Meneja wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa Tanga Specioza Owure akimkabidhi dawa mmoja wa wagonjwa wanaohitaji msaada wa kufanyiwa opareshini katika Hospitali ya Rufaa wa mkoa wa Tanga Bombo wakati walipotembelea kuwaona ikiwa ni wiki maalum ya kuwashukuru walipa Kodi wa mkoa huo.

Meneja wa TRA mkoa wa Tanga Specioza Owure akimkabidhi kaimu Mganga mfawidhi wa hospital ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo,  Orpar Msuya baadhi ya vifaa na dawa walizojitolewa kwajili ya  kuwasaidia wagonjwa wanaohudumiwa katika hospital hiyo.

 
 Meneja wa TRA mkoa wa Tanga (kulia) Specioza Owure akikabidhi miongoni mwa vifaa walivyojitolea kuwasaidia   wazazi wa watoto  wenye matatizo mbalimbali wanaohudumiwa katika hospital ya Bombo

Na Denis Chambi, Tanga.

Katika kuendelea kusherehekea kipindi hiki cha kutoa shukrani kwa walipa kodi mamlaka ya Mapato Tanzania TRA mkoa wa Tanga imechangia vifaa mbalimbali matibabu ikiwemo dawa na matumizi mengine vyenye thamani ya shilingi Million tatu na laki tano (3, 500, 000) kwa ajili ya wagonjwa waliopo katika hospital ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo. 

 Akizungumza mara mara baada ya kutembelea wodi ya watoto pamoja na wagonjwa wengine meneja wa mamlaka ya mapato Tanzania 'TRA' mkoa wa Tanga Specioza Owure amesema kuwa wamejipanga kuwakatia bima ya afya watoto wanaopatiwa matibabu katika hospitali hiyo hii ikiwa ni njia ya kuwapunguzia gharama za matibabu wanazotumia wazazi katika kipindi chote wanapokuwa wakipatiwa huduma. 

 "Tunaamini kabisa kwamba tunaishi na jamii ambayo haipo kwenye kisiwa , na jamii ikiwa imara na afya bora hata na kodi yetu inaongezeka kwa sababu jamii ikiwa na afya imara ndio tunapata nguvu za kuweza kufanya biashara na kulipa kodi stahiki"

 "Tumetembelea wodi ya watoto kuwaona na kujua matatizo yao, tuna lengo la kuwakatia bima ya afya kwa sababu tunaona kuna watoto wengi wanahitaji bima kwa kuanzia tunategemea tutawakatia bima watoto wasiopungua 25 na baadaye tutaongeza pia" alisema Owure.

 "Lakini pia tumetembelea wagonjwa wawili ambao wamehitaji msaada wa fedha kwaajili ya kufanyiwa oparesheni na tumekubali kwamba tutatoa hicho kiasi chote ambacho kinatakiwa kwaajili ya wote kufanyiwa oparesheni". aliongeza meneja huyo. 

 Hayo yanafanywa na mamlaka ya mapato Tanzania mkoa wa Tanga 'TRA' kama ishara ya kusherehekea ushindi walioupata kwa kuvuka lengo la makusanyo ya kodi ambapo itakumbukwa kuwa kwa mwaka wa fedha uliopita 2021/2022 Tanga waliibuka vinara na kuongoza mikoa yote ya Tanzania bara katika ukusanyaji wa mapato ambapo waliwekewa lengo la kukusanya shilingi Billioni 169.68 na hatimaye kuvuka lengo wakifanikiwa kukusanya Billioni 207.52 sawa na asilimia 121.6%. 

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo kaimu mganga mfawidhi katika hospitali ya rufaa mkoa wa Tanga Bombo Orpar Msuya aliwapongeza na kuwashukuru mamlaka ya mapato 'TRA' mkoa wa Tanga kwa kuguswa na kuona ipo haja ya kusaidia baadhi ya wagonjwa wanaopatiwa matibabu ambao wameshindwa kulipa gharama kutokana na sababu mbalimbali.

 "Nashukuru sana kwa kupokea msaada huu kwaajili ya wenzetu ambao wana uhitaji asanteni sana Mungu awabariki tunaomba msiishie hapa tuna mahitaji mengi watu wanahitaji basi mkiwa na chochote mnakaribishwa kujitolea" alisema Orpar. 

Baadhi ya wazazi wenye watoto waliosaidiwa msaada huo akiwemo Zaituni Zuberi na Munila Binuru wameishukuru TRA na kuendelea kuiomba jamii kuwashika mkono kwa hali na mali katika kuhakikisha wanamudu gharama za matibabu kwa watoto wao wanaoendelea kupatiwa huduma katika hospital hiyo.

 "Nimemleta mtoto mgonjwa ambaye ni mlemavu sio wakubebwa mgongoni ni wakupakatwa tu muda wote kwahiyo nashukuru sana kwa msaada huu mliotukumbuka na pia tunazidi kuhitaji msaada wenu maana wengine hali yetu ya uwezo wa kifedha ni ngumu mtusaidie mtushike mkono kwa kila kitu" alisema Zaituni" 


Share To:

Post A Comment: