Na John Walter-Babati
Shirika la umeme Tanzania katika mkoa wa Manyara limeendelea kuwaunganishia umeme wateja wake kidijitali kupitia huduma mpya ya NIKONEKT.

Ikumbukwe kwa mkoa wa Manyara huduma ya NIKONEKT ilizinduliwa rasmi siku Mei 30 huku lengo likiwa ni kurahisisha huduma kwa wananchi.

Afisa uhusiano na wateja kutoka shirika la umeme Tanzania katika mkoa wa Manyara Marcia Simfukwe amesema huduma ya hiyo ni rahisi na rafiki kwa wateja wao kwani mteja ataweza kutuma maombi ya maunganisho Mapya bila kufika ofisi za TANESCO.

Huduma hiyo inapatikana kupitia simu ya mkononi kwa njia ya kupakuwa app ya NIKONEKT au kwa kubonyeza *152*00# na kwenye website yao.

Share To:

Post A Comment: