Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameweka jiwe la msingi na kupanda mti katika Skuli ya Sekondari ya Ufundi Kizimkazi Mkunguni, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja.
Hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali za kutekeleza miradi ya Muungano, ukiwemo ujenzi wa skuli hiyo unaotekelezwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar (WEMA).
Skuli hiyo inatarajiwa kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia, pamoja na kuwawezesha wanafunzi kupata maarifa na ujuzi wa ufundi utakaowaandaa kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya Taifa.
Mradi huo pia, unalenga kuimarisha upatikanaji wa elimu ya ufundi na kukuza ujuzi miongoni mwa vijana hatua inayotarajiwa kuongeza fursa za ajira na kuwaandaa kushiriki katika shughuli za kiuchumi na kijamii.









Post A Comment: