vya Wilaya ya Kisarawe,” amesema Dkt. Jafo.

Ameeleza kuwa kikao hicho na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ni cha muhimu sana kwa kuwa ni timu inayobeba jukumu la kuimarisha uhai wa chama pamoja na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Aidha, Dkt. Jafo ametumia mkutano huo kueleza mikakati ya maendeleo ndani ya Wilaya ya Kisarawe, ikiwemo kuboresha sekta za afya, elimu, barabara, maji, umeme pamoja na ujenzi wa viwanda vya kati na vikubwa kwa lengo la kuongeza thamani ya mazao na kutoa ajira kwa vijana.

“Wilaya ya Kisarawe ipo na mtazamo mpya wa maendeleo, kuhakikisha tunasonga mbele kwa kasi zaidi katika kuboresha maisha ya wananchi,” amesema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kisarawe, Khalfan Sika, amesema jukumu la wanachama wa CCM ni kuipa ushirikiano Serikali ili kuhakikisha Ilani ya Uchaguzi inatekelezwa kikamilifu.

“Ilani tuliyowapa Mhe. Rais, Mbunge na Madiwani ni Ilani ya CCM. Utekelezaji wake ndio mafanikio na suluhisho la kero za wananchi. Huu ni mkataba kati ya wananchi na CCM,” amesema.

Ameongeza kuwa Ilani hiyo ni maelekezo ya chama ambayo Serikali imepewa dhamana ya kuyatekeleza kwa vitendo, huku akimpongeza Rais Samia na Mbunge Jafo kwa maono makubwa waliyonayo ya kuwaletea maendeleo wananchi.

Kadhalika, Mwenyekiti huyo amempongeza Dkt. Jafo kwa uungwana wake wa kukutana na Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya mara baada ya kumalizika kwa shughuli za uchaguzi.

“Mara nyingi baada ya uchaguzi, watu waliobeba mzigo mkubwa wa kampeni hawakumbukwi kushukuriwa. Nimpongeze sana Mbunge Jafo kwa kuona umuhimu wa kukutana na wajumbe hawa na kuwashukuru,” amesema.

Amefafanua kuwa katika Wilaya ya Kisarawe, kampeni zilifanyika katika vijiji vyote 84 na mikutano 105 ilifanyika katika ngazi ya vijiji na vitongoji, kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanaielewa Ilani ya CCM na sababu za kuchagua chama hicho.

Amesema katika matokeo ya uchaguzi, Rais Samia alipata ushindi wa asilimia 98 huku Mbunge Jafo akipata asilimia 95, hali inayoonesha imani kubwa ya wananchi wa Kisarawe kwa viongozi wao na Chama Cha Mapinduzi.

“Jukumu letu sasa ni kusimamia utekelezaji wa Ilani, kwa sababu uchaguzi mwingine utafanyika mwaka 2030, na wananchi watataka kuona ni kwa kiasi gani tumetekeleza ahadi tulizotoa,” amesema.

Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo,akiwasili katika ukumbi  kwa ajili ya kuzungumza na Wajumbe wa  Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kisarawe kikao kilicholenga kuwashukuru wajumbe kwa mchango wao katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuwashukuru kwa kuchaguliwa tena kuwa Mbunge wa jimbo hilo.

Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo,akizungumza  na Wajumbe wa  Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kisarawe,kikao kilicholenga kuwashukuru wajumbe kwa mchango wao katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuwashukuru kwa kuchaguliwa tena kuwa Mbunge wa jimbo hilo.

Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo,akizungumza  na Wajumbe wa  Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kisarawe,kikao kilicholenga kuwashukuru wajumbe kwa mchango wao katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuwashukuru kwa kuchaguliwa tena kuwa Mbunge wa jimbo hilo.

Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo,akizungumza  na Wajumbe wa  Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kisarawe,kikao kilicholenga kuwashukuru wajumbe kwa mchango wao katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuwashukuru kwa kuchaguliwa tena kuwa Mbunge wa jimbo hilo.

Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo,akizungumza  na Wajumbe wa  Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kisarawe,kikao kilicholenga kuwashukuru wajumbe kwa mchango wao katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuwashukuru kwa kuchaguliwa tena kuwa Mbunge wa jimbo hilo.

Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo,akizungumza  na Wajumbe wa  Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kisarawe,kikao kilicholenga kuwashukuru wajumbe kwa mchango wao katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuwashukuru kwa kuchaguliwa tena kuwa Mbunge wa jimbo hilo.

Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo,akizungumza  na Wajumbe wa  Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kisarawe,kikao kilicholenga kuwashukuru wajumbe kwa mchango wao katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuwashukuru kwa kuchaguliwa tena kuwa Mbunge wa jimbo hilo.

Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo akimsikiliza Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kisarawe Khalfan Sika,wakati ,akizungumza   na Wajumbe wa  Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kisarawe,kikao kilicholenga kuwashukuru wajumbe kwa mchango wao katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuwashukuru kwa kuchaguliwa tena kuwa Mbunge wa jimbo hilo.

Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo akimsikiliza Katibu  wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kisarawe Bi.Josephine Mwanga wakati akizungumza  na Wajumbe wa  Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kisarawe,kikao kilicholenga kuwashukuru wajumbe kwa mchango wao katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuwashukuru kwa kuchaguliwa tena kuwa Mbunge wa jimbo hilo.

Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo akimsikiliza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kisarawe, Aidan Kitare wakati akizungumza  na Wajumbe wa  Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kisarawe,kikao kilicholenga kuwashukuru wajumbe kwa mchango wao katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuwashukuru kwa kuchaguliwa tena kuwa Mbunge wa jimbo hilo.

Wajumbe wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo (hayupo pichani) wakati,akizungumza  na Wajumbe wa  Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kisarawe,kikao kilicholenga kuwashukuru wajumbe kwa mchango wao katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuwashukuru kwa kuchaguliwa tena kuwa Mbunge wa jimbo hilo.

Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo,akiwa katika picha ya pamoja  Wajumbe wa  Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kisarawe,mara baada ya kuzungumza nao kikao  kilicholenga kuwashukuru wajumbe kwa mchango wao katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuwashukuru kwa kuchaguliwa tena kuwa Mbunge wa jimbo hilo.

Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Alex Sonna

Post A Comment: