Na John Walter-Babati

Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Babati Abdulrahmani Kololi ameiagiza Halmashauri hiyo kuwaondoa mbwa wanaozagaa mtaani ovyo kwa kuwaua.

Amesema amepokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuwa mbwa hao wamekuwa kero na wakati mwingine kung'ata watu hali inayowapa hofu.

Akizungumza katika baraza la madiwani,Kololi amesema mitaa inayoongoza kwa kuwa na mbwa wengi wanaozurura ni mjini Babati na Bagara.

Mwaka 2017 Jumla ya Mbwa 347 kati ya zaidi ya 3600 wanaozurura mitaani katika mji wa Babati waliuawa kwa kupigwa risasi na Idara ya mifugo ya Halmashauri hiyo.
Share To:

Post A Comment: