Spika wa Bunge la Kenya Moses Wetangula akishangilia goli la kufutia machozi la Kenya


WENYEJI Sudan Kusini wameanza vizuri katika Michezo ya 12 ya Mabunge ya Afrika Mashariki baada ya kushinda katika mchezo wa netball na soka.


Katika soka Sudan Kusini wamewaangushia kipigo Cha mabao 3-1 Bunge la Kenya, wakati katika Netball wamewalaza Bunge la Tanzania Kwa magoli 29-25.

 katika Soka Bunge la Africa Mashariki watavaana na Bunge la Uganda wakati Bunge la Tanzania watavaana na Bunge la Burundi saa 10 jioni Kwa masaa ya hapa Juba ambayo ni sawa na saa 11 nyumbani Tanzania.


Jumapili itakuwa ni maalum Kwa ajili ya mchezo wa Riadha.


Share To:

Post A Comment: