Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) leo, Agosti 11, 2026, imeendelea na vikao vyake kwa kupitia na kuchambua taarifa za hesabu zilizokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) za Manispaa ya Shinyanga, Halmashauri za Wilaya za Kishapu na Msalala.

Uchambuzi huo ni sehemu ya utekelezaji wa ratiba ya Kamati katika kufuatilia usimamizi wa rasilimali za umma katika Serikali za Mitaa na kuimarisha mifumo ya uwajibikaji, kuhakikisha wananchi wanapata huduma zinazoendana na thamani ya rasilimali zinazotengwa kwa ajili ya maendeleo yao.









Share To:

Post A Comment: