Mkuu wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo  kushoto akipokea wakati msaada wa vifaa vya ujenzi na vifaa tiba kwa baadhi ya taasisi na shule zilizopo jirani na shamba hilo vyenye thamani ya zaidi ya Milioni 10, kutoka kwa Mkuu wa hifadhi wa shamba la miti Lunguza Ellyneema Mwasalanga
Mkuu wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo  kushoto akipokea wakati msaada wa vifaa vya ujenzi na vifaa tiba kwa baadhi ya taasisi na shule zilizopo jirani na shamba hilo vyenye thamani ya zaidi ya Milioni 10, kutoka kwa Mkuu wa hifadhi wa shamba la miti Lunguza Ellyneema Mwasalanga
Mkuu wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo  kulia akiwa na  Mkuu wa hifadhi wa shamba la miti Lunguza Ellyneema Mwasalanga katikati wakikabidhi msaada huo
MKUU wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo katika akiwa na 
Mkuu wa hifadhi wa shamba la miti Lunguza Ellyneema Mwasalanga kulia wakiwa kwenye madawati hayo mara baada ya kukabidhi

Na Oscar Assenga,Muheza

SERIKALI wilayani Muheza Mkoani Tanga imepiga marufuku shughuli za kibinadamu ikiwemo ukataji wa miti katika maeneo ya Hifadhi ya Msitu wa Miti wa Lunguza huku ikieleza haitasita kuwachukulia hatua watakaokaidi.

 

Marufuku hiyo ilitangazwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo  wakati akipokea msaada wa vifaa vya ujenzi na vifaa tiba kwa baadhi ya taasisi na shule zilizopo jirani na shamba hilo vyenye thamani ya zaidi ya Milioni 10.

 

Akitangaza mkakati huo baada ya kupokea vifaa hivyo alisema kuwa ukataji miti hovyo, uchimbaji wa madini ikiwemo na uchomaji misitu vinasababisha madhara ya kimazingira ikiwemo uhaba wa mvua,hivyo ni muhimu Wananchi wakahifadhi mazingira ya msitu huo .

 

Aliwataka wananchi wanaoishi jirani na msitu huu kushirikiana katika kuhakikisha kunakuwa na usimamizi na matumizi endelevu ya raslimali za misitu ili uweze kuwa endelevu  ikiwemo waweze kunufaika na msitu huu

 

Awali Mkuu wa hifadhi wa shamba la miti Lunguza Ellyneema Mwasalanga  amesema kuwa wametoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya kurudisha Kwa jamii katika kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo

 

Alisema kwamba wameweza kutoa msaada wa saruji mifuko 240,viti na meza 40,vifaa tiba 12 vyenye thamani ya sh Mil 2.5 kwa ajili ya zahanati ya kwafungo ambavyo vyote vina thamani ya sh Mil 10.1.

 

Alisema faida nyengine ambazo wanazipata wananchi ni kilimo mseto (taungya) ambapo wananchi huruhusiwa kulima katika maeneo yaliyo andaliwa kwa ajili ya kupandwa au yaliyopandwa yenye miti midogo kwa utaratibu maalumu.

 

Aidha alisema sambamba na hayo wananchi wananufaika na malighafi za kujengea (nguzo,fito) ajira katika maeneo mbalimbali ikiwemo kazi za kuhudumia shamba,uvunaji ,usafirishaji, uchakataji wa malighafi viwandani na kukua kwa biashara mbalimbali katika maeneo ya Muheza.

 

 

 

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: