Na OWM - TAMISEMI, Bahi

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, amesema Mhe. Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amemuarifu kuwa, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la wananchi wa Kata ya Chifutika lililowasilishwa na Mbunge wa Jimbo la Bahi Mhe. Kenneth Nollo la kupatiwa shilingi milioni 544 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Chifutuka ambayo itakidhi uhitaji wa wananchi wa kata hiyo. 

Prof. Shemdoe amesema hayo leo Aprili 17, 2026 wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa darasa la nne, darasa la saba, kidato cha pili na kidato cha nne wilayani Bahi, iliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Chiona wilayani humo. 

“Mhe. Mbunge alinifuata kabla sijasimama kuzungumza, akiomba shule ya sekondari ijengwe Kata ya Chifutika, nikawasiliana na Mhe. Waziri Mkuu na kuliwasilisha ombi hilo kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ameridhia milioni 544 ziletwe kujenga shule ya sekondari,” amesema Prof. Shemdoe.

Kutokana na kuridhiwa kwa kiasi hicho cha fedha, Prof. Shemdoe kwa niamba ya wananchi wa Kata ya Chifutuka Wilayani Bayi amemshukuru kwa moyo wa dhati Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mhe. Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchema kwa upendo mkubwa waliouonesha kwa wananchi wa Kata hiyo Chifutuka.

Prof. Shemdoe amefafanua kuwa, fedha hizo zimeridhwa na Mheshimiwa Rais kwasababu lengo la Serikali ni kuendelea kuimarisha elimu nchini, ikizingatiwa kuwa Bahi imeonesha juhudi kubwa na kuwa Halmashauri ya kwanza kitaifa kwenye ufaulu wa mitihani ya darasa la saba kwa mwaka 2025.









Share To:

Post A Comment: