Katibu wa michezo kutoka Shirika la viwango Tanzania 'TBS' Nyabuchwenza Mitisela akizungumza  na waandishi wa habari mara baada ya timu yao ya mpira wa miguu kufanikiwa  kuingia hatua ya nusu fainali kwenye  mashindano ya SHIMUTA yanayoendelea mkoani Tanga.
     Mlinda mlango wa kikosi cha TBS Lukas Gula.
 

Na Denis Chambi Tanga.

SHIRIKA la viwango Tanzania TBS  kupitia timu yake  ya mpira wa miguu limefanikiwa kuingia  hatua ya  nusu fainali kwenye  mashindano ya Shimuta yanayoendelea mkoani  Tanga baada ya kuwatapa nje wapinzani wao   mamlaka ya usimamizi wa wanayama pori Tanzania 'TAWA' kwa mikwaju ya penati 5-4 mchezo uliochezwa november 25, 2022  kwenywe dimba la Popatlal jijini Tanga.

Mchezo huo ulilazimika kuamuliwa kwa mikwaju ya penati baada ya timu zote mbili kumaliza mchezo wakitoshana nguvu ya goli 1-1 wakitangulia kupachika bao TAWA  mapema kabisa kunako dakika ya 3  ya mchezo huku TBS nao wakisawazisha kwenye dakika ya 16 ya kipindi cha kwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ushindi huo Katibu wa michezo kutoka Shirika la viwango Tanzania 'TBS' Nyabuchwenza Mitisela alisema kuwa  kila hatua waliyokuwa wakipiga mpaka hapo walipofikia ilikuwa ni katika harakati za kutaka kutimiza malengo na matarajio  walioelekezwa na viongozi wao ya kuvuka  robo fainali ambapo waliweza kufanikisha na kupiga hatua zaidi.

"Mwaka jana tuliishia robo fainali kwahiyo mwaka huu tukawa tumejiwekea malengo  kuwa ni lazima tufike nusu fainali tunashukuru Mungu malengo yetu yametimia na tunafurahi wachezaji wetu wamejituma uwanjani na wamecheza  vizuri tunawapongeza sana" alisema

Katibu huyo  amewaomba mashabiki wao kuendelea kuwaombea kunako hatua ya nusu fainali ikiwa ni pamoja na kuwatia motisha wachezaji huku akiwaahidi kuipeleka timu hiyo kucheza fainali na hatimaye kuibuka mabingwa wa mchezo huo kwa mwaka 2022.

"Nilikuwa naiona robo fainali ni ngumu zaidi lakini niwaahidi tu wapenzi na mashabiki wa timu yetu ya TBS  kuwa tunaamini  tutavuka nusu fainali na Mungu akipenda kwenda kucheza fainali na kuibuka washindi" alisema Mitisela.

Mlinda mlango wa kikosi cha TBS Lukas Gula ambaye aliibuka kuwa shujaa wa mchezo huo akiokoa mchomo mmoja wa penati na yeye kucheka na nyavu mara moja alisema  mwaka huu kwenye shimuta walijiuliza ni wapi walikosea mwaka jana kulikowapelekea kuishia hatua ya robo fainali hivyo mwaka huu kuja na mpango kazi kabambe wa kupiga hatua zaidi ambapo walifanikiwa na sasa wakiwa wanaichungulia fainali.

"Siri ya ushindi wa leo ni maandalizi mazuri na malengo ambayo tulijiwekea  katika michezo ya mwaka jana TBS ni miongoni mwa timu ambazo ziliingia robo fainali lakini tuliondolewa kwa hatua ya matuta na TPDC , tulivyokuja mwaka huu tulijiandaa vizuri  sana licha ya kwamba tulicheza pungufu lakini tulifanikiwa kuhimili mchezo na kuwashinda wapinzani wetu " alisema Gula.

"Timu yetu imeonyesha timu nyingine kuwa sisi ni watu wa viwango na tulijiwekea viwango mwaka huu kuwa lazima tufike fainali na tumefikia katika malengo yetu kwahiyo ni funzo kwa timu nyingine ninaamini kwatika hatua inayofuata na michezo mingine inayokuja kila mtu anaiogopa TBS kwa sababu ni timu ambayo imejiweka katika viwango fulani" aliongeza nyanda huyo.

Mashindano hayo  yaliyoanza kutimua vumbi November 15 yanahusisha  timu za  watumishi kutoka mashirika ya umma ,  taasisi binafsi na makampuni 52 kote nchini na yanatarajiwa kutamatika November 29 mwaka huu kwa fainali za michezo kucheza ikiwemo  mpira wa miguu,  Kikapu,  Wavu,  Pete ,   pamoja na michezo ya jadi ikiwemo Draft,  Dats  riadha huku yakuliongozwa na kaulivmbiu ya 'Shimuta Familiya moja' .  
Share To:

Post A Comment: