Mchezaji wa timu ya mamlaka ya mapato Tanzania 'TRA' kushoto akiwania mpira dhidi ya mchezaji wa chuo kikuu cha Dar es salaam 'UDSM' wakati wa mchezo wao wa nusu fainali uliochezwa juzi katika uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga ambapo TRA walishinda kwa vikapu 51-45 na kufanikiwa kuingia fainali ya Shimuta.
Kikosi cha timu ya mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania 'TPA' kitakachocheza fainali za SHIMUTA mwaka 2022 dhidi ya mamlaka ya mapato Tanzania 'TRA'.
Na Denis Chambi, Tanga.
Kesho November 27, 2022 inasubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi, mashabiki na
wadau wa mchezo wa mpira wa kikapu wakitaka kushuhudia ni nani mbabe
atakayeibuka bingwa wa mchezo huo kati ya timu ya mamlaka ya usimamizi
wa Bandari Tanzania 'TPA' dhidi ya mamlaka ya mapato Tanzania 'TRA'
zilizofanikiwa kutinga hatua ya fainali ya mchezo huo kwenye mashindano
ya Shimuta mwaka huu.
Timu
ya mamlaka ya mapato Tanzania TRA ilifanikiwa kukata tiketi ya kucheza
fainali hizo baada ya kuwafunga mahasimu wa shirika la umeme
Tanzania 'TANESCO' kwa vikapu 51-45 huku Bandari wao wakiwatembezea
kipigo wapinzani wao chuo kikuu cha Dar es salaam 'UDSM' kwa kuwafunga
vikapu 71 -53 katika hatua ya nusu fainali mechi zote zikichezwa
katika uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga.
Akizungumza
mara baada ya kutinga hatua ya fainali katibu wa michezo kutoka TRA
Kamna Shomari alisema kuwa mwaka huu wana jambo lao ambalo lazima
walitimize hususani katika mchezo wa mpira wa kikapu wakipanga
kutawadhwa kuwa mabingwa kwa mwaka huu wa 2022.
"Mwaka
huu tumekuja na adhima moja tu ya kuhakikiaha kwamba linakufa jitu na
tunachukuwa hili kombe la Basketball mpaka sasa hivi sisi hatuhesabu
kwamba haya ni mafanikio sisi malengo yetu makubwa ni kuchukuwa ubingwa
wala hatuna jambo lingine lolote" alisema
Shomari
alikiri wazi kuwa haikuwa rahisi kwao kuwafunga Tanesco kwenye mchezo
wa wa nusu fainali ambao wana uzoefu na historia nzuri kwenye shimuta
hii ikionyesha kuwa upinzani ulikuwa ni mkubwa kutoka kwao lakini uimara
wa kikosi chake uliweza kuamua matokeo na kuibuka washindi huku
wakifurahia kuwafunga vigogo wa kundi lao wakiwemo UDSM.
"Upinzani
ulikuwa ni mkali Tanesco wenzetu wanahistoria nzuri kwenye michezo
hii , ukiangalia wametupa upinzani mkubwa lakini mwishoni wa mchezo
kwa sababu sisi ni bora tukaweza kufanikiwa kuwafunga" alisema Shomari
Aidha
alilipongeza shirikisho linalo simamia michezo hiyo maarufu kama
Shimuta kwa kuwaletea mashindano hayo kila mwaka ambapo mbali na
kukutana na upinzani kwenye michezo umewajengea ukaribu ushirikiano
baina yao wafanyakazi wa taasiai mashirika na makampuni mbalimbali
yanayoshiriki michuano hiyo.
"Kwa
ujumla tunawapongeza waandaaji halmashauri kuu ya shimuta kwa
kusimamia na kuongoza michezo yote ambayo inahusisha taasisi 52 sio
jambo rahisi hata kidogo, tunaomba michezo hii iendelee kuwepo na
kuboreshwa zaidi ina manufaa makubwa kwetu mbali na kutukutanisha
kimichezo lakini imekuwa ni sehemu yetu wafanyakazi kubadilishana mawazo
kujenga na kuimarisha mahusiano baina ya taasisi na taasisi" alisema
katibu huyo.
Mashindano
hayo ya Shimuta yanayofanyika kitaifa mkoani Tanga kwa mara ya pili
mfululizo yalinza kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali tangu
November 15 yakibebwa na kauli mbiu ya mwaka huu 'Shimuta Familiya moja'
na yanatarajiwa kufungwa rasmi November 29 , 2022.
Post A Comment: