Na John Walter-Babati

Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Daniel Sillo  ametoa mabati 600 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa miradi ya elimu na afya jimboni humo.

Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika leo agosti 26,2022 katika ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Babati ikiwa ni mkakati wa Mbunge huyo (CCM)  kusaidia kukamilisha miradi ya afya na elimu  inayoendelea kujengwa wilayani hapo.

Mbunge huyo ametoa mabati hayo kwa mgawanyo katika vijiji sita vya Tsamas (150), ,Secheda (117),Boay (84),Kisangaji (29),Datar (110) na Yorotonik (110).

Amewataka madiwani na watendaji wengine kusimamia bati hizo zikatumike kwenye miradi iliyokusudiwa.

Aidha ameishukuru benki ya NMB kwa msaada huo walioutoa ambao umetokana na mahusiano mazuri waliyonayo yeye na benki hiyo. 

Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Babati imempongeza Mbunge Sillo kwa jitihada za kuwaletea wananchi maendeleo kama inavyoelekeza ilani ya chama cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza kwa niaba ya madiwani, diwani wa kata ya Ufana Bernad Bajuta amesema mabati hayo yatasaidia sana kumaliza miradi ya elimu na afya iliyokwama kwa muda mrefu.

Mbunge wa Babati vijijini mheshimiwa Daniel Sillo akimkabidhi diwani wa Ufana Mabati kwa ajili ya kumalizia miradi ya afya na elimu katika kata hiyo.

Mbunge wa Babati Vijijini Mheshimiwa Daniel Sillo akimkabidhi mabati diwani wa kata ya Boay kwa ajili ya kukamilisha miradi ya maendeleo katika kata hiyo kwenye afya na elimu,Mabati hayo yametolewa na mbunge huyo kwa msaada wa benki ya NMB.

Mbunge wa Babati Vijijini Mheshimiwa Daniel Sillo akimkabidhi mabati diwani wa kata ya Qash kwa ajili ya kukamilisha miradi ya maendeleo katika kata hiyo kwenye afya na elimu,Mabati hayo yametolewa na mbunge huyo kwa msaada wa benki ya NMB.






Share To:

Post A Comment: