Na John Walter-Manyara.

Mku wa mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere amewatahadharisha wanaocheza michezo ya kubahatisha kuwa  wasitumie michezo hiyo kama sehemu ya kazi kwao.

Ametoa rai hiyo akizungumza wakati wa  semina ya Bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini (GBT) ikieleza majukumu yake kwa kamati ya ulinzi na Usalama ya mkoa huo. 

Aidha Nyerere amewataka wanaocheza Mchezo huo kuzingatia taratibu zilizowekwa na bodi hiyo.

Mkurugenzi wa huduma za bodi Ole Sumoyan Daniel amesema Bodi ya michezo ya kubashiri Tanzania ipo kwa mujibu wa sheria na imepewa mamlaka ya kusimamia kuyaendesha na kutoa adhabu au faini kwa kampuni zitakazo kiuka kanuni za uendeshaji na pia kupendekeza  utaratibu wa namna gani makampuni ya michezo hii ya kubashiri yanatakiwa kuendeshwa, pia imepewa mamlaka ya kusajili na kufuta makampuni yatakayo kwenda kinyume na sheria husika.

Ameeleza kuwa Kuwepo kwa bodi hiyo kunatoa unafuu dhidi ya njama ambazo hapo kabla zilikuwa zikiripotiwa sana, kuhusu utapeli uliokuwa ukifanyika na makampuni hayo ya kubashiri dhidi ya wateja wao walio kuwa wana shinda michezo yao.

Ameongeza kuwa  kuwepo kwa bodi kumemaliza tatizo hilo na kila kitu kuanzia kucheza, mpaka hatua ya mwisho zipo kisheria.

Amesema sekta ya Michezo ya kubahatisha mbali ya kuwa ni burudani lakini pia inatoa fursa kiuchumi kwa washindi wanaobahatika.

Amesema mashine za Michezo ya kubahatisha inarusiwa kuwa kwenye nyumba zizopewa leseni kwa ajili shughuli hiyo.

Bodi ya Michezo ya kubahatisha ndo  inahakikisha utaratibu haukiukwi wa uendeshaji ulioelekezwa na mamlaka husika kwa kuzingatia utaratibu wa michezo yenyewe, kuwa kanuni zake zinazingatiwa na mshindi anapo patikana apewe stahiki yake kwa kiwango kile alicho cheza na sio kinyume na hapo.

Share To:

Post A Comment: